Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa ndani ya makatakombe ya Priscilla,Roma tarehe 2 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko akiwa ndani ya makatakombe ya Priscilla,Roma tarehe 2 Novemba 2019  (ANSA)

Asili ya makatakombe na historia yake kuthibitisha imani ya Wakristo wa kwanza!

Wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kumbu kumbu ya Marehemu wote tarehe 2 Novemba 2019,Baba Mtakatifu Francisko aliadhimisha Misa Takatifu katika moja ya Makatakombe ya Priscillla mjini Roma.Je historia ya makatakombe hayo ni ipi?Katika makala hii utajifunza jambo muhimu na juu ya urithi tulio nao wa wakristo wa kwanza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 2 Novemba 2019 ilikuwa ni siku ya kumbu kumbu ya marehemu wote na kama ilivyo kwa kila mwaka katika mwezi wa Novemba, umewekwa kwa ajili ya kuwakumbuka kwa karibu watu ambao wametutangulia katika raha ya milele. Katika siku hiyo kwa ajili ya kuwaombea marehemu wote, Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi  jioni alikwenda kuadhimisha Misa Takatifu katika moja ya Makatakombe yaliyoko mjini Roma (Catacombs of Rome).  Kufuatia na neno Katakombe ambalo siyo geni lakini hata kuwa la  kawaida kusikika kwa walio wengi, leo hii ninapenda kutumia fursa hii kulizungumzia kwa kifupi katika makala  ambayo  nimeeita “historia ya Makatakombe”.  Hata hivyo wazo hili kiukweli limenijia tu mara baada ya kuombwa nielezee juu yake kutokana na kuandikajuu ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyofanya katika Makatakombe ya Priscilla mjini Roma.

Makatakombe yanafafanua imani na maisha ya wakristo wa kwanza 

Awali ya yote nikirejea katika mahubiri yake bila kuandika, Baba Mtakatifu Fracisko  siku hiyo alianza kusema kuwa  maadhimisho ya kumbu kumbu ya marehemu wote katika katakomba hiyo, kwake yeye ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kuingia na ulikuwa mshangao kwake; na makatakombe hayo yanajifafanua kwa mambo mengi. Ni kufikiria maisha ya watu wale ambao walikuwa wanajificha, na ambao walikuwa na utamaduni huo wa kuzika watu wao na kuadhimisha Ekaristi ndani humo.  Ilikuwa ni kipindi kibaya cha kihistoria, lakini ambacho hakijaisha. Hata leo hii bado ni zaidi Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza. Makatakombe ni mengi katika Nchi nyingi mahali ambamo wanaingia ndani humo utafikiri  wanafanya sikukuu na kumbe wanaingia humo ili waweze kuadhimisha Ekaristi kwa sababu katika maeneo hayo au nchi hizo  hawaruhusiwi kufanya ibada zao. Hata leo hii wakristo wanateseka zaidi kuliko karne za kwanza alibainisha. Ndugu wasomaji na wasikilizaji wa Vatican news, kufuatia na maelezo hayo basi tuone asili ya makatakombe haya.

Asili ya Makatakombe 

Makatakombe yalianzishwa mjini Roma kati ya mwisho wa karne ya II na mwanzo wa Karne ya III baada ya Kristo (d.C), kutokana na  kuchaguliwa kwa Papa Zefìrino kunako mwaka  (199-217) aliweza kumkabidhi shemasi Callisti na ambaye baadaye yeye alichaguliwa kuwa  Papa kuanzia mwaka  (217-222).  Shughuli yake ilikuwa ni kusimamia makaburi yaliyokuwa katika njia ya Appia Roma, mahali ambapo walikuwa wamezikwa watu muhimu kama mapapa wa karne ya III. Matumizi ya kuzika watu chini ya ardhi ilikuwa tayari inajulikana hata kipindi cha “watrusiki (Etruscans) ambao walikuwa ni watu wa zamani sana kabla ya kuundwa Roma, na historia yake. Hawa waliunda ustaarabu mkubwa moyoni mwa nchi ya Italia, kwa kuweka misingi ya wakati ujao Barani Ulaya), pia walikuwapo wayahudi na waroma, lakini  teno la  kuingia kwa wakristo,wakaanzisha  makaburi chini ya ardhi, iliyokuwa  ngumu lakini inawezekana na  pana ili kuwawezesha jamii nzima ya kikristo katika mji kuwa katika jumuiya moja.  Jina la kizamani katika maeneo hayo liliitwa coemeterium, neno litokalo katika lugha ya kigiriki ikiwa na maana ya mahali pa kulala (Dormitory), ikiwa ni kutaka kusisitiza ukweli kwamba kwa Wakristo mazishi siyo kitu zaidi ya kupumzika kwa muda mfupi, huku wakingojea ufufuo wa mwisho. Neno katakomba, iliyopanuliwa kuwa na maana ya makaburi yote ya Kikristo ilikuwa inajieleza katika nyakati za zamani kwenye eneo tu  la Mtakatifu  Sebastian  kwenye njia ya Appia Roma.

