Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa na vijana wakati waziara yake ya kutume kunako Julai 2015 Baba Mtakatifu Francisko akiwa na vijana wakati waziara yake ya kutume kunako Julai 2015 

Paraguay:2020 ni wa Neno la Mungu.Chombo mwafaka katika huduma ya kichungaji!

Kanisa Katoliki nchini Paraguay kwa mwaka 2020 utaongozwa na mada"Neno la Mungu ni kisima,zana na chambo mwafaka kwa ajili ya huduma kichugaji kwa watu wetu”.Na kwa mujibu wa Rais wa Baraza la maaskofu nchini humo anasema kipimo cha mafaniko ya shughuli hizo,kitaonekana kutokana na uwezo wa kusikiliza wakiangazwa na Neno lililofanyika mwili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hitimisho la mwaka wa Tatu kwa vijana, jitihada za kuwa Kanisa linalotoka nje kwa mujibu wa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko, Mwaka wa Neno la Mungu, ndiyo mada msingi ambazo zimeguswa na Askofu Adalberto Martínez Flores, wa  Villarrica, ambaye ni Rais wa Baraza la Maakofu Katoliki Paraguay, wakati hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wao wa mwaka wa Baraza la Maaskofu nchini humo. Mkutano wa unafanyika sehemu ya Luque, katika Jimbo Kuu Katoliki la  Asunción, kuanzia tarehe  4 hadi 8 Novemba 2019. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la habari za kimisionari Fides, zinasema, mkutano wao pia utafikiria mada zinazohusiana na hali halisi ya kijamii na kikanisa katika nchi hiyo. Katika ajenda ya mkutano huo pia kuna ripoti ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Asunción, Askofu Mkuu Edmundo Valenzuela, kuhusiana na Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Kanda ya Amazoni ambaye pia alishiriki na ripoti ya Askofu Pierre Jubinville, wa Jimbo la Mtakatifu Pedro, kuhusu hatua ya miaka mitatu iliyokuwa imetotolewa kwa ajili ya kujikita hatua na safari ya kiroho kwa vijana.

Hija ya vijana Caacupe na kuufunga miaka mitatu ya safari ya vijana 

Tarehe 30 Novemba kutakuwapo na hija ya vijana huko  Caacupé, mahali ambapo wanatarajia kufunga hatua ya mchakato wa safati ya kiroho kwa miaka mitatu ya vijana. Akielezea juu ya hatua hiyo ya miaka mitatu amesisitiza Rais wa Baraza la Maaskofu wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo kwamba imekuwa kipindi cha neema, na ambacho kimeanza kutoa matunda tayari kwa maana ya kuhamasisha katika changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo; katika matendo ya kichungaji ya Kanisa na huku wakifungua njia mpya za kuwasindikiza kwa karibu na kukabiliana mahitaji yao, ndoto na matumaini ya kuwa raia wema na wafuasi wa kimisionari wa Yesu Kristo; aidha kwa ajili ya kuhamasisha Kanisa linalotaka kutoka nje, na katika huduma ya jamii mpya inayoangazwa na thamani msingi za Injili.

Kusindikiza ndoto za Papa kuhusu Kanisa moja la kimisionari

Katika mapendekezo hayo Askofu Martínez Flores amewashauri Maaskofu na makuhani wote ili kuwa makini katika uhusiano na waamini walei kwa ujumla na vijana kwa namna ya pekee huku akiwaalika waweze  kutembea nao kuelekea katika Kanisa la upamoja. Kama Wachungaji wa Kanisa maalum ambao ni mahujaji wa Paraguay,  Askofu anabainisha kwamba, wanapaswa kusindikiza ndoto ya Baba Mtakatifu ya kuwa Kanisa moja la Kimisionari, lenye uwezo wa kusikiliza na kusindikiza kilio cha masikini, ambao wanapaza sauti zao ili wapate maisha yenye hadhi na timilifu, kwa kutumia majengo yao na zana zote walizo nazo.

Shughuli za kichungaji nchini Paraguay 2019-2020

Askofu Adalberto Martínez Flores kwa maelezo hayo  amebainisha juu ya shughuli za Kanisa la Paraguay kwa ajili ya mwaka 2019-2020 waliyokuwa wameamua katika Mkutano uliopita, na ambao unajikita na mada: “Neno la Mungu ni kisima, zana na chambo mwafaka kwa ajili ya huduma ya kichugaji kwa watu wetu”. Zaidi ya hayo, anasema matendo yote ya Kanisa kwa mwaka 2020 yatakuwa yanaelekeza na kuungozwa na Neno la Mungu. Kipimo cha mafaniko ya shughuli zao, itaonekana kutokana na uwezo wao wa kusikiliza huku wakiangazwa na Neno lililofanyika mwili.

05 November 2019, 14:22