Tafuta

Kwa kipindi kirefu hakuna mvua na imesababisha mateso ya watu  nchini Australia,kwa maana hiyo Maaskofu wametangaza mwezi Novemba kuwa maalum kwa ajili ya kuomba zawadi ya mvua Kwa kipindi kirefu hakuna mvua na imesababisha mateso ya watu nchini Australia,kwa maana hiyo Maaskofu wametangaza mwezi Novemba kuwa maalum kwa ajili ya kuomba zawadi ya mvua 

Kanisa nchini Australia linaomba kwa Mungu zawadi ya mvua!

Kufuatia na uhaba wa mvua kwa kipindi kirefu katika maeneo nchini Australia,Kanisa limeamua kuweka Mwezi Maalum wa Novemba kwa ajili ya kuomba kwa Mungu zawadi ya mvua.Askofu Columba Macbeth-Green,wa Jimbo la Wilcannia-Forbes anawaalika watu wote na zaidi ambao wana fursa ya maji ya kutosha wawe na mshikamano kwa wanaoteseka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katisa Katoliki la Australia limejiwekea mpango mkakati wa sala kwa Mwezi Novemba 2019 kwa ajili ya watu wanaoteseka kwa sababu ya ukame uliokumba baadhi ya maeneo ya nchi. Kwa mujibu wa habari za wanahewa kitaifa nchini wanathibitisha kuwa  badhi ya maeneo ya Australia Mashariki, ndiyo wamekumbwa na ukame wa kutisha kwa karibia miaka 100 hivi. Kwenye mwaliko wa Baraza la Maaskofu Australia, wanasema maparokia, mashule, familia na jumuiya zote katoliki katika nchi hiyo wajikite kwa dhati katika Kampeni ya Kitaifa kuhusu mamobi kwa ajili ya zawadi ya mvua dhidi ya ukame.

Watu wote wawe na utambuzi na mshikamano kwa wanaoteseka

Na kwa mujibu wa Askofu Columba Macbeth-Green, wa Jimbo la Wilcannia-Forbes amesema  wale wanaoishi mahali ambapo kuna maji ya kutosha au kutosha kidogo, utafikiri hawatambui ni jinsi gani kuna mateso yanayosababishwa na ukame na jambo hili linasababisha kuongezeka kwa matatizo kwa wale ambao tayari wanateseka na ukame huo. Waamini walei, watawa, mapadre, maaskofu na Kanisa zima la Australia lazima wawe na mshikamano na watu ambao wamekumbwa na ukosefu wa maji, wakati wakiomba sala zao pia wajikite katika matendo ya dhati.

Maombi ya sala ni jibu katika kazi ya pamoja

Askofu katika jimbo hilo linalofunika mji Mpya wa Galles ya Kusini ukijumuishwa na baadhi ya maeneo ndiyo yenye uhaba wa mvua na maji kwa ujumla katika nchi na hivyo anasisitiza kwamba, Mwezi Maalum wa sala ni jibu la kazi mahalia ya pamoja  ambayo inajikita ndani ya jumuiya zilizo kumbwa na ukosefu wa mvua! Hali halisi za kidini, kisiasa na serikali zinajitahidi kufanya kazi maalum ya kuwasaidia watu kwa njia ya zana, huku wakitoa hata msaada wa kifedha na kuwasaidia kwa mahitaji ya kihisia na kiroho kwa watu. “Lakini katika mantiki ya imani ya watu, sehemu kubwa ya jibu letu katika tatizo ni kujiunda ndani ya  maombi”, amesisitiza.

Hata katika Biblia inaonesha kuwa mvua ni zawadi

Akiendelea na maelezo kuhusu ukame, Askofu Macbeth-Green amesema hata katika Biblia inawakilisha historia kuwa mvua ni kama zawadi ya Mungu kwa ajili ya watu wanaoteseka. Kipindi cha ukame kama kile ambacho wanafanya uzoefu hadi sasa, waamini wote wanapaswa kusali kwa Mungu kwa ajili ya zawadi ya mvua. Bwana mwenye nguvu ana uwezo wa kutofautisha kila ardhi iliyo kavu hata kuweza kutuliza nyoyo za watu wengi wanaoteseka, amehitimisha.

05 November 2019, 12:26