Tafuta

Vatican News
Askofu wa Livingstone nchini Zambia anasema lazima kufanya uamuzi juu ya Neno la Mungu ambalo linahubiriwa kwetu sisi na siyo kuliacha lifike Askofu wa Livingstone nchini Zambia anasema lazima kufanya uamuzi juu ya Neno la Mungu ambalo linahubiriwa kwetu sisi na siyo kuliacha lifike  

Zambia:maandiko matakatifu yawe msingi katika mzunguko wa maisha ya binadamu!

Askofu Valentine Kalumba wa Jimbo la Livingston nchini Zambia katika fursa ya Maadhimisho ya Dominika ya Neno la Mungu iliyoanzishwa na Papa Francisko amesema Maandiko yanapaswa yawe chimbuko na katika mzunguko wa maisha ya binadamu. Ni lazima kufanya uamuzi juu ya Neno la Mungu ambalo linahubiriwa kwetu na siyo kuliacha lifike na kupita.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Lazima tuazimie juu ya Neno la Mungu ambalo linahubiriwa kwetu na siyo kuliruhusu lifike na lipite kwetu. Amesema hayo Askofu Valentine Kalumba wa Jimbo la  Livingston nchini Zambia katika fursa ya Maadhimisho ya Dominika ya Neno la Mungu iliyoanzishwa na Papa Francisko.

Askofu Kalumba ambaye pia ni Mwanashirika wa Waoblati wa Maria Mkingiwa wa Asili amesisitiza kuwa Maandiko matakatifu yanapaswa yawe mstari wa mbele kwa kila mzunguko wa maisha ya binadamu. “Labda hatuhubiri vizuri” amesema akiwashauri makuhani kusasisha kwa dhati namna ya kuhubiri na kuweka kipaumbele cha uchungaji wao.

Askofu Kalumba amesema kuwa: “tunahitaji kuandaa Neno la Mungu kwa ajili ya Watu wa Mungu kwa maana wanayo haki ya kusikiliza mahubiri yaliyo mazuri. Hatupaswi kuwa na mahubiri yasiyofurahisha”.  Akiwageukia waamini Askofu zaidi amekumbusha kuwa Neno la Mungu linapaswa kushwishi hata katika maisha ya kisiasa: “sisi sote ni familia moja ya kikristo inayotegemeana hata na  matakwa tofauti ya kisiasa”.

Katika fursa hiyo, Kanisa mahalia la Livingston nchini Za,bia limeweza kuuza hata Biblia kwa gharama nafuu kabisa, waliandaa hata maswali pia ya kibiblia kwa ajili ya makundi na vyama vya tamasha la nyimbo zenye mada za kibiblia. Askofu wamewatia moyo wakristo wote kuhusiana na utumiaji Bibilia kichungaji, akiwaalika kuwa na tabia ya usomaji, kujifunza, kusali na kushirikishana  ma  zaidi hata kusali Rosari na tafakari za kila siku katika masomo ya kiliturujia.

Hatua hivyo hata hivyo ikumbukwe kuwa Baraza la maaskofu nchini Zambia walipotangaza Mwaka wa Neno la Mungu walisisitizia juu ya shughuli za kichungaji na kuwatia moyo majimbo yote ili kutoa mafunzo ya kudumu katika Huduma ya Neno kwa ajili ya wakala wa kichungaji kwenye Tume ya Katesi, Biblia na Liturujia za kijimbo na kwa wale ambao wanahusika katika vyombo vya matangazo mfano Radio , tlevisheni na katika utume wa Elimu.

29 January 2020, 17:04