Tafuta

Vatican News
Wasafiri wanameshaanza kujikinga kufuatia na kesi ya kwanza ya virusi vya corona katika uwanja wa ndege wa Phnom Penh nchini Cambodia. Wasafiri wanameshaanza kujikinga kufuatia na kesi ya kwanza ya virusi vya corona katika uwanja wa ndege wa Phnom Penh nchini Cambodia. 

Cambodia:Virusi vya Corona,COVID-19:kuweni kidete katika imani!

Hofu ni kubwa pia imewafikia hata mji wa Cambodia baada ya kuthibitiswa kesi ya COVID-19 kwa msafiri aliyekuwa kwenye Meli ya kitalii ambayo ilikuwa na wasafiri 1200.Msimamizi wa Kitume nchini humo anatoa taarifa kuwa kwa sasa ni kipindi kigumu kwa wote,kipindi hiki ni cha kujitoa sadaka kwa wote.Tunaalikwa kuunganika katika sadaka ya Kristo katika Mateso yake kwa njia ya kupokea ekaristi kwa tamaa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Virusi vya Corona vimeingia hata  Cambodia. Kesi zimethibitishwa hadi sasa japokuwa  bado inabaki dharura  kubwa kuhusiana na wasafiri zaidi ya 1200 waliokuwa kwenye meli ya kitalii ya Marekani (American Westerdam), iliyowasiri siku za karibuni katika forodha ya Sihanoukville, mahali ambapo wanasema inawezekana mwanamke mmoja akawa amewaambukiza kwa maana  alikuwa anasafiri nao na ambaye alipatikana na  “Covid-19”.  Waziri wa Afya nchini humo ameweka kwa haraka utaratibu na sheria za usalama kwa kuzuia mikusanyiko. Vile vile Makanisa yameweza kuchukua hatua ya kuwatangazia waamini kuacha misa za makanisani na badala yake maadhimisho yafuatiliwe mbashara na mitandao ya kijamii.

Zaidi ya hayo tarehe 19 Machi  2020 , Makao makuu ya kitume ya ya Phnom Penh, inayoongozwa na Askofu Olivier Schmitthaeusler, aliunda makusudi Tume ya Kichungaji iliyopewa jina  “Covid-19” ili kuelezea waamni kihusu hatua mpya ya kuzuia maambukizi. Tume hii iliwakilishwa na barua ya kuchungaji ya Askofu Schmitthaeusler. Katika barua hiyo iliyotangazwa kwa umma na shirika la habari za  Kanisa la Asia anaandika: “Mwaka huu  safari yetu kueleka Pasaka ni njia ya Msalaba kwa ajili ya dunia nzima kutokana na kusambaa kwa haraka kwa virusi vya Corona. Wasi wasi ni mkubwa unatukaba kooni  kwa sababu ya waathirika na kipeo kikubwa cha uchumi duniani ambacho kinaweza kusababishwa na tukio hili na ambacho kinaweza kweli kupelekea matokeo ya wakati ujao kuwa mbaya hasa kati ya watu masikini na wenye kuhitaji sana.

Wito katika kipindi hiki cha kwaresima ni kwamba wasifunge mioyo bali wasali kwa ajili ya Nchi, kwa ajili ya Kanisa, familia na dunia nzima! “Kwa sasa ni kipindi kigumu kwa wote, kipindi hiki ni cha kujitoa sadaka kwa wote. Tunaalikwa kuunganika katika sadaka ya Kristo katika Mateso yake kwa njia ya kupokea ekaristi kwa tamaa. Askofu Mkuu Schmitthaeusler aidha amefafanua juu ya kusitisha maadhimisho yote ya umma hadi hapo watakapotoa taarifa kutokana na hali na mazingira ya wakati huu, ambapo nchi nyingi zinapambana dhidi ya Virusi vya Corona, COVID-19!

Shughuli nyingi zinabaki katika muungano wa kiroho na Kristo na kati ya waamini kwa ajili ya kusaidiana mmoja na mwingine ili kupeleka msaada katika dunia yenye matatizo kwa njia ya sala zetu. Waamini wanakumbushwa kushiriki misa kiroho kwa njia mubashara kupitia kurasa za Facebook na YouTube, na kwati huo huo hata sala ya rosari kila siku na mwaliko wa kuwasha mshumaa katika dirisha ili mwanga wa Yesu kweli uweze kuwangaza dunia na kuiponya. Kwa njia ya vyombo vyote vya mawasiliano ya kidigitali, masomo yote ya liturujia za siku, nia za maombi kwa ajili ya kuwasindikiza waamini vinapatikana.

Kipindi hiki cha sala kitaruhusu kuwa katika muungano na Kanisa la Ulimwengu, duniani na kusali kwa ajili ya wote waliopatwa na mkasa huu wa virusi vya Corona na kwa ajili ya amani duniani,  anaandika Msimamizi wa kitume Schmitthaeusler. Aidha anwaomba makuhani na wahusika wote wa Kanisa  ili  kuwatia moyo wanaparokia wao kwa njia ya simu, vipaza sauti na kengele za saa 6 mchana na saa 12 kamili jioni kwa kuwakumbusha watu wote kuwa Mungu yupo pamoja nasi. Makanisa yatabaki wazi kwa ajili ya sala binafsi. Sakramenti ya ubatizo, ndoa vimesitishwa wakati huo mazishi yatafanyika na wana familia tu nchini humo. Na kufuata na maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu ya  Pasaka taarifa zitatolewa baadaye.

Msimamizi wa kutume Monsinyo Schmitthaeusler anahitimisha akiwashukuru  wote kwa msaada na sadaka zinazotolewa na jumuiya: “kwa sasa tunahitaji kuliko wakati mwingine mioyo yenu kama wachungaji, kwa mfano wa sura ya moyo wa Mungu”. Aidha wanawageukia watoto na vijana ambao shughuli zote za parokia na shule zimesimamishwa, ya kuwa  Ofisi za kichungaji kwa vijana na Elimu katoliki vitabaji kuwa karibu nao kwa njia ya vyombo vilivyopo vya kijamii na hivyo anawatia moyo ili wasali na kujisomea wakati huu ambao wamelazimika kukatisha masomo yao na kuwa nyumbani. Na kwa waamini wote anasema Mungu yuko katikati yao mahali palipo na giza, hivyo wafuate kweli sheria na kanuni zilizowekwa na wizara ya afya ya nchi. Hii ni katika kusaidiana mmoja na mwingine hasa kwa kuzingatia wenye kuathirika sana  kama wazee, wagonjwa na amaskini; “Katika kipindi hiki kigumu tubaki kidete, tuungane zaidi pamoja na kwa matumaini ya Mungu mwenyezi.

 

21 March 2020, 14:59