Vatican News
Licha ya wasiwasi wa maaskofu wa Congo Drc kuhusu hali halisi ya kisiasa, bado wanapongeza msimamo wa elimu na malipo kwa walimu uhusiano wa kidiplomasia na uhuru wa vyombo vya habari. Licha ya wasiwasi wa maaskofu wa Congo Drc kuhusu hali halisi ya kisiasa, bado wanapongeza msimamo wa elimu na malipo kwa walimu uhusiano wa kidiplomasia na uhuru wa vyombo vya habari. 

Congo DRC:Wasiwasi wa Maaskofu kuhusu mizozo nchini humo!

Maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)wana wasiwasi mkubwa juu ya mivutano ya sasa ambayo wanaendelea kuiishi.Ni kwa mujibu wa ujumbe wa Tume ya Baraza la maaskofu wa Congo mara baada ya kikao cha pamoja kuanzia tarehe 24-28 Februari 2020 ambapo pampja na mambo ya kikanisa pia wametathimini hali halisi ya kisiasa-kijamii katika nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wana wasiwasi mkubwa juu ya mivutano ya sasa ambayo wanaendelea kuishi. Ni kwa mujibu wa ujumbe wa Tume ya Baraza la maaskofu wa Congo DRC waliounganika kwa pamoja kuanzia tarehe 24-28 Februari 2020 ambapo katika mkutano huo wametathimini hali halisi ya siasa kijamii katika nchi hiyo.

Katika mkutano huo wameweza kugusia pia juu ya Kongamano la Tatu le Ekaristi kitaifa litakalofanyika kuanzia tarehe 7-14 Juni 2020 huko Lubumbashi. Kuhusiana na mfumo wa kiserikali, katika ujumbe wao wanabainisha  suala la rushwa, ulimbikizaji mali ya umma, wanalalamiki akuhusu hukosefu wa usalama katika nchi hiyo iliyojaa makundi yenye silaha  kwa namna ya pekee katika wilaya ya Ituri, Kivu kaskazini na kusini. “Haijawahi kuhesabika idadi kubwa ya vifo namna hii kabla ya mwaka mmoja kuisha katika maeneo haya” wamebainisha maaskofu.

Maaskofu, aidha wanaonesha hata matatizo mengine  ya Congo kama vile  ukosefu wa sensa ya watu, kuvamiwa kwa ardhi inayopelekea migogoro kati ya makabila na sehemu ambazo zinaogopwa na kuahirishwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa  na mifumo iliyokuwa imekubaliwa, licha ya ombi lililokuwa limezinduliwa na Baraza la Maaskofu  na Kanisa la Kristo huko Congo ambao waliweza kukusanya mamilioni ya sahihi. Hata hivyo pamoja na hayo yote maaskofu wanapongeza serikali kwa kuanzisha mambo mengine kwa mfano juu ya ufundishaji wa bure na malipo kwa ajili ya walimu.  Wanashukuru uboreshaji wa hali ya kisiasa na huru wa nafasi za vyombo vya habari, pia, kwa kidiplomasia, na kwamba Congo imepata nafasi yake katika uwanja wa kimataifa pia kuhusu mkataba wa Vatican ambao ni kwa manufaa ya watu wa Congo.

Ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la  Maaskofu unamalizika kwa kutoa ushauri  kwa Rais wa Jamhuri  ili kuendelea na juhudi za kuirudisha  amani katika maeneo yenye ishara za kutokuwa na usalama; kwa wale ambao wamechaguliwa wanapaswa waweze kushiriki mateso ya dhati  na matarajio ya kina kwa ujumla wa watu; kwa watawala wote wanapendekeza kuwepo na marekebisho muhimu, hasa katika uwanja wa mahakama;  Na kwa jamii ya kimataifa wanaomba wasaidie Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kupata suluhisho la kudumu dhidi ya mikasa hiyo na iweze kutatuliwa. Hatimaye maaskofu wanawageukia watu wa Congo Drc wakiwasihi  waweze kukuza mshikamano, uvumilivu na majadiliano  baina ya jamii kwa ajili ya upatanisho na amani katika kesi za migogoro. “Wananchi wanatarajia, kutoka kwenye muungano  hadi madarakani, uboreshaji wa hali ya maisha. Hii inaweza kutokea tu kutokana na mabadiliko ya mioyo yetu, akili zetu na mazoea yetu”. Wanahitimisha.

03 March 2020, 14:21