Hali ya nchi ya Camerun eneo la lugha ya kingereza bado hawana amani kati yao ni ghasia na vurugu Hali ya nchi ya Camerun eneo la lugha ya kingereza bado hawana amani kati yao ni ghasia na vurugu 

Camerun:mivutano na ghasia katika wilaya ya Kaskazini inaendelea!

Baadhi ya maeneo yanaonesha kuacha ugomvi na ghasia lakini bado katika maeneo fulani fujo ni kubwa katika wilaya ya lugha ya kingereza nchini Camerun.Nguvu za madola jijini Yaoundé wameweka mfumo wa ukandamizaji ambao unawapiga watu vibaya sana.Na wanamgambo ambao hawako mbali na mji wa Bamenda wanajibu kwa ugumu ule ule na kusabisha hofu kubwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika wilaya ya lugha ya kingereza nchini Camerun ghasia bado zinaendelea. Hata kama baadhi ya maeneo yanaonesha kuacha ugomvi na ghasia lakini bado katika maeneo fujo ni kubwa. Nguvu za madola jijini Yaoundé wameweka mfumo wa ukandamizaji ambao unawapiga watu vibaya sana. Na wanamgambo ambao hawako mbali na mji wa Bamenda  wanajibu  kwa ugumu ule ule. Hakuna ustaarabu bali ni hofu tupu. Siku chache zilizopita huko Bambui karibu na Bamenda, mji mkuu wa Wilaya Kaskazini Mashariki, nyumba nyingi zimechomwa moto na mapigano ya kutumia silaha yalionekana. Watu wengi wameuwawa na Polisi wanaendelea kuwatishia watu hasa wazee ambao wanathibitisha kutokuwahi kuona suala la namna hii katika maisha yao. Hata hiyo ni kwa mjibu wa Mtawa mmoja kutoka Camerun akieleza ghasia nyingi zilizomo ndani ya nchi.

Miezi ya mwisho imeona matukio ya ghasia

Idadi ya watu sio kuwaogopa tu polisi, lakini pia wanamgambo wa kujitenga. Mbele yao watu wanawaogopa sana. Miezi ya mwisho imeona matukio mbali mbali hata ya kumteka nyara Padre. Jambo ambalo alilazimika Askofu Andrew Nkea Fuanya, wa  Mamfe, kufunga hata maparokia matatu ya jimbo lake na pia Askofu George wa jimbo la Kumbu alitekwa nyara. Na hiyo si  kwa viongozi wa kidini, lakini pia hata wa kiraia wanatekwa nyara kila siku na ili waweze kulipa fidia. Mvutano huo unazuia maendeleo ya maisha ya kijamii na kiuchumi katika wilaya. Kuendelea kwa mapigano ni chanzo cha kukwama kufanya shughuli za asasi za kiraia. Pia katika uwanja wa uchumi shida zinaongezeka kwani wafanyabiashara wengi wameacha kufanya kazi katika maeneo yao.  Wilaya hizo mbili maisha yake yaategemea kilimo ambapo sasa  kwenda shambani kulima kumekuwa vigumu, wakulima wengi waliuawa wakati wakiwa mashambani wanafanya kazi.

Uchaguzi wa rais na viongozi wa serikali 2020

Je uchaguzi wa rais na viongozi kwa 2020 utabadilisha hali hiyo?  katika swali hili Mtawa huyo anasema kuna mashaka kwani baadhi ya vyama vya siasa, kama vile Social Democratic Front, chenye muundo mkuu wa upinzaji, wamejiondoa. Kwa maana hiyo wanahofia kuwapo kwa udanganyifu wakati wa mchakato wa kupiga kura, pia kuogopa mlipuko wa ghasia. Kanisa Katoliki linaendelea kuhubiri kwamba vurugu haziwezi kuleta suluhisho chanya. Maaskofu wanaomba ufunguliwe mchakato wa mazungumzo ya pamoja kwa maana ya kwamba vyama vinavyogombea waweze kukabiliana bila ubaguzi na hukumu. Mbele ya vitisho vya kila wakati, hasa kwa upande wa vyama vilivyojitenga na Kanisa Katoliki wanatafuta kuwakaribia vijana na kuwafundisha thamani ya maisha.

26 November 2019, 16:40