Tafuta

Vatican News
Waratibu na wakurugenzi wa kichungaji wa ofisi za maendeleo na huduma ya Kanisa katoliki nchini Ethiopia wahimizwa kutoa ushuhuda kwa ajili ya kutangaza na kuinjilisha ufalme wa Mungu Waratibu na wakurugenzi wa kichungaji wa ofisi za maendeleo na huduma ya Kanisa katoliki nchini Ethiopia wahimizwa kutoa ushuhuda kwa ajili ya kutangaza na kuinjilisha ufalme wa Mungu  

Ask.Bergamaschi:Huduma ya maendeleo ni ishara ya upendo wa Mungu!

Askofu Roberto Bergamaschi,Msimamizi wa kitume huko Hawassa nchini Ethiopia katika hotuba yake kwenye mkutano wa waratibu wa kichungaji na wakurugenzi wa ofisi ya maendeleo na huduma ya Kanisa Katoliki nchini Ethiopia amesema huduma ya maendeleo ni ishara ya upendo wa Mungu na hivyo Watu wote wanaalikwa kuwa mashuhuda wa upendo wa Mungu na kushirikishana na wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Roberto Bergamaschi, Msimamizi wa kitume huko Hawassa nchini Ethiopia katika hotuba yake kwenye mkutano wa waratibu wa kichungaji na wakurugenzi wa ofisi ya maendeleo na huduma ya Kanisa Katoliki nchini Ethiopia, amethibtisha kwamba Kanisa halipaswi kujitambulisha kama wakala wa maendeleo bali ni kuhudumia kwa roho ya Kristo. Na utume  wake msingi ni ule wa kuinjilisha. Amesisitiza hayo katika mkutano uliofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Desemba 2019 huko Hawassa.

Katika hotuba yake Msimamizi wa kitume amesisitiza kuwa kila kitu kinachofanywa ni kwa ajili ya utangazaji wa Ufalme wa Mungu na kwa ajili ya wokovu wa Watu wake. Ikiwa watu wanaona Kanisa na huduma yake, wanapaswa kushukuru Mungu na siyo taasisi zao au mtu binafsi. Watu wote wanaalikwa kuwa mashuhuda wa upendo wa Mungu na kushirikishana na wengine, kwa mana huduma ya maendeleo ni ishara ya pendo wa Mungu!

Katika mkutano wao, washiriki wameweza kujadiliana ni kwa namna gani wanaweza kufanya maamuzi na maelekezo yaliyotolewa katika Mkutano wa Mwisho wa Baraza la Maaskofu nchini Ethiopia ambao umefanyika huko Meki kuanzia tarehe 9 hadi 13 Desemba 2019. Kwa namna ya pekee katika Mkutano huo pia walijikita kugusia kuhusu namna gani ya  kukarabati taasisi ya Kanisa Katoliki ili kuboresha utume wa uinjilishaji na kwa ajili ya kukuza uwajibikaji kiuchumi, kuwa na uwazi na hatimaye kuweza kufikia namna ya kujiendeleza  na kujitosheleza!

23 December 2019, 14:28