Vatican News
Maaskofu nchini Bolivia wanasema "Tumeishi kwa vurugu,ghasia, ufisadi wa kisasa na ulaghai kwa upande wa taasisi mbalilmbali. Tumeona vifo vingi vya ndugu au majeruhi".Ni wakati wa kujenga amani. Maaskofu nchini Bolivia wanasema "Tumeishi kwa vurugu,ghasia, ufisadi wa kisasa na ulaghai kwa upande wa taasisi mbalilmbali. Tumeona vifo vingi vya ndugu au majeruhi".Ni wakati wa kujenga amani. 

Bolivia:maaskofu wanatoa wito wa kuwa na amani!

Wakati wa kuhitimisha mkutano wao maalum wa Baraza la Maaskofu nchini Bolivia wametoa waraka kwa waamini wakiufungua kwa kutumia maneno ya Nabii Isaya 9,1:"watu waliotembea katika giza wameona mwanga mkubwa”.Ni waraka ukiwatakia matashi mema ya furaha,matumaini na amani ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana inayokaribia lakini pia kuangazia hali halisi ya nchi hiyo ya sasa.

Watu waliotembea katika giza waliona mwanga mkubwa” katika maandishi hayo ya Nabii Isaya (9,1), ndiyo yanafungua ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Bolivia  (Ceb), uliosambazwa mara baada ya kumaliza mkutano wao maalum.  Mkutano huo ulifanyika tarehe 11 na 12 Desemba 2019 huko Tarjia.  Katika ujumbe huo maaskofu wanawaelekea waamini awali ya yote wakiwatakia matashi mema ya furaha, matumaini na amani ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ambayo inakaribia. Na hasa kwa kutazama unyenyekevu wa Kristo ambaye alijifanya mdogo kama Mtoto mchanga  kwa ajili ya kukutana na kila mti ambaye unaweza kujivua kila aina ya kiburi ili kuweza kugeuka kuwa mnyenyekevu zaidi na mwamini zaidi. Furaha ya Kuzaliwa kwa Bwana iweze kuwapatanisha na kuwapa amani huku ikiwasaidia kusamehana kwa pamoja, wanaandika maaskofu wa Ceb.

Mtazamo wa hali halisi ya nchi

Katika Ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Bolivia wameweza kupanua mtazamo wao hasa wa  hali halisi ya nchi yao na kusema: “mwaka huu nchini Bolivia tumeona na kuishi kipindi kigumu na maalumu, kwa ishara wazi za matumaini, lakini pia hata za giza”. Tumeishi kwa vurugu, ghasia, ufisadi wa kisasa na ulaghai kwa upande wa taasisi mbalilmbali. Tumeona vifo vingi vya ndugu au majeruhi”. Na kwa maana hiyo maaskofu wanaonesha mshikamano wao kwa mateso ya familia waliokumbwa katika mikasa hiyo ya ghasia. Waraka wa Maaskofu unafika hata hivyo baada ya maandamano mengi ya kupinga ambayo yalitokea baada ya uchaguzi mkuu wa rais kunako tarehe 20 Oktoba iliyopita ambapo alishinda kwa takriban nusu ya asilimia kutoka kwa rais aliyekuwa madarakani  Bwana Evo Morales. Hata hivyo mpinzani wake, msaidizi wa mgombea Carlos Mesa, alikuwa umekemea juu ya udanganyifu, ambao ulifuatiwa na mapigano ya barabarani na uonevu kwa upande wa polisi nchini humo. Mwishowe, Morales aliachana na miaka kumi na tatu baada ya muhula wake wa kwanza kunako 2006, na  akajiuzulu. Kwa viongozi wa Tume ya Uchaguzi, badala yake waliwekwa pingu mikononi kutokana na udanganyifu wa uchaguzi uliofanywa. Hatimaye  seneti ya upinzani Bi Jeanine Anez wa chama cha Unidad cha kidemokrasia ndiye aliyetajwa kuwa rais wa mpito wa Bolivia.

Mwaka 2020 uwe wa haki uhuru na upendo kwa wote

Pamoja na hayo yote maaskofu wanasema: “Lakini Kanisa Katoliki la Amani  halisahau kutaja matukio mazuri ambayo yameonyesha wito wa demokrasia wa watu wetu”. “Tumeona  ​​maandamano ya amani, imani ya  umma, katika sala na imani ya vijana kuwa mstari wa mbele; ishara ambazo zinatujaza tumaini na kuturuhusu tuwe na  tumaini la siku bora zijazo kwa nchi yetu”. Kufuatia na sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, Maaskofu nchini Bolivia wanasema inachukua maana yake maalum ya neema katika imani. Kama wakristo wabatizwa, mitume wamisionari wa Yesu Kristo  wanaalikwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu katika Taasisi za Nchi, katika familia zao na katika maisha yao binafsi huku wakiruhusu msamaha na mapatano ambayo watu wote nchini Bolivia wanahitaji. Ni matarajio yetu ya haraka ya kuweza kuona ujenzu wa nchi ya Bolivia inaungana katika Mungu wa maisha na kwa maana ya kuunganisha zaidi kuliko kutengana. Muundano huo unajikita katika historia ya pamoja na wakati endelevu wa pamoja, Mwokozi wa pamoja na kazi ya pamoja. Hivyo ndivyo vya kujenga nchi katika haki na maendeleo. Maaskofu wanatoa baraka wakiwa na matumaini ya kwamba mwaka 2020 uweze kuwa wa kweli, wa haki , wa uhuru na upendo kwa wote!

14 December 2019, 14:42