Afrika Kusini:mpango mpya wa kichunga:jumuiya moja ya uinjilishaji katika huduma ya Mungu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kubadilisha nanma ya kuwa nini Kanisa leo hii Afrika ya Kusini ili iweze kutangaza Injili kwa namna ya kweli na uhai zaidi katika mantiki ya mwendelezo wa utamaduni na kijamii. Ndiyo lengo la mpango wa Kichungaji wa Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini, katika kutaka Jumuiya ya kuinjilisha kwa huduma ya Mungu, ya ubinadamu na kazi yote ya uumbaji. Matunda hayo ni karibu ya miaka 10 ya kutafakari ambayo yamo katika Hati iliyotolewa rasmi tarehe 26 Januari 2020 huko Soweto mara baada ya Mkutano wao mkuu wa maaskofu wa Sacbc, unaounganisha maaskofu 29 wa Afrika Kusini kuanzia Botswana na Eswatiti (ex Swaziland).
Hati hiyo inajibu daima zile dharura ambazo zimejionesha kwa miaka hii ya mwisho katika Mabaraza ya Maaskofu Afrika ya Kusini na ili kufikia kusasisha mpango wa mwisho wa Kichungaji wa mwaka 1989 kwa mwanga wa maendeleo ya kijamii, kisiasa, na kiutamduni katika nchi za Afrika ya Kusini hasa baada ya suala la ubanguzi. Kama alivyokumbusha Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu Sithembele Sipuka, wakati wa mchakato wao wa mkutano huko Pretoria, kwamba “hata jamii ya Afrika ya kusini imebobea tayari katika mantiki za kiulimwengu na ambazo katika kukua unaanza kuweka pembeni Kanisa na Injili, kwa tafakari na tamaduni, juu ya sheria na matukio mbalimbali ya kijamii”.
Changomoto sasa ni mbili: Kwa mujibu wa Hati hiyo inasema kuwa , kwa upande mmoja ni kutaka kutoa uhai ile imani na tasaufi ya waamini huku wakiwatia moyo katika kupyaisha uhusiano wao binafsi, Kristo na jirani, na mbapo inatakiwa kuanzishwa utume mpya wa uinjilishi katika Kanisa la Afrika ya Kusini na zaidi kuwajumuisha walei ili waweze kuwa hai na chachu ya mashuhuda wa Kristo; na kijamii katika jamii ambayo leo bado inaona migogoro ya nguvu katika sera za kisiasa, na kijamii, pia ongezeko la ukosefu wa usawa vurugu za ubaguzi, ufisadi, uhalifu na ukosefu wa usalama.
Kwa ukaribu wa mambo hayo ni muhimu, yanayohusiana na ambayo yanazingatia mpango mpya wa kichungaji uliowekwa na Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini Sacbc ambao, alielezea Askofu Sipuka, kwamba yanataka kusaidia Kanisa la Afrika Kusini ili kuhama kutoka katika huduma ya kichungaji iliyokuwa na tabia ya kuhifadhi na ili kuingia katika uhai wa umisionari kama anavyohimiza Papa Francisko katika Wosia wake wa “Evangelii Gaudium”. Hati hiyo imeundwa na kurasa 12 ya maandishi ambayo yamegawanywa katika sehemu nane za mada zinazohusi uinjilishaji; malezi na kuhamasisha jukumu la walei; maisha na huduma ya makuhani na mashemasi; ndoa na familia; vijana, haki ya kutotumia nguvu; uponyaji na mapatano; utunzaji wa kazi ya uumbaji na mazingira.