Tafuta

Vatican News
Port-au-Prince:Kikundi cha madaktari wakipata maelekezo zaidi huko Haiti  kuhusu maambukizi ya virusi vya COVID-19 Port-au-Prince:Kikundi cha madaktari wakipata maelekezo zaidi huko Haiti kuhusu maambukizi ya virusi vya COVID-19 

Haiti:#coronavirus:Janga la corona katika nchi iliyokwisha jaribiwa 2010!

Hakika Janga la virusi vya corona haLIbagui na wala kuchagua,kujali,kuonea huruma,hapana!Ni katika muktadha wa Kisiwa cha Haiti ambacho kwa miaka kumi Iliyopita ilipata pigo la tetemeko la ardhi na kupoteza watu zaidi ya 200elfu.Katika janga hili linawakuta bado watu wengi wanalala nje na makazi duni,huku vituo vya afya ni shida wanakosa kila kitu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Janga la  Covid-19 halibagui utafikiri kutaka kuwa pigo kuu kwa mataifa yote duniani. Lakini katika baadhi ya nchi pigo hili linafanya hali kuwa vibaya sana.Ni katika muktadha wa Kisiwa cha Haiti nchi ambayo bado inaendelea kuona magofu na matatizo ya janga la tememeko,lililowakumba miaka kumi iliyo pita na kusababisha vifo vya watu 200,000 na kuacha madhara mkubwa sana ambayo hadi sasa bado mapengo ni mengi.

Katika hali kama hii, Padre  Renold Antoine, mkuu wa Kanda ya Shirika la Mkombozi (Redentorist) katika kisiwa cha Haiti amesema kwamba wako mbele ya janga lisiloweza kuelezeka. Kwa mujibu wa shirika la habari Katoliki kisiwani humo amenukuliwa Padre akisema, kile kitakachotokea kwa sababu ya janga hilo kitakuwa janga la kutisha, kwa sababu huko wanaishi siku kwa siku na hawana  vifaa muhimu vya kukabiliana na virusi hivi.

Kwa sasa kisiwani Haiti wamerekodiwa kesi karibia nane wenye virusi vya corona lakini Padre Antoine amebainisha kuwa huo ndiyo mwanzo wa janga kubwa zaidi baada lile la kwanza au baadaye litakalowakumba watu wote. Kwa sasa watu wanaishi bado barabarani, tangu janga la tetemeko. Hwana maji safi hata ya kunawa mikono, hakuna umeme katika nyumba zao na hata katika miundo ya majengo ya mahospitalini.

Kwa mujibu wa Padre huyo na ambao wanajikita katika shughuli ya kutoa msaada wa kiroho, hata kwa zana, wanasema baada ya kufunga makanisa  kwa mujibu wa hatua za kisheria ya serikali na kanuni za afya, katika  kuzuia kuenea kwa virusi, Misa zinatangazwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii. Vile vile matenki ya maji safi yanawekwa kwa ajili ya watu ili kuwasaidia kunawa mikono yao.  Pamoja na hayo wapo watu wengi ambao hawajiwezi kabisa na kwamba wanashirikishana chakula kwa watu walio waskini zaidi. Amehitimisha akiomba Bwana kulinda nchi, na zaidi watu wasio kuwa na kitu chochote katika vituo vya afya  na ambavyo havitoshi kukabiliana na shida kubwa kama hiyo.

Ikumbukwe: ilikuwa tarehe 12 Januari 2010 ambapo tetemeko la ardhi liliweza kuikumba kisiwa cha Haiti. Katika harakati ya kutaka kuamka tena imekuwa bado ni vigumu mchakato wa ujenzi na ambao hadi sasa  unaendelea polepole, licha ya kuwapo msaada wa jamumuiya ya kimataifa. Zaidi ya watu 300elfu bado wanaishi katika makazi duni na asilimia 55 ya wakazi wanaishi chini ya dola mbili kwa siku na wana njaa. Katika muktadha huu mgumu, Kanisa linajitahidi kuwa karibu kwa kuhisi uchungu huo kupitia wamisionari wa eneo hilo  kama vile wanashirika wa Camillian Wascalabrini, vile vile wasalesiani, pamoja na Waredentorist ambao bado kwa pamoja wanafungua mikono yao katika kutoa huduma mbali mbali kwenye vituo vya afya na kuwakaribisha idadi ya watu huku wakisaidia hata kujenga upya vijiji katika  nyumba walizohamishwa.

31 March 2020, 12:45