Tafuta

Hali hii kiurahisi  ya virusi vya corona haitabiriki na wala kushikia kwa maana hiyo tusichezee maisha ya watu wetu, kwa sababu kila maisha ni matakatifu Hali hii kiurahisi ya virusi vya corona haitabiriki na wala kushikia kwa maana hiyo tusichezee maisha ya watu wetu, kwa sababu kila maisha ni matakatifu 

Congo DRC#coronavirus:Askofu Ambongo akosoa hatua mbadala!

Kardinali wa Congco DRCkwa maoni yake katika nchi hiyo ni kufungwa moja kwa moja kwa shughuli zote katika mji ndiyo ingekuwa suluhisho la kuweza kuzuia maambukizi zaidi ya janga hili lisilo tabirika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tusichezee maisha ya watu wetu ndiyo kilio cha Kardinali  Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Kinshasa, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika ujumbe wake akikosoa hatua mbadala zilizowekwa katika mji mkuu kufuatia na  dharura ya virusi vya corona. Kwa mujibu wa Kardinali, viongozi wa raia hawatendi vema kuhusiana na dharura ya kiafya.  Askofu katika ujumbe wake amesema, “Hali hii kiurahisi  ya virusi vya corona hatabiriki na wala kushikika kwa maana hiyo tusichezee maisha ya watu wetu kwa sababu kila maisha ni matakatifu”. Amebainisha Kardinali.

Aidha ameongeza kwa maoni yake kwamba kufungwa moja kwa moja kwa shughuli zote katika mji wa Kinshasa ndiyo ingekuwa suluhisho la kuweza kuzuia angalua maambukizi ya janga hili lisilotabirika.

Kwa mujibu wa Kardinali anasema kwamba inapaswa zichukuliwe hatua za dharura kwa kufanya yapatikane mahitaji msingi kama vile: kwa wenye kuhitaji zaidi, kuruhusu maji ya bure na umeme pia kufuatilia upandishaji hovyo wa bei  za bidhaa muhimu kwa watu.

Kardinali Ambongo Besungu hali kadhalika anawasihi  watu wote pia kufuata kwa kina hatua zote na sheria zilizowekwa na  mamlaka na  kutoa wito wa kuwa na mshikamano, hasa kwa upande wa maskini.

01 April 2020, 10:28