Mvua zinazidi kunyesha Kusini mwa Tanzania na kusababisha mafuriko.Askofu wa Lindi anaomba msaada kwa ajili ya waathirika Mvua zinazidi kunyesha Kusini mwa Tanzania na kusababisha mafuriko.Askofu wa Lindi anaomba msaada kwa ajili ya waathirika 

Tanzania:Askofu wa Lindi,aomba msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko!

Tangu mwisho wa mwezi Januari mwaka huu,mvua zinaendelea kunyesha Kusini mwa Tanzania na mikoa mingine na kusababisha mafuriko.Kufuatia na hili,Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi anaomba msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Hali ni mbaya sana kuhusiana na hali ya hewa nchini Tanzania mahali ambapo tangu mwishoni mwa mwezi Januari, mvua zimeendelea kunyesha kwa nguvu na kusababisha mafuriko katika maeneo ya Kusini Mashariki mwa Nchi na kwa namna ya pekee katika Mkoa wa Lindi, Mwanza, Morogoro na Manyara. Takwimu sahihi bado hazijatolewa, lakini wanakadiria kuwa karibu watu 21 wamekufa au kupotea wakati huo huo mafuriko hayo kusababisha watu 21,000 kurundikana kwa pamoja. Kufuatia na tukio hili, Askofu Bruno Pius Ngonyani wa Jimbo Katoliki la Lindi ametoa tamko la nguvu, huku akiomba msaada na zaidi kuhamasisha Caritas mahalia, watu wenye mapenzi mema, viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya serikali ili kuweza kuingilia kati kusaidia waathirika wa mafuriko hayo.

Baadhi ya maeneo ya Tanzania  kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (Amecea), hayawezi kuingilika kwa sababu mvua bado zinaendelea na kuaharibu miundo mbinu kwa upande wa barabara au njia. Shule zimegeuka kuwa ndiyo makazi ya kuwapokea watu kwa muda na kusababisha kukatisha shughuli za mtaala wa masomo.  Majengo ya afya na madawa haviwezi kupatikana au kuwafikia watu ambao wamekumbwa na mafuriko hayo. Madhara makubwa hata yanatazama sekta ya kilimo kwa uharibifu wa hekari 495 ikiwemo hata mazao. Kwa sasa hakuna chakula na mbegu na baadhi ya maeneo yaliyo na maji yaliyotuama yanaonesha kuchafuka sana ambapo uwezekano wa mlipuko wa magonjwa ni mkubwa sana

Hata hivyo kufuatia na mvua zinazoendelea katika mikoa kadhaa nchini Tanzania, Jumatatu tarehe 2 Februari 2020, magari ya mizigo na mamia ya abiria waliokuwa wakisafiri kwenda  au kutoka mikoa ya Morogoro na dodoma wamekwama njiani mara baada ya daraja la Kiyegeya eneo karibu na Gairo Kusombwa na maji.

03 March 2020, 10:27