Tafuta

     Kila tarehe 11 Oktoba 2019 Kanisa Katoliki linamkumbuka Mtakatifu Yohane XXIII,aliyekuwa anajulikana kwa walio wengi kuwa ni Papa mwema. Kila tarehe 11 Oktoba 2019 Kanisa Katoliki linamkumbuka Mtakatifu Yohane XXIII,aliyekuwa anajulikana kwa walio wengi kuwa ni Papa mwema. 

Mtakatifu Yohane XIII ni msimamizi,padre,kaka na rafiki!

Wakati wa mahubiri ya Askofu Mkuu Santo Morciano wa Jimbo la Kijeshi nchini Italia,kwenye Kanisa la Mtakatifu Maria wa Ara Coeli,Roma amesema kuwa kumchagua Mtakatifu Yohane XXIII kama msimamizi wa wanajeshi ni kuthibitisha jitihada za wanajeshi wa Italia na kujikita katika huduma ya amani kwa ujumla.Misa ilifanyika mkesha wa siku ya Mtakatifu huyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 10 Oktoba 2019 Askofu mkuu Santo Marcianò, wa Jimbo la Kijeshi nchini Italia , ameongoza Misa takatifu katika Kanisa la Maria Mtakatifu wa Ara Coeli, ikiwa ni fursa ya mkesha wa siku kuu ya Mtakatifu Yohane wa XXIII ambaye ni msimamizi wa Wajeshi ambayo Mama Kanisa anamkumbuka kila ifikapo tarehe 11 Oktoba. Wakati wa mahuburi yake kwa wanajeshi waliokuwa wameunganika ndani ya Kanisa hili zuri amekumbusha kuwa, siku ya Mtakatifu Yohane  wa XXIII ni sikukuu ya wanajeshi wote wa Italia  na ambao aliwasalimia kwa upendo mkubwa. Sikukuu yao kama wanajeshi na kama Kanisa wamekuwa wakiiadhimisha kwa kina mwaka baada ya mwaka. Mtakatifu Yohane XXIII alitangazwa kuwa msimamizi wao na pia kwa heshima yake wameita jina la Shule ya mafunzo ya  kijeshi ya  mapadre wao. Na kwa heshima yake, mwaka 2018, Askofu Mkuu  Marcianò, alitabaruku  Kanisa la Shama, huko nchini Lebanon na kuliweka chini ya usimamizi wa Mtakatifu Yohane XXIII

Mtakatifu Yohane XIII kwa hakika ni mmoja wao, ni rafiki tangu akiwa mwanajeshi, baadaye, padre msimamizi wa kikanisa cha wanajeshi na aliweza kuhudumia Kanisa amesema Askofu Mkuu Marcianò. Kumekuwapo na ukomavu wa uhusiano wao na na Mtakatifu huyo  na wakati huo huo kama inavyojitokesha kwa watu wapendwa ambao wanawakilisha mahali sehemu ya kuegemea katika mchakati safari ya wa maisha. Kipindi kinasaidia kuongeza nguvu ya uhusiano na kujikita kwa kina zaidi ya imani, kukua na kutafuta  kukaa pamoja. Aidha anasema  Askofu mkuu kwamba hawana hofu ya kuzungunza juu ya urafiki katika mantiki ya muungano wa Kanisa, watakatifu na zaidi kwa watakatifu wasimamizi, ambao ni wasindikizaji wa safari, wakihakikisha  uwepo wao na msaada… Kwa maana hiyo, Mtakatifu Yohane XXIII aweze kuwasaidia wanajeshi ili watambue kusoma hali halisi na ili wajibu kwa namna ya kweli katika wito wao wa kuhudumia Serikali, watu na amani. Aidha  amesema “Tunajua jinsi utume wenu usivyokuwa rahisi. Huduma ambayo nyinyi wanaume na wanawake wa Jeshi la Italia mmeitwa kutekeleza si rahisi, katika mazingira mbali mbali ya kihistoria, kisiasa na kijamii ambayo inawahusisha katika miji mikubwa au vituo vidogo, majengo ya maigizo, sinema kama ilivyo katika nafasi za usahihi wa hali ya juu ya kisayansi, kwenye dharura na majanga ya asili na katika nafasi za amri. Si rahisi kukabili haya yote, ukizingatia pia hali za kibinafsi na familia za kila mmoja; na sio rahisi, wakati huo huo, na kuweka macho wazi juu ya changamoto kubwa ambazo jamii inapendekeza na juu ya mahitaji halisi ya watu”.

