Coronavirus.Jumuiya ya Mtakatifu Egidio:Kikosi cha kazi kuokoa wazee wanaoishi kwenye taasisi.
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kuundwa kwa kikosi kazi cha madaktari na wafanyakazi wa afya kufuatilia hali halisi ya ndani ya taasisi kama vile nyumba za wauguzi na nyumba za kupumzikia wazee na miundo mingine ya ukarimu. Ndivyo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imeomba Serikali na Mikoa baada ya visa vingi vya kutisha vilivyorekodiwa katika siku hizi katika miundo ya amajengo mbali mbali ambayo inatunza wazee. Katika ripoti yake wanasema dadi kubwa ya wenye virusi inaonesha kuwa wafanyakazi wanaosaidia, waathiriwa hawakuwekwa usalama kwa maana hiyo nao wamekuwa waathirika kutokana na ukosefu wa zana muhimu za kujilinda.
Ikiwa haifanyiki hatua hiyo ya ulinzi ni kuingia kwa kile kiitwacho mtandao wa utamaduni wa ubaguzi ambao umeenea sana unakataa hadhi ya usawa na maisha ya watu dhaifu zaidi ambapo matokeo yake yanaweza kuwa ni janga, kama idadi ya waathiriwa kuongezeka, kutokana na aina ya miundo iliyofungwa ambayo wazee wanakaribishwa ndani humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya amaombi ndipo ombi linapendekezwa la kufanyia haraka ili kuuunda kikosi cha kazi kabla hawajachelewa sana kwa wale wanaokaa ndani na wale wanaofanya kazi humo. Kwa haraka sawa na hiyo wanaomba kutumwa kwa vibarakoa, viambukua, vitakasa, mitungi ya oksijeni na vifaa vingine vya matibabu na kinga ambavyo katika miundo hiyo mara nyingi vinakosekana pamoja na utakasaji wa mazingira yaliyo hatari. Aidha amesema hii inaathiri dhamiri ya raia wa nchi ambao kwa hakika hawawezi kushuhudia mauaji ya kizazi na ambao kama wazee wamefanya kazi nyingi katika utamaduni na ustawi kwa ajili ya kizazi endelevu, inahitimisha ripoti.