Tafuta

Vatican News
Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa  Lussemburg  na Mwenyekiti wa Tume ya Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece), Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Lussemburg na Mwenyekiti wa Tume ya Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece),  (Archeveche de Luxembourg / SCP)

Kard.Hollerich:Ikiwa Umoja wa Ulaya haufanyi kitu,Kanisa liwe sauti ya kinabii na kuzindua dhamiri ya Ulaya.

Nje ya Mkutano kuhusu mediteranea mpaka wa amani,Kardinali Hollerich(Comece),amesisitizia juu ya ufunguzi wa mikondo ya kibinadamu ambayo inastahili hata kumwokoa mtu mmoja tu.Uthibitisho unafuatia baada ya barua ya pamoja uliyoandikwa na wenzake wawili wakiomba kwa mara nyingine tena maparokia,jumuiya za kidini,monasteri na madhabahu kukaribisha wakimbizi na wahamiaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mbele ya macho yetu tunaona janga wa wakimbizi. Tunawaona katika visiwa vya Ugiriki na Libia ni aidu kwa bara la Ulaya. Sisi tunazungumza sana juu ya maadili ya Ulaya lakini tunasahau utimilifu wake linahitajia suala la kusaidia. Amesema hayo Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa  Lussemburg  na Mwenyekiti wa Tume ya Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece), alipokutana na waandishi wa habari huko Bari asubuhi tarehe 21 Februari 2020, nje  ya Mkutano kuhusu 'Mediteranea mpaka wa amani'.

Uthibitisho wa Kardinali unakuja baada kutangazwa kwa Barua waliyo itume kwa Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya, pamoja na Kardinali Konrad Krajewski, msimamizi wa Sadaka ya Papa na Kardinali  Michael F. Czerny,  Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya binadamu huku wakiomba kwa mara nyingine tena maparokia, jumuiya za kidini, monasteri na madhabahu, Ulaya nzima kukaribisha angalau hata mkimbizi na mhamiaji mmoja kama moja ya  kuunga mkono ule  mpango wa mikondo ya kibinadamu.

Kardinali  Hollerich kuhusiana na barua hiyo anasema “ sijuhi barua hii itapokelewa vipi katika majimbo yetu, maparokia yetu, lakini nimeona tayari kuwa kuna dalili kwani  nimepokea  barua pepe  kutoka upande wa wanasiasa wengi ambao wanaomba kuwa na mawasiliano". Aidha amesema " Inabidi kuwa watu halisi,  lakini hata kwa kuokoa mtu mmoja ni muhimu kufanya”. Hata hivyo mwaka jana Kardinali alikuwa ametembelea wakimbizi waliokuwa wamezuia katika kisiwa cha Lesvos hivyo anasema “ hatuwezi kuacha kisiwa cha ugiriki na Nchi nyingine peke yao, katika matatizo haya. Kanisa kwa njia ya Caritas ya Ugiriki, wanafanya kazi kubwa sana lakini bado hiyo haitoshi kutokana na watu kuwa wengi".

Kadhalika Askofu Mkuu amesema, "ikiwa tunaweza kufungua mikondo ya kibinadamu, inawezekana kabisa kusaidia kutuliza mateso hayo kwa watu". Kufuatana hilo ametoa wito kwa serikali zote ili ziweze kushirikiana kwa dhati  na mpango huo. Wito pia anauelekeza kwa Umoja wa Nchi za Ulaya ili wachukua angalau sera za kisiasa za pamoja zinazofanana kama chombo kile cha Mkataba wa Dublin ili kusaidia watu na kutekeleza wito kwa uaminifu wa Injili. “ Tunataka kutoa wito hata kwa sera za siasa zote ili kupambana na sababu za uhamiaji pia kufanya jitihada kwa ajili ya amani, hadhi ya kibinadamu,na uhuru wa dini”.  Hizi ni hali ambazo zinaunda kwa hakika na ulazima huo,  kwani wote tunayo haja ya kuwa na haki ya kubaki katika nchi mahalia. Ikiwa Umoja wa Ulaya haufanyi kitu, Kanisa lazima liwe sauti ya kinabii na kugeuka kuwa dhamiri nafsi ya bara la Ulaya.

22 February 2020, 15:38