Mkutano wa 20 wa AMECEA utafanyika jijini Dar es Salam, Tanzania kunako 2022! Mkutano wa 20 wa AMECEA utafanyika jijini Dar es Salam, Tanzania kunako 2022! 

Tanzania:Zinaanza mbio kuelekea Mkutano wa 20 wa AMECEA,2022!

Nchi ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Afrika Mashariki AMECEA uliopangwa kufanyika kunako mwaka 2022.Ni tamko lililotolewa baada ya kuhitimishwa kwa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania(TEC)hivi karibuni.Mara ya mwisho mkutano huo ulifanyika jijini Addis Abeba,Ethiopia 2018.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) uliopangwa kufanyika kunako mwaka 2022. Tangazo hilo limetolewa wakati wa hitimisho la mkutano wa kwanza wa uongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, TEC uliofanyika hivi karibuni. Shirikisho la AMECEA linajumuisha wawakilishi kutoka Eritrea, Ethiopia, Sudan / Sudani Kusini, Uganda, Kenya, Malawi na Zambia, pamoja na washirika wa Jibouti na Somalia na, ikiwemo Tanzania yenyewe.

Katika hatua ya kwanza ya ajenda, ufafanuzi wa bajeti wa mkutano wa mwaka umebainishwa kwa  maneno ya Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania akiwaaalika kuandaa miundombinu, nyumba na juu ya  maadhimisho ya liturujia ambazo zitafanyika wakati wa shughuli ya mkutano huo. Mkutano mpya wa maandalizi unatarajiwa kufanyika tarehe 7 Februari 2020.

Hata hivyo hapo awali kunako tarehe 20 hadi 24 Januari 2020, mkutano wa Sekretarieti ya AMECEA ulifanyuka Nairobi  ambapo uliodhuliwa na washiriki kutoka Idara nne za Shirikisho hili zikiwa ni : Idara fedha na Utawala; Maendeleo fungamani ya kibinadamu; Mawasiliano ya kichungaji na kijamii.  Katika ajenda ya 2020 pia ilikuwa ni kwa ajili ya kuweka mwamko kwa jumuiya ndogo ndogo za kikristo kwa namna ya pekee katika maeneo yaliyo na wahamiaji; kuongeza jitihada za mapadre na shughuli za uchungaji kwa ajili ya vijana; utekelezaji wa mipango ya kulinda watoto; juu ya miito; uchapishaji na usambazaji wa nyenzo za habari kwa waamini.

Aidha kwa kuongezea wataangalia utumiaji wa majukwaa ya kidijitali kwa ajili ya uinjilishaji na uboreshaji wa mtandao wa habari wa Signis kupitia ushiriki thabiti wa Makanisa yote mahalia”. Hatimaye pia ni kuhusu msaada wa shughuli za amani katika nchi ya Sudan Kusini; utekelezaji wa Wosia wa “Laudato si” wa Papa Francisko kuhusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja na uzinduzi wa mtandao wa mihimili ambayo inafanya kazi ya kulinda kazi ya uumbaji, ndani ya kanda nzima ya AMECEA.

Katika mkutano huo pia walionesha kuwa AMECEA  inakabiliwa na changamoto mbili kwa namna ya pekee ya ndani na nje ambazo zinapaswa zikabiliwe mwaka huu ni kuwa: “kwa ngazi ya ndani, ni ile ya kuandaa na kupanga upya na uboreshaji wa mifumo ya kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za michango, pia kutumia fursa hiyo kuorodhesha maktaba ya Sekretarieti, ambayo sasa imemalizika”. Na kwa ngazi ya nje “changamoto ni ile ya kuunda kiungo cha ofisi ya kikanda ambacho kitasaidia kupokea na kuwakilisha habari za moja kwa moja kutoka mikutano ya Baraza la Maaskofu mahalia”.  Katika ajenda ya 2020 pia ni kwa ajili ya kuwekwa mwamko kwa jumuiya ndogo ndogo za kikristo kwa namna ya pekee katika maeneo yaliyo na wahamiaji; kuongeza jitihada za mapadre na shughuli za uchungaji kwa ajili ya vijana; utekelezaji wa mipango ya kulinda watoto; juu ya miito; uchapishaji na usambazaji wa nyenzo za habari kwa waamini. Kwa kuongezea, wataangalia utumiaji wa majukwaa ya kidijitali

Ikumbukwe kuwa Mkutano wa kwanza wa AMECEA ulifanyika Dar- es Salam Tanzania kunako 1961 na wa mwisho kufanyika ulikuwa 2018, mwenyeji akiwa nchi ya Etiopia katika mji wa Addis Ababa. Katika fursa hii, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana, Paolo Ruffini, aliwatumia ujumbe washiriki wa kazi hiyo akisisitiza juu ya ukaribu wa Vatican kwa Kanisa la Afrika. Ni ukaribu chanya ambao katika kambi za mawasiliano, katika ishara ya kukuza ufunganishwaji na ushiriki.  Urafiki wa karibu pia katika uwanja wa mawasiliano, katika ishara ya ushirikiano unaokua, ufungamanishwaji na mshikamano kati ya vyombo vya habari bila kupuuza nchi za kiafrika zenye ufikiwaji mdogo wa teknolojia za kidigitali.

06 February 2020, 16:21