Vatican News
Mji wa Bari unamsubiri Papa Francisko tarehe 23 Februari 2020 Mji wa Bari unamsubiri Papa Francisko tarehe 23 Februari 2020 

Furaha ni kubwa huko Bari ya kumpokea Papa Francisko!

Maandalizi huko Bari yanapamba moto kwa mujibu wa Padre Vincenzo Corrado, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu wa Italia CEI na kwamba wako tayari kabisa kumpokea kwa shangwe kuu.Papa anatarajia kuadhimisha misa ya kufunga Mkutano unaongozwa na Mada“Mediteranea mpaka wa amani” tarehe 23 Februari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika maandalizi ya kumpokea Papa Francisko siku ya Jumapili tarehe 23 Februari 2020 huko Bari, katika fursa ya kufunga Mkutano wa Baraza la Maaskofu, Italia CEI wakiongozwa na mada ya “Mediterranea  mpaka wa amani”, Padre Vincenzo Corrado, Mkurugenzi wa ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu wa Italia CEI anasema wako tayari kabisa kumpokea Papa kwa shangwe kuu.

Katika njia ya Vittorio Emanuele II wako wanajiandaa kumalizia jukwaa kwa ajili ya maadhimisho ya Papa Francisko wakati wa kufunga mkutano  huo katika mkoa wa Puglia kwa mara nyingine tena mkutano uliopendekezwa na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia  Kardinali Gualtiero Bassetti, ili  kutafakari kwa kina kuhusu maisha endelevu ya makanisa ambayo yanapakana na Bahari ya Mediteranea.

Masuala haya yanayo tazama Kanisa la sasa, ni kuhusu matatizo ya kweli lakini vile vile hata kuwa na matumaini. Kuna dhamana mbili  ambazo ni kitovu cha Utume wa Maaskofu kwenye mkutano huo wa Bari. Na kwa sasa Padfre Corrado amesema kuwa karibia watu 60 hivi kutoka katika nchi 20 tofauti ambao wanafika kufanya  mkutano unaonza tarehe 19 Februari. Na wakati huo huo mji kwa hakika unapumua hali halisi ya subira  na siku kuu kwa ujumla. Watu wanapita na kuona huku wakitafakari tukio hili la maandilizi. Hata hivyo si tu subira, lakini subira kubwa kwa ajili ya Papa Francisko ambaye atafika kuhitimisha siku hizi tatu za kina na kuwatia moyo maaskofu ili kuendelea na mchakato wa safari ya ujenzi wa kweli wa amani.

Watakao sikiliza hotuba ya Papa Francisko Dominika tarehe 23 Februari wanatarajiwa kufika mamia elfu ya waamini, mapadre na mashemasi zaidi ya 500, watawa wa kike na kiume 600. Aidha ni tukio linalitazamiwa kuwaona watu 500 wa kujitolea na ushiriki karibu wa wahudumu 400 wa mawasiliano. Kwa wastani ni idadi kubwa na ambayo Padre Corrano anaamini kwamba ni eneo ambao kwa kawaidia limezoe kuwa na ukarimu na hata kuwafanya wahisi joto hilo la ukarimu wanaofika.

19 February 2020, 14:43