Tafuta

Vatican News
Katekesimu ya Kanisa Katoliki imetafsiriwa kwa lugha  Umbundu ambayo ni lugha ya pili nchini  Angola baada ya lugha ya kwanza ya kireno inayozungumzwa Katekesimu ya Kanisa Katoliki imetafsiriwa kwa lugha Umbundu ambayo ni lugha ya pili nchini Angola baada ya lugha ya kwanza ya kireno inayozungumzwa 

Angola:Katekisimu ya Kanisa Katoliki imetafsiriwa katika lugha ya Umbundu!

Kuanzia sasa na kuendelea waamini wa Kanisa Katoliki nchini Angola wanaweza kujisomea na kujifunza mengi ya imani yao kupitia katika Katekesimu ya Kanisa Katoliki iliyotafsisiriwa kwa lugha yao ya Umbundu, lugha ya pili nchini humo baada ya kireno.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Umuhimu wa habari mpya kwa waamini Katoliki nchini Angola ni kwamba tangia sasa na kuendelea, wataweza kusoma “Katekisimu ya Kanisa Katoliki” iliyotafsiriwa katika lugha yao ya Umbudu ambayo ni lugha ya pili inayozungumzwa nchini humo baada ya lugha ya Kireno. Kazi ya kutafsiri imewakilishwa na Askofu Mkuu mstaafu Francesco Viti, wa Huambo. Akizungumza wakati wa uwakilishi wa tafsiri hiyo Askofu Mkuu mstaafu Viti amesema kuwa Katekisimu ni maandishi yenye uhakika na wa dhati kwa ajili ya mafundisho ya Kanisa Katoliki. Shukrani kubwa kwayo ambapo inawezekana kwa hakika kujua kile ambacho Kanisa linakiri na kuadhimisha, kuishi na kusali katika maisha ya mwamini ya kila siku.

Lugha ya Umbundu inazungumzwa na watu milioni 6 hivi

Na kwa sababu hii, Askofu Mkuu Mstaafu Viti ameamua kutafsiri Katekisimu hiyo katika lugha ya Umbundu. Aidha wakati wa kusungumza kuhusu hilo ameweza kubainisha kwamba kazi hiyo ilikuwa ni ngumu, kwa sababu inagusa  maneno ya kifalsafa, kitaalimungu, kisayansi na elimu ya viumbe. Lugha ya Embundu inazungumzwa sana katika Mkoa wa Magharibi mwa Angola karibia watu milioni 6 hivi. Na lugha hiyo imewekwa katika makundi kama lugha ya kibantu na ambayo inajiunda katika makundi madogo madogo zaidi ambayo yanazungumza lugha hiyo katika nchi za Afrika ya Kusini. Umbundu pia inaweza kutamkwa “mbundu huko kusini ili kutofautisha na Kimbundu au mbundu ya Kaskazini mwa nchi hiyo ambayo inazungumza katika maeneo ya Luanda mji Mkuu wa Angola.

Tafsiri ya Lugha ya kiajemi ya Katekesimu ya Kanisa Katoliki

Hata hivyo ni lazima kukumbuka kuwa lugha ya Umbundu ndiyo ya mwisho katika kazi ya kutafsiri Katekisimu  katika mchakato wa kipindi hiki kuhusiana na maandishi ya Katekisimu. Kati ya lugha ambazo zinapaswa kukumbukwa pia ni ile ya kiajemi, ambayo ilifanyika kunako mwaka 2014 na msomi mmoja mwislam wa kishiiti wa Chuo Kikuu cha Dini kinachojulikana huko Qom, nchini Iran. Aliyeoongoza kazi hiyo ya kiajemi, katika utangulizi  wake alikuwa ni Hayati Kardinali Jean-Louis Tauran, aliyekuwa ni Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Kazi hiyo ilipitishwa rasimu ya kwanza na Mtakatifu Yohane Paulo II na Katiba ya Kitume ya Fidei Depositum  ya tarehe  11 Oktoba 1992. Na “Katekisimu ya Kanisa Katoliki” ilianza kutumika rasmi kunako tarehe 15 Agosti 1997 kwa Waraka wa Kitume wa Laetamur Magnopere ya Mtakatifu Yohane Paulo II.

Nyongeza mwaka 2005 na 2018

Kunako mwaka 2005 chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, walichapisha na kutangaza nyongeza, na wakati tarehe 2 Agosti 2018 Baba Mtakatifu Francisko aliidhinisha rasimu mpya ya kifungu cha 2267 cha  maandishi ili kudhibitisha kwamba “adhabu ya kifo haikubaliki kwa sababu ya umakini wa kutokiuka na hadhi ya mtu” na tunasisitiza kwamba Kanisa “linajibidisha kwa uamuzi wa kukomesha kwake katika ulimwengu wote”. Zaidi ya hayo tarehe 26 Novemba 2019, wakati wa hitimisho la Ziara ya Kitume ya nchini Thailand na Japan, kama kawaida ya kufanya mkutano wake na waandishi wa habari ndani ya ndege ya kurudi Roma, Baba Mtakatifu Francisko alithibitisha kuwa: “Matumizi ya silaha za nyuklia ni tabia mbaya, kwa hivyo lazima iende katika Katekisimu ya Kanisa  Katoliki na sio matumizi tu, hata milki, kwa sababu ajali au uwenda wazimu wa baadhi ya watawala fulani unaweza kuharibu ubinadamu.”

14 December 2019, 14:19