Noeli iwe  fursa ya kupyaisha matumaini katika nchi inayoteseka kwa mujibu wa Kardinali Urosa askofu Mkuu mstaafu wa Venezuela katika fursa ya siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana Noeli iwe fursa ya kupyaisha matumaini katika nchi inayoteseka kwa mujibu wa Kardinali Urosa askofu Mkuu mstaafu wa Venezuela katika fursa ya siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana 

Venezuela:Kard.Urosa amesema Noeli ni fursa ya kupyaisha matumaini katika nchi iliyopiga magoti!

Kardinali Jorge Urosa Savino,Askofu Mkuu wa Msataafu wa Caracas amesema kuwa Noeli ni fursa ya kupyaisha matumaini katika nchi ambayo inateseka sana na zaidi ni wale walio maskini zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika fursa ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bwana ni lazima kuongeza nguvu zaidi ya kuwa na matumaini katika mtazamo wa hali halisi iliyo ngumu na inayozidi kuelemea siku hadi siku nchini Venezuela. Siku kuu hii iwe ni fursa ya kuwa na uhai zaidi wa matumaini katika nchi inayozidi kuteseka. Huo ni uthibitisho wa wa kutoa moyo wa Kardinali Cardinale Jorge Urosa Savino, Askofu Mkuu wa Mstaafu wa Caracas, ambaye amelezea hali halisi mbaya na kwamba wanaoteseka ni maskini zaidi.

Hali halisi nchini Venezuela inazidi kuwa mbaya kwa mtazamo wa mambo mengi anasisitiza Kardinali Urosa. Uchumi unazidi kuwa mbaya zaidi  kutokana na kutojali kushuka kwa bolivar, yaani thamani ya fedha ya nchi hiyo. Dola moja ilikuwa na thamani ya bolivar 60 kwa miezi 16 iliyopita na sasa imefikia kiasi cha 47,000. Hii ina maana kuwa gharama za maisha kwa namna ya pekee chakula zimezidi kuwa ngumu sana anathibitisha Kardinali Urosa Savino. Aidha anafikiria suala hili kama kitu kisichoweza kuelezeka hasa juu ya kutopatikana  mambo mengi msingi na uendeshaji wa serikali kwa ajili ya kutatua hali halisi nchini Venezuela. Hii ina maana ya kuona nchi ambayo ni yenye kujulikana kwa utuoaji wa mafuta, lakini hadi sasa  inakosa hata petroli na gesi ya nyumbani. Ni jambo la la  aibu sana, anasisitiza Kardinali Urosa!

Ni hali halisi mbaya sana kwa mtazamo na zaidi wanaoteseka ni walio maskini ameongeza kusema askofu Mstaafu wa Caracas.  Na katika matazamio ya sherehe za kuzaliwa kwa Bwana , kwa waamini wote na watu wenye mapenzi mema wanaalikwa kupyaisha matumaini. Hata katikati ya matatizo hayo, amesema ni lazima waongeze bidii katika dini yao na kwenda kanisani lazima kuudhuria misa ya kila Jumapili na kupokea sakramenti ya kitubio na Ekaristi huku wakimtumainia Mungu! Vile vile anawaasa waamini kwamba waishi kwa kina ule upendo kindugu hasa kwa wale wote wanaohitaji msaada.

24 December 2019, 09:04