Kuelimisha  wanawake maana yake ni kuongeza nguvu katika familia na kwa maana hiyo katika jamii nzima.Ni mada iliyozungumzwa katika mkutano wa kidini huko Nairobi Kenya Kuelimisha wanawake maana yake ni kuongeza nguvu katika familia na kwa maana hiyo katika jamii nzima.Ni mada iliyozungumzwa katika mkutano wa kidini huko Nairobi Kenya 

Kenya:Mkutano wa kidini:kupaza sauti za wanawake na haki zao!

Katika Mkutano wa kidini uliohitimishwa tarehe 24 Januari 2020,Nairobi Kenya, wametoa wito wa kuwapa sauti zaidi wanawake na haki zao.Mkutano huo unasisitizia kwamba kuelimisha wanawake maana yake ni kuongeza nguvu katika familia na kwa maana hiyo katika jamii nzima ya watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuelimisha  wanawake maana yake ni kuongeza nguvu katika familia na kwa maana hiyo katika jamii nzima. Ndiyo ufupisho wa kile kilichojitokeza kwenye mkutano wa kidini ulifanyika tarehe 24 Januari 2020, jiji Nairobi Kenya kwa kuongozwa na mada “Haki za uchache wa kidini na ujumuishwaji wa kuelimishwa katika dini kwa mtazamo wa wanawake”. Waliokaribisha mkutano huo ni Taasisi ya Chuo Kikuu cha Tangaza (Tuc), kilichoona washiriki 50 hivi wanawake wa kikristo, ikiwa ni wakatoliki, waanglikani na kiislam ambao wameelezea umuhimu wa kusikiliza sauti zao zaidi ndani ya jamii katika maisha ya kidini.

Kati ya watoa mada pia ni Padre Lucas Ongesa Manwa, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya (Kccb),  ambaye amesisitizia juu ya nafasi msingi ya wanawake  na zaidi hasa  kurithisha ule  utambuzi na imani kwa watoto wao. Kwa maana hiyo Padre huyo amesema: “elimu kwa wanawake ni kuongeza nguvu katika familia na katika jamii nzima.” Aidha amebainisha kuhusu nafasi msingi ya wanawake katika kujenga amani, kwa maana wanawake wanarithisha zile thamani msingi ambazo zinapelekea mapatano katika mantiki ya kifamilia  na kijamii.

Kutokana na hiyo Katibu Mkuu wa Kccb ametoa wito wa ulazima wa kusaidia kuelimisha wanawake huku akikimbuka kuwa Kanisa Katoliki linakuza kwa dhati elimu fungamani na ya uelewa. Katika muktadha huo,  hata wawakilishi wa kianglikani wamebainisha  juu ya umuhimu wa kuunda nafasi za kweli   kwa ajili ya wanawake ndani ya Kanisa na katika jamii ambazo zinaweza kuwaleta pamoja katika kushirikishana maswala yanayo tazamana kwa karibu

Aidha wamesema wawakilishi wa kiangilikani kuwa mara nyinyi, wanawake wanadharauliwa haki zao na kwa maana hiyo kuanzishwa kwa jukwaa la mafunzo ni jambo msingi ambalo linaweza kuwafanya kweli  kuwa na utambuzi ya kwamba:  “ wao ni nani na kuelezwa nafasi yao wanaliyo, na haki zao kama binadamu.  Hata hivyo mantiki ya mkutano huo ni kama mwendelezo wa mkutano ulifanyika kunako Januari 2019 uliokuwa unaongozwa na mada ya “nafasi ya wanawake ndano ya tamaduni za kisni na mchango wao wa kujenga amani.

28 January 2020, 12:52