Tafuta

Vatican News
Madaktari na wauguzi therathini kutoka Albania wamefika Italia kuweza kusaidia kukabiliana na janga la corona katika mahospitali mbalimbali. Madaktari na wauguzi therathini kutoka Albania wamefika Italia kuweza kusaidia kukabiliana na janga la corona katika mahospitali mbalimbali.  (ANSA)

Coronavirus:Albania yaikumbatia Italia kukabili dharura!

Madaktari na wauguzi therathini wamefika nchini Italia kutoka nchini Albania kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na dharura ya afya ya virusi vya corona.Tangazo limetolewa na Waziri Mkuu wa Albania,Bwana Edi Rama.Maneno yake ni yenye thamani ya ushirikishano na udugu kati ya nchi hizi mbili na kutoa hisia nzuri ya utambuzi huo kwa watu wengi!

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Mlipuko wa virusi vya corona (covid-19) kwa sasa imezunguka dunia nzima na kufanya kila nchi kuanza kukumbizana katika harakati za kuzuia, kutibu na kushinda matatizo ya kiafya ambayo yanaikumba nchi zote  zenye waathrika waliolazwa hospitalini. Katika hilo, hisia shukrani zimewaendea kwa ishara nyingine tena ya nchi ya Albania ambayo imeamua kutoa msaada wao kwa Italia ili kukabiliana kuzuia na kutibu wagonjwa wa covid-19.

Hawa ni madaktari na manesi therathini  ambao tayari wameshafika nchini Italia katika kusaidia shughuli zote mahospitali mbalimbali ya dharura inayoendelea. Ni ishara ambayo imependezwa na wengi sana na kuwa na utambuzi kwa upande wa watu wa Italia. Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Albania, Bwana Edi  Ramana.

Kwa mujibu wa maoni yake ni kuonyesha shukrani ya ule uhusiano mwema wa kidugu na urafiki kati ya nchini hizi mbili na kukumbusha jinsi gani Tirana mji mkuu wa Albania hauwezi kamwe kusahau msaada uliotolewa kutoka Roma wakati wa kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe kunako mwaka 1990, ambapo wazalendo wengi wa Albania walikimbia vurugu na ghasia wakapokelewa nchini Italia.

Vatican News, akihojiana na Askofu Ottavio Vitale askofu wa Albania  karibu miaka 30 hivi amesema ishara ya Waziri Mkuu wa Albania Bwana Rama ni jambo ambalo ni zaidi ya ishara ya ushirikishano kati ya nchi zilizo karibu. Hii ina maana ya ishara ambayo inawakilisha taadhari kwa Ulaya, ambayo kwa muda huu imekumbwa na matatizo kwa ujumla na ambayo bado hawajaweza kupata suluhisho la pamoja ili kukabiliana na dharura ya covid-19. Ishara kama hizi kwa ujumla Askofu amehitimisha zinapaswa pia zitawale ndani ya mioyo ya wazalnedo wa nchi zote mahalia.

31 March 2020, 09:45