Onyesho la Sanda ya maziko ya Yesu kwa mara nyingine huko Torino Italia!
Na Padre Angelo Shikombe;- Vatican
Askofu Mkuu Cesare Nosiglia wa Jimbo la Torino ametoa tangazo la kufanyika tena maonyesho ya kipekee juu ya Sanda ya maziko ya Yesu Kristo yanatarajiwa kurudiwa tena mnamo tarehe 28 desemba 2020 katika Kanisa Kuu la Torino nchini Italia. Hija hiyo inaongozwa na kaulimbiu: “Hija ya imani duniani” na mbayo imepata mwitikio chanya kutoka jumuiya mbalimbali hapa nchini Italia. Ameyasema hayo katika mkutano wa maandalizi ya maonyesho hayo yanayowalenga vijana mahujaji. Aidha Askofu mkuu Cesare Nosiglia amesema Jumuiya ya Kiekumene ya kimataifa Taizé imeichagua sehemu ya Torino nchini Italia kuwa sehemu muafaka ya hija yao itakayoanza tarehe 28 Desemba 2020 na kumalizika Januari mosi, 2021.
Naye mwandishi wa Vatican News Robin Gomes ametaarifu kuwa, Maonyesho haya ya tano tangu yaanze kufanyika mnamo mwaka 2000 yanatarajiwa kuwa na ufanisi mkubwa japokuwa Torino hakuwahi kuwa na historia ya mafundisho kikanisa. Kwa mara ya mwisho maonyesho hayo yalifanyika kunako tarehe 24 Juni 2015 katika Kanisa kuu la Torino nchini Italia.
Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 21 na 22 Juni 2019 alisali kwa muda mfupi katika Grotto hiyo na akiwa katika Misa na kufafanua juu ya Groto hiyo kuwa ni alama ya upendo wa Kristo. Grotto inayohifadhi Sanda hiyo Katika kanisa kuu imekuwa kivutio kwa watu wengi na hasa kwa wenye mahangaiko. Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea sehemu ya Grotto hiyo mnamo 1998 na kuona mazingira maajabu ya kimazingira ambayo yanavuta kufanya utafiti ili kuona kama kweli masalia ya nguo za maziko ya Yesu Kristo zilikuwa mahali hapo.
Baba Mtakatifu Mstaafu Benedicto XVI alielezea kuwa alama hiyo imeandkwa kwa damu ya mtu aliyesulibiwa. Askofu Mkuu Nosiglia alibaini eneo hilo kuwa linafaa kwa hja ya vijana wa Italia wanaotokea maeneo ya Piedmonte. Askofu Mkuu Nosiglia amefanya mkutano mnamo tarehe 3 Januari 2020 huko Torino, Italia ili kuandaa hija hiyo.