Maaskofu wa Mexico wanasema dharura ya wahamiaji inaanzia na misafara mikubwa ya mwaka 2018 na kuendelea katika mwaka 2019 ambayo  imekuwa fursa ya utambuzi wa dhati wa Upendo wa kanisa lao la Mexico, kwa kutoa msaada wao kidugu Maaskofu wa Mexico wanasema dharura ya wahamiaji inaanzia na misafara mikubwa ya mwaka 2018 na kuendelea katika mwaka 2019 ambayo imekuwa fursa ya utambuzi wa dhati wa Upendo wa kanisa lao la Mexico, kwa kutoa msaada wao kidugu 

Mexico:msisitizo wa maaskofu kuhusu wahamiaji,watoto na uhuru wa kidini!

Maaskofu wanakumbusha jibu la dharura ya wakimbizi wa Amerika ya Kusini wa miaka miwili ya mwisho; Maendeleo katika katiba ya Tume ya kijimbo kwa ajili ya ulinzi wa watoto;Kutunza waathirika manyanyaso katika nchi na kulinda haki msingi kwa ajili ya uhuru wa dini na wito wa kutazama kwa imani na amatumaini mwaka 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Maaskofu katoliki nchini Mexico katika ujumbe wao kwa ajili ya mwaka mpya 2020, wamsema “tunaendelea kusali kwa ajili ya hali halisi hasa ambayo tunaishi na kuwasindikiza kwa nguvu zetu thati  za kuendelea kuwatunza watu ambao Bwana ametupatia. Ujumbe wao umetiwa sahihi na  Askofu Mkuu Rogelio Cabrera López, wa Jimbo Kuu Katoliki la Monterrey na mabaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Mexco (Cem) na Askofu Msaidizi Alfonso G. Miranda Guardio, wa  Jimbo kuu katoliki la  Monterrey na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Mexico (Cem).

Mchango wa Kanisa la Mexco kwa ajili ya wakimbizi

Daharura ya wahamiaji wanasema inaanzia na misafara mikubwa ya mwaka 2018 na kuendelea katika mwaka 2019 ambayo  imekuwa fursa ya utambuzi wa dhati wa Upendo wa kanisa lao la Mexico, na katika watu wao ndugu, kaka na dada wahamiaji. Aidha “Maelfu na maelfu wameingia katika Nchi yetu kwenye miezi ya mwisho na wimbi ambalo halikusimama”. Mchango wa dola za kimarekani 500,000 zilizotolewa na Papa Francisko kwa ajili ya kusaidia wahamiaji nchini Mexico zimetumika kwa ajili ya kukamilisha mipango 32 ya kujibu maombi ya dharura ya chakula, afya na mavazi.

Matarajio ya kumaliza mipango yao iliyukusudiwa

Katika kesi nyingine wamekarabati mazingira ya vituo vya kukaribisha, ambavyo kwa sasa vimejaa sana wahamiaji na wengine walinunua fanicha na vifaa, wanaandika maaskofu. Kwa usalama wa wanaojitolea na wahamiaji, umekamilishwa kuwekwa uzio wa mzunguko wa vituo kadhaa vya mapokezi. Kwa maana hiyo,Maaskofu wanasema “ni matatajio yetu kumaliza miradi yote ifikapo februari  mwaka huu na kuweza kuendelea kutumainia juu ya ukarimu wa watu wa Mungu katika kuendelea na usaidizi huu kwa ndugu zetu wanaohama”.

Ulinzi wa watoto wadogo na waathirika wa manyanyaso katika Nchi

Aidha maaskofu pia wamkumbusha juu ya maendeleo katika katiba ya Tume ya kijimbo ambayo kwa sasa inajumuisha watu 14. Baraza la Kitaifa kwa ajili ya ulinzi wa watoto limefungamani na wajumbe wa Baraza la Mamama wakuu wa Mashirika nchini Mexico(Cirm) ili kutembea kwa pamoja na mashirika ya kidini katika kudhibiti kila aina ya manyanyaso ya kijinsia katika muktadha wa Kanisa.

Kusasisha sheria juu ya uhuru wa dini

Nafasi kubwa ya mkutano pia imejihusiana na masuala ya kijamii ambayo Kanisa Katoliki nchini Mexico inajikita nayo. Kwa maana hiyo ujumbe wa Maaskofu wanasisitiza kwamba ili kuendelea kushirikiana kwa ajili ya jamii, lazima kusasisha sheria ambazo zinajaribu  kutekeleza moja ya haki msingi kwa ajili ya kila jamii ya kidemokrasia ya kisasa na ambayo ni uhuru wa dini. Aidha  kusasisha sheria ya pili juu ya uhuru wa kidini; kushikilia kanuni ya kihistoria ya kujitenga kati ya Kanisa na Serikali, kulingana na vigezo vya hali ya juu zaidi vya kimataifa, ni muhimu. Maaskofu wanasisitiza kwamba hawaombi upendeleo kwa chama chochote cha kidini, lakini kwamba wanataka Makanisa na wahudumu wao  waweze kufanya kazi ipasavyo, kwamba uhuru wa kidini unalindwa na ulinzi bora wa kisheria na kwamba haki na majukumu ya juu ya watu yanaheshimiwa, kwa  kukuza maisha ya dini katika kuwa na uhuru katika jamii.

Kutazama mwaka 2020 kwa imani na matumaini

Hatimaye katika ujumbe wao  maaskofu wa Mexico unatoa mwaliko wa kutazama kwa imani na matumaini mwaka 2020 kwa sababu amani, mapatano na majadiliano ndivyo vitawale  kwa watu wote kama ilivyo hata katika jamii na kujitahidi kutunza kila ndugu na nyumba ya pamoja, huku wakiinua mtazamo na moyo kwa Mwokozi Yesu Kristo.

 

 

16 January 2020, 13:54