Tafuta

Vatican News
 Tarehe 8 Mei 2020 Mtakatifu Yohane Paulo II atakuwa anatimiza miaka 100 ya kuzaliwa. Tarehe 8 Mei 2020 Mtakatifu Yohane Paulo II atakuwa anatimiza miaka 100 ya kuzaliwa. 

Poland:mchakato wa kuwatangaza wenyeheri wazazi wa Mt.Yohane Paulo II

Jimbo Kuu la Cracow,limekubaliwa kwa upande wa Baraza la Maaskofu Poland kupeleka ombi katika Makao makuu ya kitume Vatican kwa ajili ya kuomba idhini ya kuanzisha mchakato wa kijimbo wa kuwatangaza wenyeheri,wazazi wa Mtakatifu Yohane Paulo,II baba yake Karol Wojtyla na mama yake Emilia Kaczorowska.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Mkutano wa 384  wa mwaka wa Baraza la Maaskofu nchini Poland uliofanyika tarehe 8 na 9 Oktoba 2019, maaskofu hao wamejadiliana mantiki nyingi kuhusu maadhimisho ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Karol Wojtyla (Mtakatifu Yohane Paulo II) itakayotimia kunako tarehe 8 Mei 2020. Vile vile Jimbo Kuu la Cracow, limekubaliwa kwa upande wa Baraza la Maaskofu wa nchi hiyo kupeleka ombi katika Makao makuu ya kitume Vatican  kwa ajili ya kuomba idhini ya kuanzisha mchakato wa kijimbo wa kuwatangaza wenyeheri, wazazi wa Mtakatifu Yohane Paulo, II baba yake  Karol Wojtyla na  Emilia Kaczorowska.

Mtakatifu Yohane Paulo II ni papa wa familia

Hakuna wasiwasi wowote kwamba tasaufi ya wakati endelevu wa Papa Mtakatifu Yohane Paulo II aliojiunda ndani ya familia, ni shukrani kubwa kwa sababu ya kurithishwa kwa imani ya wazazi wake, kwa mujibu wa maneno kutoka kwa Kardinali Stanislaw Dziwisz, aliyewahi kuwa katibu maalum wa Mtakatifu Yohane Paulo II. Aidha Kardinali Dziwisz ana uhakika kuwa, wazazi wa Mtakatifu Yohane Paulo II wameweza kuwa mfano wa kuigwa kwa familia za kisasa hasa kukumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye wakati wa maadhimisho ya kuwatangaza watakatifu alikuwa amempatia jina la Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa ni "papa wa familia". Mama yake Emilia Kaczorowska alifariki wakati Mtakatifu Yohane Paulo II akiwa na umri wa   miaka 9 tu. Na baba yake mwenye jina lake Karol, yeye alifariki kunako mwaka 1941 wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.

Papa kuwa msimamizi wa upatanisho kati ya wapoland na watu wa Ukraine

Hata hivyo katika mkutano wao wa mwaka pia wameunga mkono juu ya wazo la Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa msimamizi wa upatanisho kati ya wapoland na watu wa Ukraine, kwa sababu ya matokeo yaliyofuata kuhusu uhalifu wa kutisha wakati wa migogoro ya vita vya mwisho vya dunia. Vile maaskofu wanakubaliana kwamba Taalimungu ya majadiliano, ya mapatano na ya msamaha iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, yenye msingi wa thamani ya Injili imewezesha watu wa sehemu hizo mbili  kutimiza hatua muhimu katika njia ya maelewano na  majadiliano ya pamoja.

Misingi ya mada katika mkutano wao mkuu

Katika mada nyingi walizoweza kukabiliana nazo katika mkutano wao mkuu ni pamoja na makubaliano ya sheria mpya ya mafunzo ya makuhani, ambayo wanasema yanapaswa yaende sambamba na maelekezo kutoka Makao makuu ya Vatican, Mwezi Maalum wa Kimisionari, uchaguzi mkuu  wa tarehe 13 Oktoba na mapambano dhidi ya manyanyaso ya kijinsia katika Kanisa. Kadhalika wamejikita  kutazama kwenye Motu Proprio ya  “Vos estis lux mundi” ya Baba Mtakatifu Francisko,  ambapo maaskofu wameamua kuwasiliana na waathirika wa manyanyaso kwa kila jimbo ili kurahisisha na hata kwa kutumia mtandao wa moja kwa moja. Maaskofu pia wameanzisha Mfuko Maalum kwa lengo la kuwasaidia wathirika wa manyanyaso ya kijinsia katika jumuiya ya Kanisa.

Wito wa maaskofu wa kushiriki katika uchaguzi tarehe 13 Oktoba 2019

Kuhusiana na uchaguzi wa kisiasa, unaotarajiwa kufanyika nchini Poland Dominika tarehe 13 Oktoba 2019, maaskofu wamesisitiza umuhimu wa maadili ya kushiriki kupiga kura, kwa kutuma ujumbe wao unaowalenga wazalendo wote wa Poland siku chache zilizopita kwa mujibu wa  Rais wa Baraza la Maaskofu wa Poland Askofu Stanisław Gadecki.

11 October 2019, 15:30