Maaskofu Kanda ya Afrika:Ombi la amani katika kanda ya Maziwa Makuu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Hali halisi ngumu ya uchungaji kijamii katika Jamhuri ya Kidemokarasaia ya Congo, ya Rwanda na Burundi, jitihada za amani ya kudumua katika Kanda yote ya Maziwa Makuu na Motu Proprio ya Papa Francisko “Vos estis lux Mundi” kuhusu ulinzi wa watoto na watu walioathirika katika Kanisa. Ndiyo masuala msingi katika mada ya siku kwenye Kamati ya kudumu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati (Aceac), kwenye Mkutano wao uliofanyika hivi karibuni huko mjini Bukavu, Congo DRC.
Na kama hiyo haitoshi pia kuendelea kwa ukatili wa virusi vya ebola, mvua nyingi katika miezi ya hivi karibuni ambayo imesababisha vifo
Wakati wa kazi yao ya mkutano kwa mujibu wa ujumbe wao wa mwisho maaskofu wamebainisha hali halisi ya sasa kijamii inayoleta wasi wasi kubwa katika nchi tatu kuanzia ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo, kwa namna ya pekee katika mipaka, mahali ambapo panasalia kuwapo makundi ya mgambo ya kutumia silaha. Maaskofu pia wameonesha kuwa kupunguza nguvu ya ununuzi ni kupunguza viwango vya maisha vya familia nyingi ambao tayari wanaishi na umaskini. Na kama hiyo haitoshi pia kuendelea kwa ukatili wa virus vya ebola, mvua nyingi katika miezi ya hivi karibuni ambayo imesababisha vifo hata uharibifu mkubwa wa nyumba na zana mbalimbali. Kufuatia na hili Maaskofu wa Afrika ya Kati wameweza kupongeza juhudi za Caritas na Tume ya Haki na amani mahalia, ambazo zimejikita katika kusaidia watu waliokumbwa na maafa hayo, pia wanarudia kuwaomba wakristo wote waendelee kuonesha mshikamano kwa waathirika hao.
Maaskofu wamepyaisha ahadi zao za kufanya kazi pamoja na madhehebu mengine ya kidini
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya kanda ya Maziwa makuu (Aceac) wanatoa wito wa kuwa na dhamiri nyoofu katika srikali za Kinshasa, Gitega na Kigali na ili kuweza kuweka moyoni suala la usalama na matarajio mema ya watu. Kuzorota kwa hali ya kisiasa katika nchi hizo tatu kiukweli kuna hatari ya kuzidisha tishio la mapigano ya silaha ambayo yanaendelea hasa katika majimbo ya kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC. Kwa upande wao, maaskofu wamepyaisha ahadi zao za kufanya kazi pamoja na madhehebu mengine ya kidini kwa ajili ya amani ya kudumu katika Kanda ya Maziwa Makuu.
Lazima kuwepo na muundo wa kushughulikia ripoti za unyanyasaji wa kijinsia, ikionyesha mchakato mzima ambao lazima ufuatwe
Mada nyingina mabay pia ilikuwa katika mpango wa kazi yao ilikuwa ni kutazama majimbo katoliki ya Congo, Rwanda na Burundi juu ya usimamizi na ulinzi wa watoto wadogo na watu walioathirika katika Kanisa kwa mwanga wa mwongozo wa Motu Proprio “Vos estis lux Mundi”, uliotangazwa na Papa Francisko mara baada ya Mkutabo mjini Vatican wa mwezi Februari 2019 kwa marais wa Mabaraza ya Maaskofu katoliki duniani kote. Hati hiyo ya kipapa inapendekeza kwamba kufika Juni mwaka huu, tayari kila jimbo liwe na muundo wa kukubaliwa na kushughulikia ripoti za unyanyasaji wa kijinsia, ikionyesha mchakato mzima ambao lazima ufuatwe.