Tafuta

Vatican News
Kardinali PHILIPPE OUEDRAOGO Askofu mkuu nchini Burkina Faso amewaandikia wanajimbo wake na watu wote wa Mungu kuwashukuru kwa sala zao kutokana na kuambukizwa na Corona. Kardinali PHILIPPE OUEDRAOGO Askofu mkuu nchini Burkina Faso amewaandikia wanajimbo wake na watu wote wa Mungu kuwashukuru kwa sala zao kutokana na kuambukizwa na Corona. 

Burkina Faso#coronavirus:Ujumbe wa Kard.Ouedraogo kwa wagonjwa wa Jimbo lake na marafiki wote!

Kardinali Ouedraogo Askofu Mkuu wa Ouagadougou,nchini Burkina Faso amewatumia ujumbe wanajimbo kuu na marafiki wote mara baada ya kuambukizwa na virusi vya Corona.Anawashukuru wote kwa ukaribu ambao wanamuonesha katika kipindi hiki cha majaribu.Anatoa mateso yake kwa kipindi hiki kwa wagonjwa wa covid-19 na wenye shinda nyingine na kwa ajili ya amani nchini mwake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Philippe Ouedraogo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Ouagadougou,  nchini Burkina Faso ameandika ujumbe wake kwa wanajimbo kuu lake na marafiki wote kuwajulisha kuwa tarehe 30 Machi 2020 alipokea matokeo ya vipimo kutoka kwa madaktari alivyokuwa amefanya masaa 48 kabla na kuonyesha matokeo chanya ya kuambukizwa na virusi vya Corona. Kwa maana hiyo amesema kwamba  ameungana na umati mkubwa wa wagonjwa katika mapambano duniani kote kutafuta namna ya kutibiwa. “Haya hayatokei  kwa wengine tu! Amesema Kardinali.

Kardinali Philippe Ouedraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, katika ujume wake alioulekeza kwa wanajimbo lake lakini hata kwa marafiki wakristo na wasio, umetangazwa katika tovuti ya Baraza la Maaskofu nchini humo. Kardinali ameshangazwa sana  kwa idadi kubwa ya vielelezo vya mshikamano na huruma mbele yake. Katika ujumbe huo pia anatoa shukrani ya kina kwa wote ambao katika ugonjwa huu wameweza kuwa karibu, kuweza kumtunza, wahudumu wa jimbo kuu, maaskofu, ubalozi wa kitume, watawa na hasa madaktari ambao wametenda kadri ya uwezo wao na taaluma yao.

Aidha anabainisha kwamba wengi wamejionesha kuwa hai, ndugu, marafiki, na wajuani kutoka kwa kila dhehebu, kwa njia ya simu na ujumbe mfupi, anaandika Kardinali, huku akiwashauri kuandaa novena za sala kwa ajili ya uponywaji. Kama Yesu Kristo aliyetoa maisha yake juu ya Msalaba, kwa ajili ya wokovu wa dunia, kwake Yeye na baada Yake,  Kardinali anasisitiza, kuwa naye  anatolea  kwa upendo wake katika kipindi hiki cha majaribu hasa katika sala yake ya kila siku  kwa yoyote aliye na ugonjwa wa Covid-19 au aliye na usumbufu wa magonjwa mengine; kwa ajili ya kusitisha kila aina ya mauaji ya wasio na hatia kwa upande wa nguvu za ubaya; kwa ajili ya upatanisho, haki na amani nchini Burkina Faso.

Kardinali Ouedraogo ameongeza kuandika kwamba kama usemavyo msemo wa wahenga wa kiafrika “ ‘unga haukusanywi kwa kidole kimoja’ na mbele ya mahitaji ya dharura ya zana ili kusaidia maisha ya watu wengi, waliokumbwa na virusi vya corona, tuungane wote katika mapambano ya janga hili lisilosemekana la virusi ambavyo vinaonekana katika afya ya watu, kwa ngazi ya uchumi kijamii, kiutamaduni na kiroho.”

“Katika kipindi hiki cha Kwaresima  kilichojikuta ndani ya janga la virusi vya corona, tumkabidhi Mwalimu wetu ambaye hatuachi kwamwe kwani pamoja naye tutafikia ushindi”. Amehitimisha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Ouagadougou, nchini Burkina Faso.

09 April 2020, 09:49