Tafuta

Vatican News
Kampeni ya Udugu  kwa Kanisa katoliki la Chile inayoongozwa na kauli mbiu:“mchango wako na wa kwangu ni  matumaini ya wote" unajikita katika muktatha wa Kwaresima 2020 Kampeni ya Udugu kwa Kanisa katoliki la Chile inayoongozwa na kauli mbiu:“mchango wako na wa kwangu ni matumaini ya wote" unajikita katika muktatha wa Kwaresima 2020 

Chile:Kampeni ya Kwaresima 2020 kwa ajili ya wahamiaji!

Katika kipindi cha Kwaresima 2020 nchini Chile wamendaa Kampeni ya kidugu inayotazama mipango kwa ajili ya wahamiaji katika nchi yote.Kampeni hiyo inaongozwa na mada:mchango wako na wa kwangu ni matumaini ya wote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya siku ya Jumatano tarehe 26 Februari 2020 kwenye maadhimisho ya misa ya majivu ambayo ndiyo mwanzo wa kipindi cha Kwaresima, ndiyo pia mwanzo wa  Kampeni ya Udugu  kwa Kanisa la Chile  inayoongozwa na kauli mbiu: “ mchango wako na wa kwangu ni  matumaini ya wote”. Kampeni hii itaendelea hadi tarehe 5 Aprili 2020 ambapo watakusanya fedha kwa ajili ya kusaidia mipango kadhaa  ya ukarimu, kuhamasisha hali ya kibinadamu na kufungamanisha kwa jumuiya za wahamiaji Nchini Chile.

Timu ya maandalizi ya kampeni ya kwaresima wanatashiriki huko Valparaíso, katika Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria Misa ya Jumatano ya Majivu kwa kuongozwa na Askofu Pedro Ossandón, msimamizi wa kitume wa Jimmbo hilo na Mwenyekiti wa Kampeni ya Kwaresima.  Miaka ya mwisho, kwa mujibu wa taarifa kutoka katika tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Chile wanabainisha kuwa uhamisho wa watu kuingia katika nchi yao umezidi kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kushinda uwezo wa kuwakarimu na kuwatunza hasa wahamiajai walio wadhaifu zaidi, iwe kwa ngazi ya serikali, na kama ilivyo ya kijamii na mashirika mengine ya kichungaji ya Kanisa.

Yote hayo yanageuka kuwa changamoto na ndiyo wito wa ushirikishwaji kwa Bara la Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbian. Na ndiyo maana kati ya mwaka 2019-2021 kampeni ya kwaresima imepewa kipaumbele kwa jumuiya za wahamiaji. Fedha zilizokusanywa mwaka jana zitawezesha kufanya kazi katika miradi 39 kwa kazi ya kitaifa kwa mujibu wa taarifa nchini Chile.

25 February 2020, 14:54