Tafuta

Vatican News
Jumapili Mosi Machi, Maaskofu wa Nigeria walifanya maandamano ya amani kwa ajili ya kupinga kila aina ya vurugu dhidi ya makundi ya kigaidi ya Boko haramu.Wote walivaa nguo nyeusi. Jumapili Mosi Machi, Maaskofu wa Nigeria walifanya maandamano ya amani kwa ajili ya kupinga kila aina ya vurugu dhidi ya makundi ya kigaidi ya Boko haramu.Wote walivaa nguo nyeusi.  (AFP or licensors)

Nigeria:Maandamano ya maaskofu dhidi ya vurugu za Boko haramu!

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Nigeria Askofu Augustine Akubueze, ameongoza maandamano ya kupinga vurugu na kutumia nguvu kwa upande wa makundi ya magaidi wa Boko haramu.Ameshutumu vikali shirikisho la serikali hiyo kukosa kuhakikisha kwa kiasi kikubwa usalama wa watu kwa namna ya pekee wa wakristo ambao kila siku ni kuonekana vifo,uvamizi wa nyumba na watu,makanisa,misikiti,seminari na kutekwa nyara.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maandamano ya amani yamefanyika Jumapili tarehe Mosi Machi na maaskofu wa Nigeria katika mji mkuu Abuja. Kwa mujibu wa taarifa mahalia, maaskofu walikuwa wamevaa nguo za msiba ambao wameweza kuandanamana katika barabara kwa jina karibia la “wanaigeria milioni moja wa imani ya kikristo, nusu yao wakiwa ni wakatoliki”. Aliyeongoza maandamano hayo ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Nigeria Askofu Augustine Akubueze, ambaye ameshutumu vikali shirikisho la serikali kukosa kuhakikisha kwa kiasi kikubwa usalam wa watu kwa namna ya pekee wa wakristo, mbele ya kuongezeka kwa utumiaji nguvu kwa upande wa makundi ya kigaidi ya Boko Haramu.

Askofu Akubueze amekuwa ni msemaji mkuu wa wanaigeria ambao wamechoka kabisa na serikali kushindwa kusitisha magaidi hao. “Uuaji wa watoto wa Mungu ni ubaya mkubwa sana, ukosefu wa ulinzi kwa watu wasio kuwa na hatia dhidi ya mashambulizi ni ubaya mkubwa sana; ukosefu wa kufuatilia magaidi ni ubaya sana”. Kuna makaburi mengi ya wimbi la watu, kuna utekaji nyara mwingi, uvamizi wa nyumba na  wa watu, maeneo matakatifu kama vile makanisa, misikiti na seminari na kwamba ukimya wa serikali  ni sawa na kupitishwa kwa vitendo hivi vya kihalifu na pia askofu kukumbuka kuhusu majibu dhaifu yaliyotolewa na  viongozi wa serikali wakati wa  kifo cha Mchungaji Lawan Andimi aliyeuawa tarehe 20 Januari  2020.

Hata hivyo wito wa askofu huyo unafuata ule wa Mahubiri ya Askofu Mkuu Iginatius Kaigma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wao Mwaka wa Baraza la Maaskofu Nigeria hivi karibuni kabla ya kufanyika tukio hili la maandamano, ambapo alikuwa amesema kuwa: “ hatuwezi kujifanya kuwa kila kitu kinakwenda vizuri nchini Nigeria, hivyo sala zetu ziweze kwa hakika kusikilizwa ili kuondoa kabisa ubaya katika ardhi yetu iliyojaa damu ya raia wasio na hatia”.

04 March 2020, 14:43