Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Julius Yakubu Kundi kuwa Askofumpya wa Jimbo Katoliki la Kafanchan, nchini Nigeria Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Julius Yakubu Kundi kuwa Askofumpya wa Jimbo Katoliki la Kafanchan, nchini Nigeria 

Padre Julius Kundi ateuliwa kuwa Askofu Kafanchan, Nigeria

. Askofu mteule Julius Yakubu Kundi alizaliwa mwaka 1968. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo la Kaduna na kunako tarehe 5 Desemba 2000 Jimbo jipya la Zaria lilipoanzishwa akajiunga nalo. Tangu wakati huo, amekuwa Paroko usu na Paroko kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2003. Kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2006 alijiendeleza na masomo huko Port Harcourt.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu ameteuwa Mheshimiwa sana Padre Julius Yakubu Kundi kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kafanchan lililoko nchini Nigeria. Askofu mteule Julius Yakubu Kundi alizaliwa kunako tarehe 15 Februari 1968. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, tarehe 14 Juni 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya huduma Jimbo Katoliki na kunako tarehe 5 Desemba 2000 Jimbo jipya la Zaria lilipoanzishwa akajiunga nalo. Tangu wakati huo, amekuwa Paroko usu na Paroko kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2003. Kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2006 alijiendeleza na masomo huko Port Harcourt.

Askofu mteule Julius Yakubu Kundi Aliporejea kutoka masomoni akapangiwa kuwa Paroko, Gambera msaidizi wa “. St. Josephs Minor Seminary” , Msimamizi wa Kanisa kuu la Kristo Mfalme, Jimbo Katoliki la Zaria, Mchumi wa Jimbo na Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Zaria, Gambera Msaidizi na Mlezi Seminari kuu ya Good Shepherd iliyoko Kaduna, Msimamizi wa maisha ya kiroho wa Jeshi la Polisi huko Zaria. Kati ya Mwaka 2017 hadi mwaka 2018 akateuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya St. John huko Muchia na tangu mwaka 2018 amekuwa ni Paroko usu katika Parokia ya “Our Lady of the Lake”, Jimbo Katoliki la Phoenix, nchini Marekani wakati wa mapumziko yam waka mmoja.

 

 

 

12 December 2019, 14:39