Tunawezaje kusema juu ya maridhiano,ikiwa  kwa muda mrefu hali hii ya ukosefu wa haki ipo katika ardhi yetu ya nchi Takatifu. Ni kwa mujibu wa Askofu Mkuu Pizzaballa,msimamizi wa kitume Yerusalemu Tunawezaje kusema juu ya maridhiano,ikiwa kwa muda mrefu hali hii ya ukosefu wa haki ipo katika ardhi yetu ya nchi Takatifu. Ni kwa mujibu wa Askofu Mkuu Pizzaballa,msimamizi wa kitume Yerusalemu 

Ask.Mkuu Pizzaballa:inabidi kushughulikia kushindwa kwa majadiliano!

Katika mahubiri ya Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume katika Maendeo ya nchi Takatifu amesikika akielezea hali haisi ya kuyumba kwa nchi hiyo na kusema kwamba:Katika muktadha wao wa hapo inabidi washughulikie juu ya kushindwa kwa majadiliano mengi kuhusu makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina na kutofaulu kwa makubaliano yaliyofikiwa tayari na vurugu zinazoendelea.Ni katika Misa ya Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu sambamba na siku ya 53 ya kuombea amani duniani tarehe Mosi Januari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula–Vatican

Katika maadhimisho ya Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu tarehe Mosi Januari 2020,Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa Msimamzi wa Kitume katika Maeneo matakatifu wakati wa mahubiri yake amesema kuwa hata mwaka huu anapata fursa ya kujikita katika  Neno la Mungu na kutafakari kwa pamoja maana ya siku hii ambayo zaidi ya miaka 50 imewekwa ya kuombea siku ya Amani duniani.  Pendekezo la Papa Paulo VI bado ni hai hata leo hii na lenye maanakubwa  kwa ajili ya siku ya kuombea amani na kwa maombezi ya Bikira Maria mama wa Mungu ambaye siku hii anaadhimishwa umama wake.

Kama ilivyo kila familia, hata ndani ya Kanisa tunahitaji kumkabidhi Mama nafasi hiyo ya pekee, inayoshangaza na hisiyobadilishwa na wapatanishi, kwani yeye ni mwombezi na mlinzi wa matakwa ya kweli na ya kina na moja kati ya hayo ni amani. Akiendelea Askofu Mkuu Pizzaballa amesema,Ujumbe wa Papa Francisko kwa siku ya amani ambao ameukabidhi kwa mwaka 2020 una maana yake msingi. Kauli mbiu inasema “Amani ni mchakato wa safari ya matumanini:katika majadiliano, mapatano na ukongofu wa kiekolojia”. “Kiukweli ni lazima tugundue kuwa haya ni maneno ambayo yako  mbali sana na uzoefu wetu wa sasa hapa, katika Ardhi yetu Takatifu.

Kiukweli inaonekana kwamba kwa muda mrefu hakuna majadiliano ya kweli, isipokuwa katika taasisi ndogo ndogo, kwenye vikundi vidogo, kwa kifupi, lakini hakika siyo kati ya mamlaka, iwe ya kisiasa au ya kidini au kwa ngazi zote kwa jumla. Kwa kuongezea, neno 'upatanishi' ni karibu mwiko hapa. Tunawezaje kusema juu ya maridhiano, ikiwa  kwa muda mrefu hali hii ya ukosefu wa haki ipo katika ardhi yetu? Mwishowe, suala la  uongofu wa kiekolojia haueleweki hata ni nini maana yake. Ni mada muhimu wa mtaji na ukubwa wa ulimwengu, lakini inajadiliwa karibu katika nchi tajiri na  hakika sio yetu”… ameisitiza Askofu Mkuu Pizzaballa.

Akiendelea amesema licha ya hayo yote “Je hatuna matumaini? Kwa hakika hapana. Katika sehemu ya kwanza ya ujumbe unazungumzia kiukweli juu ya safari ya matumaini. “Kwa maana hiyo tunaweza kujikita katika safari hizo za matumani ambazo ndizo utume wa Kanisa letu na ambao unapaswa utupeleke katika amani” amehimiza. Vile vile Askofu Mkuu Pizzaballa amesema: “Katika muktadha wetu wa hapa inabidi tushughulikie  juu ya kushindwa kwa majadiliano mengi juu ya makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina na kutofaulu kwa makubaliano yaliyofikiwa tayari, na vurugu zinazoendelea”.

Kadhalika ameongeza ksema, “ni lazima tushughulikie kutoaminiana kwa jumla kwa mitazamo mpya, kwa shauku ya amani, na mabadiliko iwezekanavyo. Kwa kifupi, tunazungumza juu ya majadiliano na amani wakati wageni wanakuja na katika mikutano mbali mbali iliyoandaliwa kutoka nje ya nchi, lakini tunajua katika mioyo yetu kiukweli hapa ni tofauti na kwamba mazungumzo ni mbali na maisha yetu halisi”.

Je tufanyeje? Katika swali hili Askofu Mkuu anasema: “Kwanza kabisa tunaalikwa kukubali ukweli ambao tuko pamoja na umuhimu wake, kazi zake, migogoro yake. Kufikiria kuwa Kanisa katika Ardhi Takatifu kuepuka au kukimbia migogoro, au kujaribu kuyatatua kwa mantiki zisizo za injili, labda itahifadhi miundo yetu, lakini haitakuza imani na tumaini la Wakristo wetu. Kutambua ukweli wetu mgumu wa maisha, kuhakikisha kuwa tunahisi tunasikilizwa katika maumivu yetu na kwa maana hiyo ni hatua ya kwanza kwa shuhuda wa jumuiya enye maana”.

Akihitimisha Askofu Mkuu Pizzaballa amesema “Kwa wale waliomuuliza Yesu sababu ya upofu na upuuzaji wa wakati wake, Bwana alijibu kwa kuwaalika wawe na uongofu kwa Mungu na ili kwenda katika maisha yetu (Rej.Lk 13: 1-9). Hali ya chungu ya sasa lazima iishe bila hofu nyingi. “Na pia ni fursa ambayo tumepewa sisi kutoa ushuhuda wa upendo kwa Kristo na kwa ndugu kaka na dada zetu: upendo wa kina, ilio mzuri, wa ukarimu kwa aliye na shida. Na kwa Maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Mungu, atusaidie kushuhudia pia katika mwaka huu mpya wa upendo ambao umeshinda ndani ya mioyo yetu.

02 January 2020, 13:35