Vatican News
Askofu Mkuu Ettore Balestrero  Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anawashuri maaskofu kuwa wawajibikaji wa majimbo yao katika ulinzi wa watoto. Askofu Mkuu Ettore Balestrero Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anawashuri maaskofu kuwa wawajibikaji wa majimbo yao katika ulinzi wa watoto.  (Vatican Media)

Congo:Maaskofu ni wahusika wa kwanza katika majimbo yao!

Balozi wa Vatican nchini Congo DRC,Askofu Mkuu Balestrero anasema kuwa inahitaji uthabiti mkubwa na kuingilia kati mara tu haki inapokiukwa ya ulinzi wa watoto.Amesema hayo katika semina iliyofunguliwa tarehe 2 Machi 2020 ya maaskofu wa nchi hiyo,ambapo hotuba yake imeangazia Motu Proprio ya Papa Francisko ya tarehe 4 Juni 2016 inayotazama kuhusu ulinzi wa watoto ma watu walioathirika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Balozi wa kitume nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Askofu Mkuu Ettore Balestrero, amefungua hotuba yake katika semina ya tarehe 2 Machi 2020 kwa maaskofu wa nchi hiyo inayohusu ulinzi wa watoto. Kwa kuangaziwa na Waraka wa Motu Proprio wa  Papa Francisko wa tarehe 4 Juni 2016, anasema kama mama mwenye upendo ambao Papa Francisko anauonesha na kutoa zoezi la Kanisa hasa la kulinda watoto na watu wenye kuathirika ameweza kukumbusha tena juu ya zaoezi la Kanisa la Ulimwengu akiwaelekeza wachungaji wa Majimbo.

Askofu Mkuu Balestrero aidha amesisitiza jinsi gani suala hili linapelekea uwajibikaji mkubwa na ustadi kwa upande wa maaskofu ambao katika maeneo yao wanachukua nafasi ya kuwa mahakimu katika kafanya shughuli zao kama makuhani, kwa sababu nafasi ya hakimu daima ina muhuri wa kichungaji. Kwa wakati huo huo Askofu Mkuu anaonesha kwamba inahitaji hata uthabiti mkubwa na kuingilia kati mara moja haki inapokiukwa. Kuheshimu Sheria ya Kanisa ni uhakika wa kutafuta suluhisho na siyo ya pata potea bali ukweli  kwa maana ya kichungaji . Lengo la Semina hiyo amebainisha, ni kujikita kwa undani zaidi katika mchakato wa safari ya usimamizi hasa katika kesi maalum zinazohitaji ustadi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kazi ya Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa Watu.

Hatimaye Balozi ametoa taarifa rasmi kwa maaskofu kuhusu Makubaliano  ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Vatican ambayo yamekita kuweka msimamo wa masuala ya kisheria yanayotoa kanuni ya mahusiano kati ya Nchi mbili katika nyanja ambayo Kanisa kwa namna ya pekee inahusika. Baada ya mchakato wa safari ya miaka 10 ya  mkataba iliyotiwa sahini kunako mwezi Mei 2016 na baadaye kuridhiwa na Bunge la Congo DRC kunako Julai 2018 na sasa hatimaye umeridhiwa tena mnamo tarehe 17 Januari 2020.

06 March 2020, 09:35