Kufuatia na maambukizi ya virusi vya corona, Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana,limefungwa kwa mahujaji. Kufuatia na maambukizi ya virusi vya corona, Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana,limefungwa kwa mahujaji. 

Coronavirus Covid-19:Kanisa kuu la Bethlehemu limefungwa!

Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana huko Bethlehemu limefungwa kutokana na kuzuka kwa kesi ya virusi vya corona katika mji huo.Usimamizi wa Mji Mtakatifu unafuata sheria na kanuni za mamlaka ya Nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufuatia na maambukizi ya Virusi vya Corona, Wizara ya Afya nchini Palestina imeazimia kufungwa kwa makanisa na misikiti kwa siku 14 huko Bethlehemu na Yeriko ikiwa ni pamoja na Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana. Katika mahojiano na Msimamizi wa Nchi Takatifu Padre Francesco Patton anathibitisha kufungwa huko kutokana na kugunduliwa kwa kesi za watu 7 katika Nyumba ya kulala karibu na mji wa Bethlehemu.

Msimamizi wa Nchi Takatifu Padre Francesco Patton amethibitisha hayo akiwa katika karantini ya Konventi ya Mtakatifu Salvatore huko Yerusalemu mara baada ya kurudi nchini humo akitokea Italia kwa sababu alikuwa ameshiriki Mkutano wa Maaskofu kuhusu 'Mediteranea mpaka wa aman'i huko Bari kuanzia tarehe 19-23 Februari 2020.

Padre Patton amesema kuwa, upo uwezekano wa kufunga hata Kanisa la Mtakatifu Caterina linalopakana na Kanisa Kuu kwa mujibu wa mamlaka ya Wizara ya Afya. Hata hivyo watatoa maelekezo mara baada ya kutathimini kwa pamoja na wakuu wa makanisa mengine ya kigiriki- Kiorthodox, kiarmenia na Jumuiya nyingine mbili za Kikristo pamoja na wafransiskani ambao wanashirikiana kulinda Kanisa kuu hilo.

Yote hayo pia yatategemea kutoka kwa mamlaka ya Wizara ya Afya ya nchi ya Palestina na Israeli amsema Padre Patton, kwa maana ameongeza kusema kuwa hadi sasa bado hawajaagizwa kufunga Makanisa na Madhabahu kutoka Wizara ya Afya ya  Israeli. Kwa ajili ya taadhari ya virusi wamezuzuia makundi ya hija kuingia katika mji wa Bethlehemu na Yeriko. Kwa sasa wanatarajia kufunga hata  shule, ofisi mbili za serikali na kusitisha shughuli zote za kimichezo kwa wiki mbili. Katika kukabiliana na zoezi hili la usambaaji wa virusi Isralu imefunga hata ndege zinazotoka Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Austria na Uswiss.

Padre Patton aidha ametoa amesema kwamba kinacholeta matumaini na moyo ni sala kwa maana hata katika Misale ya waamini kuna maombi dhidi ya majanga ya asili, magonjwa na litania inayobaki kuwa halali na ya sasa, isemayo:"tuachiliwe na magonjwa kwa maana hiyo hata magonjwa ya kuambukiza, tuachiliwe na njaa na tuachiliwe huru dhidi ya mabaya na aina zote za dhuluma".

06 March 2020, 11:10