Tabia za makatakombe

Katika maelezo yots hayo tunaweza kuona na kuthibitisha kwamba Makatakombe  kwa maana hiyo ni makaburi yaliyochimbwa kwenye ardhi yenye kuwa na mchanga au miambamiamba na mawe au kiurahisi kwenye ardhi lakini na thabiti hadi kuweza kuunda usanifu unapoingia ndani yake. Kwa sababu hiyo  makatakombe hupatikana hasa mahali ambapo kuna mchanga  mchanga, na katika hali hiyo kwa upande wa Italia makatakombe yanapatikana katikati, kusini na kwa ndani zaidi. Makatakombe hayo uhusishwa na uwepo wa ngazi mbalimbali na nyingi na barabara ndefu na makona ya hapa na pale yanayopelekea hata kuwapo na mwangwi, ni kama ilivyo kwenye migodi, njia ndefu nyembembe zilizochimbwa chini ya ardhi. Katika ukuta wa njia hiyo ndefu  kuna mfumo wa visanduku au sehemu za maziko ya Wakristo wa kawaida yaliyotengenezwa kwa urefu; kaburi hizi zimefungwa na marumaru au matofali. Vyumba vidogo vodogo hivyo vinawakilisha mfumo wa makaburi ya kinyenyekevu na wa heshima kuhusu hisia za jumuiya ambayo ilikuwa inaongoza Wakristo wa kwanza. Katika makatakombe hayo, hata hivyo, kuna pia kaburi ngumu zaidi, liitwalo  arcosolia, ambalo linahusisha kuchimba nguzo ya juu katika kesi ya mwamba na ambavyo ni vyumba vya mazishi halisi. (Marehemu walikuwa wakifungwa kwenye shuka kubwa aina ya nyuzi ya iitwayo Lino ambayo ilianza kutumika kwenye miaka ya 70 d.C . Ni nyuzi kongwe zaidi ya nguo zote ulimwenguni. Leo hii Jumuiya ya Ulaya inakumbuka kwa  ubora wa nyuzi, kutokana na kustahilimi kwa hali nzuri ya hali ya hewa na mchanga unaofaa. Aina ya mbegu za Lini zinalimwa nchini Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji, lakini pia hataPoland, Jamhuri ya Czech, na sehemu nyingine. Kwa maana hiyo kitambaa hiki kilikuwa maarufu sana katika maziko ya kwenye makatakombe.

Makatakombe nchini Italia na katika ulimwengu

Sehemu kubwa ya Makatakomba yanapatikana nchini Italia kwa maana inasadikika kwamba kuna makatako,mbo 60 mjini Roma na wengine yanapatikana  katika Mkoa wa Lazio. Nchini Italia makatakombe yanajulika sana hasa kusini mwa nchi, mahali ambapo udongo wake ni laini na wakati huo huo unarahisishwa uchimbaji wake. Makatakombe yaliyoko kaskazini ni yale yaliyoko kwenye kisiwa cha Pianosa wakati makuburi chini ya ardhi ni yale ya kaskazini mwa Afrika, hasa yaliyoko Hadrumetum huko Tunisia. Makatakombe mengine yanapatikana  katika eneo la Chiusi (Toscana; Todi –(Umbria); Amiterno na Aquila (Abruzzo); Napoli-(Campania); Canosa (Puglia); Venosa- (Basilicata); Palermo- (Sicilia); Siracusa -Marsala  na Agrigento;  Cagliari, S. Antioco- (Sardegna).

Sanaa ya makatakombe

Ndugu msikilizaji na msomaji, katika makatakombe inapatikana sanaa rahisi sana ambayo imeunda na sehemu ya hadithi kwa  mfano iliendelea tangu mwisho mwa karne ya II.  Zipo picha za kuchora ukutani, picha za kubandika vipande vidogo vidogo vya mawe au matofari na mapambo katika masanduku ya maziko. Vile vile  sanaa ndogo zilikuwa zinakumbusha hadithi za Agano la Kale na Jipya na kama kwamba kuwawasilisha mifano ya wokovu kwa wale walioongoka, vile vile waliwakilisha michoro ya  Yona aliyepona baada ya kumezwa na nyangumi na kubaki tumboni mwake  siku tatu ikiwa inaamanisha ufufuko wa Kristo. Aidha katika Agano la Jipya walichagua kuchora miujiza ya kuponywa wa kipofu, kiwete, mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu na ufufuko wa Lazaro, mwanamke mjane wa Naim na Mtoto wa Gairo, lakini pia hata matukio mengine kama vile mazungumzo ya mwanamke Msamaria na Yesu katika kisima na miujiza ya “wingi wa mikate”.

Sanaa ya kutumia ishara

Sanaa za makatakombe pia zinaonesha sanaa ya ishala, kwa maana kwamba dhana nyingine  ngumu iliweza kuonyweshwa kwa njia rahisi. Na ili kuweza kuonyesha Kristo  walitumia ishara ya ‘samaki’; ili kuwakilisha amani mbinguni walitumia mchoro wa ‘njiwa’; ili kuonesha imani thabiti  walitumia mchoro wa ‘nanga’. Mbele ya kifuniko cha Makaburi, mara nyingi waliweka hata alama za maana tofauti. Katika hali nyingine waliweza kuwakilisha chombo kilichokuwa kihusiana na taaluma aliyoifanya marehemu wakati wa maisha yake. Alama nyingine, ni kama glasi na mikate na vyungu ambavyo wakati mwingine vililetwa na chakula ili kula kwa pamoja kwa ajili ya heshima ya marehemu, katika chumba kilichokuwa kinaitwa kitulizo Michoro yote hiyo inaonekana wazi katika chumba cha kutulizo. Sehemu kubwa za alama zilikuwa zinaonyesha wokovu wa milele kama vile ‘njiwa’, ‘kiganja’, ‘tausi’, ‘ndege wa ajabu’ na ‘mwana-kondoo'.

MAKATAKOMBE
08 November 2019, 10:38