Katika Mkutano wa Maaskofu nchini Uswiss wametoa taarifa juu ya kutaka kukarabati jengo la Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Papa kutoka Uswiss mjini Vatican ifikapo mwaka 2026 Katika Mkutano wa Maaskofu nchini Uswiss wametoa taarifa juu ya kutaka kukarabati jengo la Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Papa kutoka Uswiss mjini Vatican ifikapo mwaka 2026 

Uswiss:Maaskofu wataka kusadia vijana wakimbizi kati ya Ugiriki na Uturuki!

Maaskofu katoliki nchini Uswiss wanaunga mkono kuhusiana na suala la ufunguzi wa mikondo ya kibinadamu pia wametangaza kuhusu kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia vijana wahamiaji kwa namna ya pekee Ugiriki na Urutuki.Hatimaye wanaonesha nia ya kutaka kukarabati Jengo la Kikosi cha Ulinzi na Usalama Vatican kutoka Uswiss kufika 2026.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hali ya wakimbizi mpakani kusini mwa Ulaya kwa namna ya pekee kati ya Ugiriki na Uturiki, inatisha na kutoa wasi wasi wa kina kama ilivyooneshwa na Baraza la Maaskofu nchini Uswiss  (Ces),  katika taarifa yao ya mwisho wa Mkutano mkuu wa 327 uliofanyika kuanzia tarehe 2-4 Machi 2020, jijini Geneva. Katika  Hati yao  ya mwisho kwa mujibu wa Shirika la Habari la Cath, Maaskofu wanaunga mkono  pia hata suala la ufunguzi wa mikondo ya kibinadamu na vile vile wametangaza kuhusu kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia vijana wahamiaji.

Kwa hakika Baraza la Maaskofu wametoa uamuzi wa kusaidia kiuchumi Mpango wa kanisa Katoliki la Kiarmeni huko Ugiriki, unakita kusaidia watu wenye matatizo, na wenye umri kuanzia miaka 18-30 na wanaweza kufuatiliwa zidi kwa mwaka mmoja kwa Kanisa hili. Kwa mujibu wa maaskofu wa Uswiss wanabainisha lengo la kutaka kusindikiza changamoto za dunia katika upyaisho wa Kanisa kwa ngazi ya kitaifa hasa katika kujadiliana na waamini wake.

Kiini cha tafakari yao pia kimegusia Wosi wa Kitume baada ya Sinodi wa Papa Francisko “Querida Amazonia” na “ndoto” zake nne zilizoelekezwa na Papa ikiwa ni ile ya kijamii, kiutamaduni, kiekokojia na kikanisa. Kadhalika katika mkutano wao pia waliweza kugusia mpango wa ukarabati wa jengo la  Kikosi cha Ulinzi cha Uswiss mjini Vatican ambapo wanasema kuwa kibali cha kuanza shughuli hiyo  kinatarajiwa kupatikana mwishoni mwa mwaka 2020. Kubomoa kwa kwa jengo la Kikosi cha Uswiss cha Ulinzi  mjini Vatican, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kunatarawajiwa kufanyika kwenye miaka kati ya  2023-2026. Hii ni miaka ambayo inaweza kupelekea mwanzoni mwa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 ya kile kiitwacho  “Sacco di Roma” yaani ‘Gunia la Roma’, kwa maana ya kwamba mwaka 2027 utakuwa mwaka wa  500  tangu walipouwawa kikosi cha Walinzi wa Papa kwa  njia ya mikono ya  jeshi la Charles V, tukio lililofanyika kunako tarehe 6 Mei 1527.

Nafasi pia katika mkutano haikukosekana kugusia suala la dharura ya Virusi vya Corona (Covid-19) mahali ambapo Baraza la Maaskofu, Uswiss wanaalika watu wote wasiangukie katika hali ya kuchanganyikiwa na hivyo watunze utulivu kwa kuweka matumaini kwa Bwana. Na ili katika kuweza kuzuia maambukizi yasienee zaidi, maaskofu wanaomba hata hivyo kubaki katika kanuni na misingi uliyowekwa tayari na malaka ya raia.  Maelekeo hata hivyo yametolewa kuhusiana na maadhimisho ya liturujia kwa mfano: watu wenye dalili za mafua ya kawaidia wanaalikwa wabaki nyumbani; ugawaji wa ekaristi ufanyike mikononi na wala hakuna kupeana mikono ya amani.

Hatimaye wametoa tarifa kuhusu mhusika mpya wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Ulinzi na manyanyaso yaliyopenyeza katika Kanisa ambapo ni Askofu Urban Federer aliyechukua nafasi ya Askofu Charles Morerod, ambaye amekataa kuendelea na kazi hiyo mara baada ya kuwapo na  uchunguzi unaoendelea wa madai ya unyanyasaji katika Jimbo lake la  Lausanne, Geneva na Friburg.

06 March 2020, 14:35