Tafuta

Vatican News
Serikali ya Italia imezuia tamasha la utamaduni wa " Carnevale" huko Vanezia kufuatia na uenezi wa COVID-19 Serikali ya Italia imezuia tamasha la utamaduni wa " Carnevale" huko Vanezia kufuatia na uenezi wa COVID-19   (ANSA)

Coronavirus:Kanisa nchini Italia liko karibu na watu waliopweke na wazee

Mkurgenzi wa Caritasi wa Milano, Italia , Gualzetti amethibitisha kuhusu mtazamo wa huduma wakati huu wa maabukizi ya virusi vya corona kwamba wanajaribu kubaki wamefungua vituo vyao lakini kwa umakini wa kesi yoyote inayaoweza kutokea. Askofu Ambrosio wa Piacenza anawalika waamini kusali kwa Mama Maria Afya wagonjwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa la Italia linaendelea kushirikiana kwa dhati na uongozi wa serikali  ya Italia ili kuweza kuthibiti usambazaji wa Covid-19. Kwa kufanya hivyo Jimbo la Milano limeamua kuacha Makanisa wazi japokuwa katika vituo mbalimbali vya usikivu na mikutano isifanyika wakati huo huo mazishi na misa za ndoa zinaweza kuadhimishwa lakini kwa kuudhuriwa na watu wachache wa kifamilia tu. Kadhalika linahahidi kutoa msaada na kuwa karibu na watu walio na upweke na wazee katika kipindi hiki maalum.

Hata hivyo Mamlaka nchini Italia imefuta pia utamaduni wa tamasha maarufu lijulikanalo  kama “Carnevale” katika mji wa Venezia “Venice”. Hili ni tamasha ambalo hufanyika kabla ya kuanza kipindi cha Kwaresima y akila mwaka. Kwa mwaka huu linafutwa kutokana n hofu ya kusambaa zaidi kwa kirusi cha corona, ambacho hadi sasa kimewashabulia watu karibia 150, Kaskazini mwa nchi ya Italia. Watu wanne hadi sasa wametajwa kuwa wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa COVID-19 na zaidi katika Mkoa wa Lombardia na maeneo mengine. Nchini  Austria walikuwa wamezuia kwa muda wa masaa manne safari za treni kutoka Italia, kwa kile walichosema ni kujipanga kukabiliana na uwezekano wa maambukizi ya kuingia kwenye mipaka yake, lakini baadaye wakaruhusu kuendelea na safari hizo za train.

Mahali pengine ni nchini Iran ambako imethibitishwa vifo vya watu wanane kutokana na ugonjwa huo, huku mataifa jirani yakifunga mipaka yao na taifa hilo la Ghuba ya Uajemi. Nchini China kuliko anzia ugonjwa, Rais Xi Jinping amesema kirusi hicho ni dharura kubwa kabisa ya kiafya kuwahi kulikumba taifa hilo tangu kuundwa kwake mwaka 1949. Hadi sasa, watu zaidi ya 2,400 wameshapoteza maisha na wengine 80,000 wameshaambukizwa duniani, wengi wao wakiwa ndani ya China.

24 February 2020, 15:27