Tafuta

Vatican News
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaomba ufuatiliaji wa  hali za ndani ya nyumba za wauguzi na nyumba za kupumzika wazee kutokana na hatari ya maambukizi ya corona Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaomba ufuatiliaji wa hali za ndani ya nyumba za wauguzi na nyumba za kupumzika wazee kutokana na hatari ya maambukizi ya corona 

Coronavirus.Jumuiya ya Mtakatifu Egidio:Kikosi cha kazi kuokoa wazee wanaoishi kwenye taasisi.

Jumuiya ya Mtakatifu Francisko imetoa pendekezo kwa serikali na mikoa kuunda kikosi cha kazi cha madaktari na wafanyakazi wa afya ili kufuatilia hali za ndani ya nyumba za wauguzi na nyumba za kupumzika wazee kufuatia na janga la virusi vya corona kushambulia katika baadhi ya vituo hivyo

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuundwa kwa kikosi kazi cha madaktari na wafanyakazi wa afya kufuatilia hali halisi ya ndani ya taasisi kama vile nyumba za wauguzi na nyumba za kupumzikia wazee na miundo mingine ya ukarimu. Ndivyo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imeomba Serikali na Mikoa baada ya visa vingi vya kutisha vilivyorekodiwa katika siku hizi katika miundo ya amajengo mbali mbali ambayo inatunza wazee. Katika ripoti yake wanasema  dadi kubwa ya wenye virusi inaonesha kuwa wafanyakazi wanaosaidia, waathiriwa hawakuwekwa usalama kwa maana hiyo nao wamekuwa waathirika kutokana na  ukosefu wa zana muhimu za kujilinda.

Ikiwa  haifanyiki hatua hiyo ya ulinzi ni  kuingia kwa kile kiitwacho mtandao wa utamaduni  wa ubaguzi ambao umeenea sana  unakataa hadhi  ya usawa na maisha ya watu dhaifu zaidi ambapo  matokeo yake  yanaweza kuwa ni janga, kama idadi ya waathiriwa kuongezeka, kutokana na aina ya miundo iliyofungwa ambayo wazee wanakaribishwa ndani humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya amaombi ndipo ombi linapendekezwa la kufanyia   haraka ili kuuunda kikosi cha kazi kabla hawajachelewa sana kwa wale wanaokaa ndani na wale wanaofanya kazi humo. Kwa haraka sawa  na hiyo wanaomba kutumwa kwa vibarakoa, viambukua, vitakasa, mitungi ya oksijeni na vifaa vingine vya matibabu na kinga  ambavyo katika miundo hiyo  mara nyingi vinakosekana pamoja na utakasaji wa mazingira yaliyo hatari. Aidha amesema hii inaathiri dhamiri ya raia wa nchi ambao kwa hakika hawawezi kushuhudia mauaji ya kizazi na ambao kama wazee wamefanya  kazi nyingi katika utamaduni na ustawi kwa ajili ya kizazi endelevu, inahitimisha ripoti.

30 March 2020, 11:46