Tafuta

Vatican News
Baraza la maaskofu nchini Kenya wameanzisha Kampeni ya kupambana na ufisadi nchini humo itakayodumu kwa miezi sita Baraza la maaskofu nchini Kenya wameanzisha Kampeni ya kupambana na ufisadi nchini humo itakayodumu kwa miezi sita 

Tamko la Maaskofu Katoliki Kenya kuhusu kampeni ya kupinga rushwa na ufisadi

Sala ya Maaskofu nchini Kenye kwa ajili ya kupambana na ufisadi:Tunakuomba kwa unyenyekevu,gusa maisha yetu na yale ya viongozi wetu ili tuweze kuelewa kuwa ufisadi ni mbaya na kujitahidi kufanya bidii kuutokomeza.Kwa kila raia ambaye amepata kitu kwa njia ya ufisadi,Bwana,umpe roho ya ujasiri wa kurudisha bidhaa zilizoibiwa na kurudi kwako.Uwafanye viongozi wenye kuogopa Mungu waweze kututunza na kutuongoza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ufisadi ni uharibifu wa moyo, ndiyo kauli waliyoitumia Maaskofu wa Kenya kama njia ya kuzindua Kampeni ya kupambana na ufisadi ambayo itadumu kwa miezi sita. Katika mantiki ya kupambana dhidi ya ufisadi, kati ya mambo mengine Baraza la Maaskofu nchini Kenya wameamua kukataza kutoa michango ya pesa taslimu na badala yake kukubali tu wale wanaotoa michango yao kupitia njia ya kieletroniki ili kuwafuatilia wafadhili na kuepuka fedha zenye kuwa na mashaka. Uwakilishi wa maamuzi yao ulifanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2019 katika Madhabahu ya kitaifa ya Mama Maria huko Subukia nchini Kenya. Hata hivyo Kampeni iliyopewa jina  “tuvunje minyororo ya ufisadi" inahusiana na shughuli zote za elimu na sala!

Sala kwa ajili ya kupambana na ufisadi nchini Kenya

Katika fursa hiyo maaskofu mchini Kenya walitunga sala isemayo kuwa:Baba Yetu uliye mbinguni, daima utazame viumbe vyako, ili tuweze kushi kama ulivyo taka daima. Ulibariki nchi yetu Kenya, kwa  rasilimali kubwa ya kibinadamu na kiasili ili kuzitumia kwa njia ya heshima na utukufu wako na kwa ajili ya ustawi wa kila mkenya. Tunasikitishwa sana na utumiaji usio sahihi wa zawadi na baraka hizi kupitia ufisadi, na matokeo yake watu wetu wengi wana njaa, wagonjwa, wasio na makazi na waliorundikana, wanaodharauriwa na wasio na utetezi. Baba,ni wewe tu unaweza kutuponya na ugonjwa huu ambao unasababisha kifo. Tunakuomba kwa unyenyekevu, gusa maisha yetu na yale ya viongozi wetu ili tuweze kuelewa kuwa ufisadi ni mbaya na kufanya bidii zote ili kuutokomeza. Na kwa kila raia ambaye amepata kitu kwa njia ya ufisadi, Bwana, umpe roho ya ujasiri wa kurudisha bidhaa zilizoibiwa na kurudi kwako. Uwafanye viongozi wawe wenye kuogopa Mungu ili waweze kututunza na kutuongoza kwenye njia ya amani, haki, ustawi, maendeleo na zaidi ya upendo kwa wote.

SALA-MAASKOFU KENYA
06 November 2019, 15:31