Katika zira ya Papa inayotrajiwa kwenda Bari kunako tarehe 23 Februari ataweza kutembelea na kusali katika masalia ya Mtakatifu Nicola wa Bari Katika zira ya Papa inayotrajiwa kwenda Bari kunako tarehe 23 Februari ataweza kutembelea na kusali katika masalia ya Mtakatifu Nicola wa Bari  

Mpango wa ziara ya Papa huko Bari katika mkutano wa kimediterranea!

Katika fursa ya Mkutano juu ya tafakari na tasaufi iliyopewa jina la“Mediterranea mpaka wa amani”, ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu nchini Italia,Papa Francisko anatarajiwa kuwa Bari tarehe 23 Februari 2020. Ratiba nzima umetangazwa katika vyombo vya habari Vatican.Matarajio ya mkutano wa Maaskofu wa Mediterrania pia utakuwa utakuwa na Misa Takatifu.

Maaskofu katoliki wa nchi 20 ambazo zinapakana na Bahari ya Bediterrania, watakuwa na Mkutano huko Bari kuanzia tarehe 19-23 Februari 2020 ili kushiriki tafakari na tasaufi ambapo maaskofu wa Italia ndiyo wameandaa, kwa mujibu wa Kardinali Gualtiero Bassetti Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia. Amethibitisha hayo wakati wa hotuba ya utangulizi wa Mkutano wao wa kudumu na kwamba ili kutoa maoni, kutoka ukanda tofauti wa bahari, kwa kile kinachotokea na kuweza kuanza mchakato mpya wa maono ya pamoja na kushirikiana kwa kazi ya dhati.

 Papa atashiriki mkutano huo tarehe 23 Februari

“Papa Francisko atajongea nao tarehe 23 Februari , ili kufunga tukio hili lenye kauli mbiu ya “Meditranea mpaka wa amani” amesema Kardinali Basseti. Na hii ni kwa mara ya pili, Papa Francisko anatembelea Bari na ni kwa mara ya nne Papa anatembelea Mkoa wa Puglia, Italia kwa ujumla ikijumuishwa hata ile ya tarehe 17 Machi 2018 huko San Giovanni Rotondo wakati wa fursa ya maadhimisho ya kumbu kumbu ya kifo cha Padre Pio; ya tarehe 20  Aprili mwaka huo huko Alessano na  Molfetta kwa ajili ya kumbu kumbu ya miaka 25 ya kifo cha don Tonino Bello.

Safari yake kutoka uwanja wa ndege wa Vatican inategemea  kuanza asubuhi majira ya Ulaya saa 1.00. Na Saa 2.15 hivi kutelemka katika uwanja wa Cristoforo Colombo huko  Bari,  mahalia ambapo atapokelewa na Askofu Mkuu Francesco Cacucci na wawakilishi viongozi wa raia, kama vile Mkuu wa Mkoa Michele Emiliano, Mkuu wa Wilaya, Antonella Bellomo  na Meya wa Mji Antonio Decaro.

Mkutano wa Kiekuemena wa Sala kwa ajili ya Amani

Kutoka katika uwanja huo kwa gari Papa atakwenda katika Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Nicola, mahalia ambapo tayari mwezi Julai 2018 alikuwa ameshiriki Mkutano wa Kiekuemene wa Sala kwa ajili ya Amani ya Nchi za Mashariki. Saa 2.30 asubuhi hivi atakuwa na mkutano na washiriki wa Mkuwano huo kuhusu Mediterranea kwa utangulizi wa hotuba ya Kardinali Gualtiero Bassetti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Italia (CEI), kufuatia  Hotuba ya Kardinali  Vinko Puljić, Askofu Mkuu wa Vrhbosna na Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu katoliki nchini Bosinia na  Erzegovina, na Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa Kitume katika Upatriaki wa Yerusalemu.

Misa kwa waamini wote 

Hotuba ya papa Francisko itafutia na shukrani kutoka kwa Askofu Mkuu Paul Desfarges, wa Jimbo Kuu Katoliki la Alger (Algeria) na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa ya Afrika ya Kaskazini. Hatimaye Papa Francisko atatelemka chini ya Kanisa ili kutoa heshima katika  masalia ya Mtakatifu Nicola wa Bari na kusalimia Jumuiya ya Mapadre Wadominikani wanasimamia Kanisa kuu hilo. Na akitoka ndani ya Kanisa Kuu, atakutana na watu na kuwasalimia kwenye uwanja nje ya Kanisa na pia kuondoka na gari kwenye njia ya Vittorio Emanuele II.  Saa 4.45 Papa Francisko ataongoza Misa Takatifu na baada ya misa hiyo kufuatia Sala ya Malaika wa Bwana. Saa 6.30 anatarjia kuondoka na Helikopta kurudi Vatican karibia saa 7.45.

22 January 2020, 11:15