Maaskofu Sudan wawakumbusha wanasiasa sala ya Baba Mtakatifu
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Matumaini yetu ni kuwa viongozi wetu wa kisiasa katika nchi ya Sudan Kusini, serikali na vyama vya upinzani, sehemu kubwa ikiwa ni wakristo wanaweza kweli kujikita katika ya wito na ishara maalum aliyoifanya Baba Mtakatifu Francisko na kuwaomba wapeleke amani katika ndugu wa Sudan ya Kusini. Ni uthibitisho maneno ya Maaskofu wa Sudan na Sudan Kusini katika ujumbe wao uliosomwa wakati wa Misa ya tarehe 1 Novemba 2019 katika Makanisa yote ya Sudan.
Baba Mtakatifu aliwaomba viongozi wapeleke amani kwa watu
Hata hivyo ikukbukwe kuwa tarehe 11 Aprili 2019 wakati wa kuhitimisha mafungo ya kiroho katika Nyumba ya Mtakatifu Marta (Domus Sanctae Marthae), Vatican, kwa viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini, Baba Mtakatifu Francisko mbele yao alitoa tamko lenye nguvu kwa ajili ya wakati endelevu wa Serikali mpya ambayo ilikuwa izaliwe tarehe 12 Mei kwa kutumia ishara ya kuwabusu miguuu Rais wa Jamhuri Salva Kiir Mayardit, na Makamu Rais waliokuwapo na kati yao Riek Machar na Rebecca Nyandeng De Mabior.
Wasiwasi wa kuzuka mgogoro tena nchini Sudan Kusini
Uundaji wa serikali mpya ya umoja wa taifa lakini uliharishwa kwa mara nyingine tena na kwa sasa unatarajiwa tarehe 12 Novemba 2019, japokuwa Rais Salva Kiir amewezesha kufanya mafunzo ya mtendaji bila uwepo wa Riek Machar. Kama ndiyo hivyo, taarifa zinabainisah kwamba kuna wasiwasi mkubwa wa kuzuka tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, katika nchi ambayo imeshakuwa na mgongoro mkubwa kwa sababu ya athari za mzozo uliotokea kunako Desemba 2013, ambao unaongezewa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko yaliyoathiri maeneo makubwa ya Sudan Kusini.
Maaskofu wa Sudan wanasema tumeona majeraha ya watu
Kufuatia na wasiwasi huo Ujumbe wa Maaskofu wa Sudan Kusini wanathibitisha “Tumeona majeraha na majonzi ya watu wetu katika kambi za watu waliohamishwa ndani katika nchi zetu mbili na katika kambi za wakimbizi katika nchi jirani. Tunahisi na kushiriki hali ngumu za kiuchumi za watu wetu huko Sudan na Sudani Kusini”. Katika Ujumbe wao uliofikia Shirika la Habari za Kimisonari Fides, Maaskofu wanasisitiza kuwa mizizi ya migogoro inapaswa ikatwe kabisha kutokana na tamaa ya kutaka mabavu na utajiri, na ambayo kwa upande wao hutumia mgawanyiko wa koo na kikabila ili kushinikiza watu kupigana kati yao. Maaskofu wanahitimisha kwa kutoa wito juu ya umoja ili kukabiliana pamoja na shida hii ya tofauti ili kushirikishana rasilimali chache walizo nazo lakini kwa faida ya wote.