Tafuta

Vatican News
Siyo rahisi kumsahau Mchungaji King wa Marekani aliyetetea haki za watu wa Mungu na ambao leo hii katika mataifa mengi bado wanaendelea kunyanyaswa na kukosa haki msingi Siyo rahisi kumsahau Mchungaji King wa Marekani aliyetetea haki za watu wa Mungu na ambao leo hii katika mataifa mengi bado wanaendelea kunyanyaswa na kukosa haki msingi 

Ask.Gomez:ndoto ya Martin Luther King bado iko mbali!

Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mchungaji King,amebainisha masuala ambayo anaona nchini Marekani bado yamesimika mizizi yake kama vile ukosefu wa haki,ubaguzi na vijana wengi asili ya Afrika kuendelea kuwawa barabarani au kufungwa wengi magereza.Hivyo ndoto bado iko mbali!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya kifo cha Mchungaji Luther King Jr nchini Marekani, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani José H. Gomez ameweka bayana kuwa bado kuna uchungu mkubwa sana kwa utambuzi wa kuona hadi sasa ndoto ya Mchungaji Martin Luther King Jr inakuwa mbali sana, mchungaji aliyependwa na jumuiya nzima ya Amerika na ambayo alitoa maisha yake. Amebainisha hayo siku moja kabla ya kuadhimisha siku  ya kumbu kumbu kitaifa ifanyikayo kila tarehe 20 Januari  kwa waamerika wote, katika kumwenzi mchunji huyu na mtetezi mkuu wa haki za binadamu Atakumbukwa sana kwa msemo wake " I have a dream".

Sehemu za pembezoni bado ni maskini kama enzi za King

Askofu Mkuu Gomez anabainisha kupendelea mfano wa mshikamano alio uonesha King Jr,  kuhusu watu walio kuwa wanateseka na haki na kwa ajili ya ushuhuda wake wa upendo wa  kutopenda kutumia nguvu na katika mapambani ya mabadiliko kijamii. Anatambua njia ambayo imefuatwa nchi yake katika miaka hii ya mwisho, lakini pamoja na hayo yote amesisitiza kuwa bado hajatosha. Na hii ni kwa sababu bado ukosfu wa haki na katika mizizi ya ubaguzi mwingi na vijana wengi wenye asili ya Afrika kuendelea kuuwawa katika barabara au kufungwa magerezani. Katika mitaa ya watu wanaoishi wachache na sehemu mbalimbali za walio pembezoni nchini Marekani wanaendelea kuwa na umaskini wa kukithiri kama enzi za King, amebainisha.

Miaka ya mwisho kuna milipuko ya kiubaguzi

Askofu Mkuu Gomezi aidha anatoa malalamiko kuwa “ miaka ya mwisho tumeendelea kuona mlipuko mbaya sana wa ubaguzi, katika kuongezeka kwa mashambulio dhidi ya Wayahudi, maandamano ya utaifa mweupe, vurugu ya Wazungu dhidi ya weusi na wahamiaji wengine. "Tunachohitaji, na kile tunachoomba, ni kubadilika kiukweli ndani ya mioyo, mapinduzi  ambayo yatlaimisha kuwa na  mabadiliko na marekebisho ya taasisi zetu na jamii”, anasisitiza mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchi Anerika huku akitaja hata juu ya Barua ya Kichugahi ya Maaskofu kuhusu ubaguzi wa rangi yam waka 2018.

Jinsi gani ya kuheshimu kumgu kumbu ya  Martin Luther King

Katika swali la kujiuliza ni kwa jinsi gani ya kufanya kumbu kumbu kwa aliyekuwa mchungaji Martin Luther King, amesema inahitajika jitihada za kujenga jumuiya pendevu ya Amerika mahali ambapo watu, wanaume na wanawake wote wanakuwa kama watoto wa Mungu walio mfano  na sura yake,  wenye kuwa na hadhi, usawa na ambapo haiwezekani tena kukataa haki zao msingi, bila kujali rangi ya ngozi, lugha anayozungumza au mahali ambapo amezaliwa. Na kwa kufanya hivyo itawezekana kweli kuheshimu na kuenzi kwa dhati kumbukumbu ya Luther King mashuhuri na mtetezi wa haki za binadamu na hadhi yake.

21 January 2020, 10:32