Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland, Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019 limeadhimisha Siku ya Uhai Kitaifa kwakupinga nyanyaso na vipigo vya wanawake majumbani. Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland, Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019 limeadhimisha Siku ya Uhai Kitaifa kwakupinga nyanyaso na vipigo vya wanawake majumbani. 

Siku ya Uhai Kitaifa Ireland: Vipigo vya wanawake majumbani!

Ukatili wa majumbani ni jambo linaloharibu maisha ya kifamilia, kikanisa na kijamii. Familia inapaswa kuwa ni shule ya upendo, haki na amani; mahali ambapo watu wanajifunza kupenda na kupendwa; kusamehe na kusamehewa. Maaskofu wanasema, vipigo, nyanyaso na ukandamizaji wa aina yoyote ile ni mambo yanayokwenda kinyume cha utu, heshima na haki msingi za binadamu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland, Jumapili, tarehe 6 Oktoba 2019 limeadhimisha Siku ya Uhai Kitaifa, ili kupambana na nyanyaso na vipigo vya wanawake majumbani. Familia badala ya kuwa ni mahali pa faraja na kitulizo, zimegeuka kuwa ni mahali pa kuchumiana majanga badala ya kukuza na kudumisha amani na upendo. Ukatili wa majumbani ni jambo linaloharibu maisha ya kifamilia, kikanisa na kijamii. Familia inapaswa kuwa ni shule ya upendo, haki na amani; mahali ambapo watu wanajifunza kupenda na kupendwa; kusamehe na kusamehewa, lakini mambo ni kinyume kwa familia nyingi nchini Ireland Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland katika maadhimisho haya linasema, Familia iwe ni mahali ambapo watu wanapendana na kuhusiana vyema na jirani zao. Ili kufikia lengo hili kuna haja ya kubadili tabia na maisha kwa kujikita katika utu wema, upole na unyenyekevu.

Hii ni changamoto ya kuachana na tabia, mila na desturi zilizopitwa na wakati kwa kudhani kwamba, kipigo kwa wanawake ni dalili za upendo wa dhati! Vipigo na nyanyaso ndani ya familia nyingi zimesababisha watu kupoteza maisha na wengine hata kupata vilema vya kudumu. Maaskofu wanasema, wanawake wengi ndio waathirika wa vipigo vya majumbani, lakini hata katika baadhi ya familia, kuna wanaume wanaopata “mkong’oto wa nguvu kutoka kwa wenzi wao wa ndoa”, lakini wanaona aibu kutangaza masuala haya hadharani! Vipigo, nyanyaso na ukandamizaji wa aina yoyote ile ni mambo yanayokwenda kinyume cha utu, heshima na haki msingi za binadamu. Maaskofu wanawahamasisha waamini kuvunjilia mbali ukimya wa vipigo vya majumbani, ili kuanza kuvizungumzia na hatimaye, kuchukua hatua madhubuti, ili kuweza kuachana na tabia hii chafu katika maisha ya ndoa na familia!

Ukatili wa Majumbani

 

08 October 2019, 10:29