Maandalizi ya mkutano wa "Uchumi wa Fransisko" kwa vijana yanapamba moto.Ni mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 26-28 Machi 2020 ukijumuisha vija kutoka nchi 115 Duniani. Maandalizi ya mkutano wa "Uchumi wa Fransisko" kwa vijana yanapamba moto.Ni mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 26-28 Machi 2020 ukijumuisha vija kutoka nchi 115 Duniani. 

Zaidi ya vijana 2000 kutoka nchi 115 wanaudhiria mkuntano

Zaidi ya vijana 2000 kutoka nchi 115 watafika kuhudhuria mkutano na Papa Francisko kuhusu mada ya “Uchumi wa Francisko” kuanzia tarehe 26 -28 Machi 2020 ambapo washiriki wanauchumi na wajasiliamali kutoka duniani kote wataweza kukabiliana na mada mbalimbali kama vile:kazi na utunzaji;usimamizi na zawadi;fedha na ubinadamu;kilimo na haki;nishati na umaskini;faida na wito; sera za furaha;Ekolojia ya usawa;biashara na amani;uchumi na mwanamke.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mji wa Assisi nchini Italia unajiandaa kuwapokea vijana zaidi ya 2000 ambao ni wanauchumi na wanajasiliamali  hadi miaka 35 kutoka duniani kote ili kuhudhuria mkutano unaohuhusu Uchumi wa Francisko. Ni tukio ambalo ni kwa matashi ya Papa Francisko utakao fanyika kwa siku siku tatu kuanzia tarehe 26-28 Machi 2020. Hata hivyo, hadi sasa tarifa zinasema kuwa ni maombi ya watu 3300 kutoka nchi zaidi ya 115. Na ili kufanikisha tukio hili , katika mji wa Mtakatifu Fransisko unaandaliwa vijiji 12 ambavyo vitaona kazi ya washiriki hawa kuhusiana na mada kubwa na maswali mengi yanayojikita katika uchumi leo na kesho kama vile: kazi na utunzaji; usimamizi na zawadi; fedha na ubinadamu; kilimo na haki; nishati na umaskini; faida na wito; sera za furaha; Ekolojia ya usawa; biashara na amani; uchumi na mwanamke; makampuni katika kipindi cha mpito; maisha na mtindo wa maisha.

Upeo wa ndani ambao unapaswa kueleweka katika maelezo ya vijiji umetolewa na  Askofu Domenico Sorrentino wa  Jimbo katoliki la Assisi, kwamba: “Uendeshaji wa tukio hilo una uhusiano na Mtakatifu Francisko, kwa uzoefu wake wa maisha na chaguzi zake, mbazo pia zina thamani katika uchumi. Ni yeye aliyechagua kati ya uchumi wa ubinafsi na uchumi wa zawadi”. Aidha ameongeza kusema tendo la kujivua kwake mbele ya macho ya baba yake na Askofu wa Assisi ni ishara ya kusisimua kwa ajili ya tukio la mwezi Machi na ndiyo sababu ya Papa kutaka lifanyike  katika mji huu wa  Assisi”. Na kwa maana hiyo ni matumaini yake  kwamba hali ya kitasaufi ya mji huu itakuwa bora katika kufanikisha mkutano huo.

Washiriki wa Uchumi wa Francisko ni watafiti vijana, wanafunzi, wanafunzi waliopata shahada (PhD); wajasiriamali na viongozi wa biashara; wabunifu wa kijamii, wahamasishaji wa shughuli za ndani na za kimataifa na mashirika; wanaoshughulikia mazingira, umasikini, usawa, teknolojia mpya, fedha pamoja, maendeleo endelevu na zaidi wote wanaojihusisha na masuala ya mwanadamu.

Siku tatu za kazi yao zinahitimisha kwa kutiwa sahihi ya vijana wanauchumi na Papa Francisko aliyewaita huko Asisi ili kwa hakika kuweza kusikiliza kilio cha dharura ya ndoto zao. Changamoto ni kubwa, lakini  haitashindwa kwa sababu ya umahiri, fikra au kwa kuiga mtindo wa Mtakatifu Francisko. Vile vile changamoto ni kubwa kama uaminifu unaowekwa kwa vijana uweze kupokelewa. Kusikiliza matakwa ya ndani ya moyo na uwezo wa kuamua kwa vitu ambavyo kwa hakika sio pesa  ambavyo vitafungua njia ya uchumi mpya.

Mambo muhimu ya kufahamu hadi sasa ni kwamba: Idhadi ya walioomba kuudhuria ni 3,300, na ambao wamekwisha thibitisha kufikia ni vijana 2,000 ikiwa na  asilimia 41%, ya wanawake na asilimia 56% ya wanaume. Vijana hawa wanatoka nchi 115. Na miongoni mwa vijana walio wadogo zaidi  wana miaka 12 ambao  wanatoka nchi za Slovakia na Thailand. Idadi kubwa ya washiriki wanatoka nchini Italia kwa wastani mahali unapofanyika mkutano, Brazili, Marekani, Argentina, Uhispania, Ubelgiji, Ufaransa, Mexico, Ujerumani na Uingereza. Zaidi ya matukio 80 ya maandalizi yatakuwapo na vijiji vinavyotengenezwa ni 12, kuwezesha tukio hili liwe la aina yake katika historia ya vijana wanauchumi na wajasiliamali.

10 January 2020, 14:59