Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Afrika ya Kusini wanafanya mkutano wao huko huko Pretoria ambapo Balozi wa Vatican nchini humo Askofu Mkuu Peter Welles amewashauri kuwa wachungaji wa huduma Maaskofu wa Afrika ya Kusini wanafanya mkutano wao huko huko Pretoria ambapo Balozi wa Vatican nchini humo Askofu Mkuu Peter Welles amewashauri kuwa wachungaji wa huduma 

A.Kusini:Maaskofu muwe mfano wa dhati!

Katika hotuba yake Balozi wa Vatican nchini Afrika Kusini Askofu Mkuu Welles,amewashauri maaskofu warudie katika uongofu wa Ubatizo ili kuweza kufikia ushiriki wa kina wa utume kimisionari na ambao kwa dhati ndiyo tabia ya Yesu, kwa maana Yesu ndiye mzizi wa uinjilishaji na aliyekukuja kuhudumia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mkutano huko Pretoria nchini Afrika Kusini wa Baraza la Maaskofu unaendelea ambapo Balozi wa Vatican nchini humo Askofu Mkuu Peter Welles, katika hotuba yake amejikita kutazama utume maalumu na ambao unapendelewa na Papa Francisko na kuwambia maaskofu kwamaba wanapaswa wawe maaskofu wenye mifano hao katika mpango mzima wa maisha ya kichungaji.

Katika hotuba yake Balozi wa Vatican nchini Afrika Kusini Askofu Mkuu  Welles,amewashauri maaskofu warudie katika uongofu wa Ubatizo ili kuweza kufikia ushiriki wa kina wa utume kimisionari na ambao kwa dhati ndiyo tabia ya Yesu , kwa maana Yesu ndiye mzizi amethibisha.  Ni wito wa kina katika huduma ya kiaskofu na siyo kwamba kwa kuwekwa wakfu mara tatu kwa kwa njia ya  Roho Mtakatifu katika vipindi vya daraja kuanzia ushemasi, ukuhani hadi uaskofu vinahakikishia utakatifu tayari, hapana, badala yake  amesema, ni uzoefu wa kila siku na wa kuendelea na uongofu.

Akikumbusha Injili ya Luka, Askofu Mkuu Welles ameeleza katika mkutano huo kuwa aliye mkuu kati yao, lazima awe kijana zaidi na kuwa kiongozi anayetoa huduma. Ameuliza swali, je ni nani aliye mkubwa kati ya yule aliye kwenye meza na yule anayehumu? Kuwa mfano hai, maana yake ni kurudi katika ukweli wa Injili na tokea hapo kiini cha utume wa Kanisa ni  kuinjilisha. Utume, hata hivyo, haubadiliki kwa wakati na nafasi, na zana zake sio hizo, na ndiyo hivyo, hata kwa maaskofu, haiwezekani kuendana na nyakati za kufikia mafundisho hayo yote ambayo yanahitaji nuru ya Injili amesema.

Akimnukuu Papa Paul VI, anasema alionesha  kazi kubwa ya kitume ambayo maaskofu wanaitwa katika kufundisha, kutawala na kutakasa. Lakini yote hayo yanapitia katika matendo ya maadhimisho ya Ekaristi, kupitia katekesi, masifu ya kila, kutafakari na ili waweze awali ya yote kuwa watu wa sala walio hai kupitia Habari Njema na  ambayo iliwekwa  kwenye maisha yao na katika ulimwengu.

Balozi hatimaye amezungumzia juu ya kipeo cha kiroho na cha makuhani kwa kusisitiza kuwa, utoaji wa huduma siyo mkataba wa kazi, bali ni zawadi inayotolewa bure na ambayo inahitaji kulindwa. Kipeo cha ukosefu wa miito na ambacho kinaonesha kwa wale wanaoacha, kinapaswa kutoa chachu na mwamko wa kujiuliza maana ya kipeo hicho kwamba: "Je tungeweza kufanya nini kwa ajili ya kukidhi haja ya uchaguzi wa huduma kwa watu wa Mungu? Vile vile kufungamanisha na hilo amezungumzia kidogo juu ya furaha. Balozi amesema "ikiwa tunataka kujua furaha ya Yesu na kuipeleka kwa wengine, ni lazima kutambua kuwa inatuhusisha, itatusukuma zaidi ile nguvu na uhakika wa wakati uliopita, kuelekea uhuru wa Roho Mtakatifu ambaye anasukuma mahali tusipojua na wale kwenda tusikokujua wenywe!

23 January 2020, 15:07