Tafuta

Vatican News
Nchini Benin imetajwa kuwa, baadhi ya watoto ni wachawi na kwa maana hiyo wanahukumiwa kuuawa Nchini Benin imetajwa kuwa, baadhi ya watoto ni wachawi na kwa maana hiyo wanahukumiwa kuuawa 

Benin:jitihada za wafransiskani dhidi ya kasumba mbaya ya uchawi!

Imetajwa kuwa,watoto ni wachawi na kwa maana hiyo kuhukumiwa kuuawa. Hii ni huzuni inayo endelea kwa watoto waliozaliwa katika baadhi ya mikoa ya Benin.

Na Padre Angelo Shikombe; -Vatican

Imetajwa kuwa, watoto ni wachawi na kwa maana hiyo kuhukumiwa kuuawa. Hii ni huzuni inayo endelea kwa watoto waliozaliwa katika baadhi ya mikoa ya Benin. Dhambi yao pekee ipo mbele ya macho ya baadhi ya makundi ya kikabila dhidi ya  watoto wanaozaliwa njiti au kuambatana na kifo cha mama au kuzaliwa na ulemavu. Hali hii ya imewapa wasiwasi katika nchi hii ya Benin na ambayo imezidi kuku ana kuwafanyaShirika lisilo la kiserikali kutoka Ufaransa ambalo linajumuisha Mashirika 12 ya kidini mahalia yenye kuwa na msukumo wa roho ya kifransiskani na ambayo imetafuta namna ya kupambana na hali hii tangu mwaka 2012.

Hatua ya kwanza ilirekodiwa mnamo 2015, wakati uhalifu wa utapeli wa kitamaduni huo uliopitishwa na wabunge, kupitia kifungu cha  340 cha sheria ya 8 Desemba 2015 inayohusiana na Utaratibu wa watoto nchini. Lakini haikutosha, matukio ya watoto kusingiziwa ni wachawi, inazidi kuendelea sasa katika makundi ya kikabila kwenye Wilaya za  Atacora, Alibori, Borgou na Donga”, amethibtisha Mkurugenizi  wa Shirika hili lisilo kuwa la kiserikali . Padre mkapuchino Auguste Agounkpé. Kwa kuongezea, anasema kulingana na utafiti uliofanywa mwaka wa 2018 na Shirika hilo hilo  kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ufaransa, zaidi inaibuka kuwa katika Manispaa kumi na moja kaskazini mwa nchi, karibu watoto wachanga kumi kati ya mia wanatuhumiwa kwa wachawi. Na kati ya hawa kumi, mmoja anapona na kifo.

Kufuatia na hali hiyo ndipo jitihada za kifransiskani  nchini Benin kwa ajili ya kutaka kuokoa maisha ya watoto hawa. Kwa namna ya pekee wanatafuta kupambana na utamaduni wa kifo, kwa njia ya kampeni ya mafunzo na uhamasishaji wa watu mahalia. Kunako machi 2012 zaidi katika nchi za Afrika wamefanya mkutano wa kitaifa kwa kujikita na mada ya watoto wachanga dhidi ya kiutamaduni kandamizi ili kujaribu kumaliza kabisa uzushi huu. Watoto wachanga ambao tunaweza kuokoa - anaelezea Padre Agounkpé - wanakaribishwa na familia za Kikristo huko Benin au kupelekwa nje ya nchi.

Shirika lisilo la kiserikali lilianzishwa kunako Aprili 2012 huko Cotonou na wamisionari wa Franciskani nchini linaloratibiwa na Padre Agounkpé pia, ni miongoni mwa malengo ya utunzaji wa watoto katika hali ngumu, masomo ya shule kwa watoto, upatikanaji na utunzaji wa maskini na utekelezaji wa mapendekezo ya  Umoja wa Mataifa juu ya haki za mtoto na juu ya haki ya elimu na habari.

20 December 2019, 15:07