Tafuta

Siku ya Kumbu kumbu ya mauaji ya wayahudi huko Auschwitz inatupasa kufikiria kwa kina na ili tukio hili lisirudiwe tena Siku ya Kumbu kumbu ya mauaji ya wayahudi huko Auschwitz inatupasa kufikiria kwa kina na ili tukio hili lisirudiwe tena  

Kard.Koch:ni lazima kujifungulia wengine ili kupinga ubaguzi!

Mjini Yeruselemu limefanyika Jukwaa la 5 la Kimataifa kuhusu mauaji ya kiyahudi iliyoandaliwa na Yad Vashem.Hii ni siku kukumbuka mauaji yaliyofanyika huko Auschwitz.Tukio la Yad Vashem limeaona zaidi ya Viongozi wakuu wa nchi 40,wakiwemo mawaziri wakuu na familia za kifalme kutoka Ulaya, Amerika ya Kaskazini hadi Australia.Kardinali Kurt Koch amewakilisha Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mjini Yerusalemu limefanyika Jukwaa la 5 la Kimataifa kuhusu mauaji ya Wayahudi Na hii ni katika kuenzi kukumbuka kukombolewa kwa kambi ya mauaji ya Auschwitz iliyoendeshwa wa Wanazi. Tukio la Yad Vashem limewaona Viongozi wakuu wa nchi  zaidi ya 40, wakiwemo mawaziri wakuu na familia za kifalme kuanzia Ulaya, Amerika ya Kaskazini hadi Australia. Kardinali Kurt Koch amewakilisha Vatican. Jukwaa hili limeandaliwa na Mfuko wa Jukwaa la Mazungumzo Duniani kuhusu mauaji ya kiyahudi kwa ushirikiano na Yad Vashem. Uwakilishi wa Vatican umeongozwa na Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo mahali ambamo ndani mwake kuna Tume ya Vatican kwa ajili ya Uhusiano wa kidini na Wayahudi.

Akihojiwa kwa simu na Vatican News, Kardinali Koch ameeleza maana ya tukio hili  kwamba kama walivyofika wawakilishi wengi kutoka Mataifa mbalimbali namna hii ni ishara ya mtazamo wa kihistoria na ambayo inataka kutoa maana kubwa dhidi ya ubaguzi wa kiyahudi. Imeeelezwa wazi hata katika hotuba mbalimbalizi kwamba tunapaswa kujifunza kutoka katika historia na jambo kama hilo lisiweze kutokea tena.

Aidha Kardinali Koch anaamini kuwa ubaguzi wa kiyahudi siyo  sura tu ya historia ambayo inaweza kuwekwa kwenye vitabu vya historia , lakini pia ni tukio ambalo hata leo hii linajitokeza kwa upya. Kwa maana hii mifano mingi imetajwa na ambayo inapaswa kuwafanya wote wafikirie. Akielezea sababu za ubaguzi huu anasema, kiukweli ni tofauti sana, ambazo haziwezi kufupishwa kwa muda mfupi hivyo. Kuna sababu tofauti za kwanini watu wanaogopa wageni, ya kuogopa wengine, kwa sababu ya changamoto nyingi wanazokabili, na kwa hivyo hii ni kuhamishiwa kwa Wayahudi.  Aidha amesema leo pia tunayo tabia dhabiti za utaifa, utaifa mpya ambao pia unaweza kujifafanua kama ufunguo wa kibaguzi kama ule ya kiyahudi. Sababu pia zipo tofauti sana kulingana na nchi na nchi. Lakini anafikiri kwamba, utaifa pia ni sababu kuu ya matukio haya.

Wakristo wanaweza kufanya nini katika kupinga ubaguzi huo? “Kwanza kabisa, ningesema kwamba hofu za watu lazima pia zizingatiwe kwa kina. Lakini lazima tuchukue pia umakini wa watu hawa kuwasaidia kuzishinda. Kwa maana hiyo, kama Yesu anavyotuambia katika Injili ya Yohana: “Katika ulimwengu mtakuwa na dhiki, lakini muwe na ujasiri: Nimeushinda ulimwengu!”

Lazima tufanye yote mawili, kwa  kufikiria hofu ya watu, lakini kwa uhakika ya kuweza kuondokana na hofu hizi kwa imani, tukijifunua kwa wengine. Ki ukweli  Kanisa Katoliki linaitwa kwa namna ya pekee kukuza kwa kina urithi wa pamoja  na Uyahudi, katika mila za pamoja , za maadili shirikishi  na zaidi ya katika Hati ya “Nostra Aetate” ambayi ni tamko kubwa la Mtaguso wa Pili wa Vatican juu ya majadiliano kati ya Wayahudi na Wakristo kwa ajili ya kuendelea kwenye njia hii. Amfafanua Kardinali Koch.

Vile vile hata Maaskofu Katoliki  barani Ulaya wakati wa wanaadhimisha miaka 75 ya kukombolewa kwa kambi ya mauaji ya Auschwitz iliyoendeshwa wa Wanazi wanazidi kulaani matamshi ya chuki dhidi ya Wayahudi, na kupotoshwa ukweli kwa malengo ya kisiasa. Hii ni historia kubwa ya maadhimisho ya kukombolewa kwa Auscchwitz na jeshi la kisovieti, iliyotokea tarehe 27 Januari 1945. Hata hivyo hatua hii inajiri wakati kukiwa bado na hali ya kukana mauaji dhidi ya Wayahudi na visa vingine vya kupindisha ukweli wa kihistoria, huku hisia za uzalendo zikiongezeka barani Ulaya. Maaskofu katoliki wametoa wito mkuu na kwa maombi wakisali wakati mishumaa inawaka kwa ajili ya watu wa mataifa yote na dini zote waliouawa katika kambi za vifo!

 

25 January 2020, 11:49