Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu nchini Afrika ya Kati wameandika ujumbe wao wakihimiza raia wate nchini kutafuta namna ya kujenga amani katika nchi ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe Baraza la Maaskofu nchini Afrika ya Kati wameandika ujumbe wao wakihimiza raia wate nchini kutafuta namna ya kujenga amani katika nchi ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe 

Afrika ya Kati:wito wa maaskofu kwa ajili ya amani na maridhiano!

Mara baada ya Mkutano wa Baraza la Maaskofu nchini Jamhuri ya Kati,uliofanyika Bungui kuanzia tarehe 6 – 12 Januari 2020 wameandika ujumbe wao wakihimiza raia wate nchini kutafuta namna ya kujenga amani na maridhiano katika nchi ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kutumia silaha,ukosefu wa haki kijamii,usifisadi na umaskini wa kukithiri.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni wakati sasa wa kutafuta kujenga amani na maridhiano ambayo yamekosa kwa muda mrefu katika hali halisi ya vita vya silaha. Wameandika hayo Maaskofu nchini Jamhuri ya Kati wakati wa kumaliza Mkutano wa Mwaka uliofanyika huko Bangui kuanzia tarehe 6 hadi 12 Januari 2020 katika muktadha wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 125 ya uinjilishaji katika nchi hiyo. Katika Ujumbe wao ambao unawalenga wahudumu wa kichungaji, jumuiya za kikristo, vijana, wanasiasa, makundi ya kisilaha na Jumuiya ya Kimataifa.

Kufuatia na wasiwasi wa hali halisi ya Siasa kijamii, maaskofu wanabainisha kuwa Wakristo wengine hutenganisha maisha yao ya kitaaluma na maisha yao ya imani ambayo kwa  wengine huchanganya mazoezi ya imani na ya kichawi na kufanya maadhimisho ya sakramenti na kwamba, wengine bado wanaruhusu kuvutiwa na madhehebu yanayofumuka kama uyoga na jumuiya nyingine  za kisiri. Maaskofu pia wanaomba Serikali ijulishe ni lini vyombo vitaanza kufanya kazi, kama vile Mahakama Maalum ya uhalifu na Tume ya kweli, Haki, Maridhiano katika kuanza huduma muhimu zinazokosa  nchini, kama  elimu, afya ambazo kwa hakika hazijadhditishwa.

Hata kama wanafanya jitihada za kupunguza ghasia, Maaskofu wanabinisha kuwa, bado  raia wanaendelea kuishi katika mantiki ya ukosefu wa usalama, hofu na huzuni mkubwa. Licha ya kujaribu kuzuia kutumia silaha, silaha nyingi nzito na nyepesi bado zinazunguka nchini humo, wamesema Maaskofu katika ujumbe wao. Aidha  wakigeukia Jumuiya za Kikristo, wanaomba  kwamba kila mtu ajitoe kwa ajili ya  faida ya wote na  wanawasihi  waende kupiga kura ili kila mtu aweze kutekeleza jukumu lake kama raia, akipigania dhidi ya upendeleo, ukabila, uvumilivu kati ya vikundi vya kikabila na kisiasa, ufisadi na udanganyifu wa kisiasa.

Wito maalum unawahusu vijana kwamba: “tambueni  jukumu lenu la msingi katika historia ya nchi yenu na ubinadamu. Msikatishwe tamaan na hali halisi ya nchi na wala kuchanganyikiwa kwa mapepo ya chuki na wajasiriamali wa vurugu na uharibifu”.

Kwa wanasiasa, maaskofu wanasisitiza kuzingatia majukumu yao kama dhamira inayopaswa kutendwa katika  nchi, kuheshimu mfumo wa katiba wa uchaguzi, kurudi kuzungumza na vikosi vyenye kutumia  silaha pamoja na ili kupata suluhisho linaloshirikishana la amani, na kuwawezesha kurudi kwa watu waliohamishwa na  wakimbizi.  Hii inaweza kusaidia mwendelezo wa kushirikiana na vikosi hai vya taifa na vyama vya siasa vyenye nguvu katika roho ya uzalendo. Hatimaye maaskofu wanomba vikundi vilivyo na silaha kuheshimu makubaliano ya kisiasa ya amani na maridhiano katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, na ili kumaliza uhasama na  unyanyasaji mbaya wa maliasili. Ujumbe wa Baraza la Maaskofu unahitimishwa kwa kutoa ushauri kwa Jumuiya ya kimataifa, ili kuzingatia heshima na kutokujali suala la kutokuwa na usawa. Lazima kuundwa mazingira ya utulivu na uwazi katika uchaguzi ujao.

14 January 2020, 09:28