Kufuatia na ishara hiyo ya urafiki wa kina na imani, Askofu Mkuu Marciano amesema ni bora kujaribu kuuliza Mtakatifu Yohane XIII, ili aweze kuwaangazia, kuwashauri, ni kwa jinsi gani ya kuishi kwa dhati na utulivu wa wito wao wa kuwa wanajeshi. Hata hivyo kama mchungaji na padre, amsema, angeweze kuwakabidhi bila shaka Neno la Mungu ambalo linatoa jibu kwa mchangao. Somo la kwanza kutoka Ezekieli (Ez 34,11-16), kwa hakika nabii Izekieli  anaonesha matatizo waliyokuwa wanaishi watu wa Israeli na ambayo yanaangazia hata historia nyingi za wakati wetu. Watu hao kama sisi sote, Mungu anawajibu kwa kutoa ahadi ambayo inahitaji kuiamini. Hawali ya yote sisi ni watu wahamiaji na  ambao wanaishi nje ya nchi yao na katikati ya watu wengine. Historiaa nyingi leo hii, za watu wanaishi katika uhamishoni na wanalazimishwa kukimbia nchi zao; na mara nyingi hali halisi yao utafikiri siyo tena nchi, na nyumba siyo nyumba tena. Askofu  Morciano amefikiria watu wanaokumbwa  na ghasisa na vita, hasa vile ambavyo vimesahulika; watu masikini wanaotiliwa vigezo na Nchi tajiri; mataifa yaliyotiwa sumu ya ghasia na vita vya mauaji; watu ambao hawajawahi kujua uhuru wa mawazo, maneno na uchaguzi na ambao wanajikuta wakinyamazishwa na nguvu za kizamanai na udikteta mpya…  Kadhalika amefikiria  hali nyingi ambazo zipo karibu sana  na ambazo Serikali haijishughulishi kwa wazalendo wake na hata namna yao ya kuishi, ya ulinzii wa haki msingi kama vile maisha, utunzaji au hadhi ya kazi, Nchi ambazo hakuna usawa na ustawi kwa manufaa ya pamoja, haki na amani.

Watu hao wote Mungu anatoa ahadi ya kuwa na nyumba na ahadi ya malisho, chakula, kama walivyoimba katika zaburi ya 22 (23). Mungu anatoa ahadi ya kuwatuma watu waweze kulinda haki, sheria, haki za watu, kuwashibisha wanye njaa na kuhamasisha ustawi wa wema wa wote, katika kulinda maisha na hadhi ya kibinadamu. Mungu anatoa ahadi ya kuwa na mchungaji kama ilivyotokea ya Mtakatifu Yohane XXIII. Yeye alijua vita, aliishi vita  akiwa mstari wa mbele kama askari na msimizi wa Kanisa dogo la kijeshi, Yeye alikubali kuanza utume wake mbali na nchi yake, kati ya watu wa tamaduni na dini mbalimbali nchini Bulgaria na Uturuki ,mahalia ambapo alipewa shughuli ya kuwa Balozi wa Kitume  wa Vatican katika nchi hizo. Wakati huo wakristo walikuwa ni wachache sana na aliweza kuwaelewa na kuwasindikiza, ambao kwake yeye walikuwa kama wageni.

Mungu anahaidi watu hawa kwamba atawakusanya pamoja. Hiyo itakuwa “mwili mmoja,” anasema Paulo katika barua yake ya pili (Efe 4: 1-7.11-13). Ni picha nzuri, ambayo Kanisa hutumia kuelezea ushirikiano kati ya watu tofauti, kati ya kazi tofauti na sauti; umoja muhimu, kama mwili ambao muhimili, ni muhimu na ambao ustawi wake unahitaji ustawi wa kila kiungo. Ulimwengu wa kijeshi pia hutumia picha hii muhimu ya  kuwa “mwili”, “familia” moja na Mtakatifu Yohana XIII anawafundisha  sanaa. Yeye alitambua kujifanya kaka na baba hata kwa wasiokuwa wakristo, wafungwa, wagonjwa, masikini na wenye nguvu. Alitambua kushinda migogoro mikubwa ya kihistoria kwa njia ya kujenga madaraja rahisi kwa kutumia majadiliano na ambapo baadaye ikawa picha nzuri, ya kweli ya amani. Kumchagua kama Msimamizi, wao wamethibitisha jitihada zile za wanajeshi wa Italia ambazo wanatoa huduma ya amani, uhamasishaji wa mazungumzo na ulinzi wa kila mtu, lakini pia ule umakini na utunzaji wa kuweza kuweka hali ya utulivu….  Ni hali ambayo kwa hakika ni misingi na jitihada ambazo ni kuu zaidi hasa uhusiano uliopo wa mapadre wasimamizi wa vikanisa vya kijeshi, ambao si tu kwa ajili ya huduma yao binafsi, lakini hata kwa ajili ya familia zao,muungano wa upendo uliopo katika Kanisa.

Jibu la Mungu ni huruma ni ile ya kutuza, kubeba hali zote kama anavyofanya mchungaji wa zizi. Siyo rahisi na wakati mwingine watu wanakuwa na vurugu na ghasia ni wagumu na ndiyo hao hao wanaohitaji msaada mkubwa. Amemtaja Baba Mtakatifu Francisko, siku moja alipokutana na wafungwa alisema iwapo hujikuta katika hali hiyo, labda hukuishi maisha yaliyo rahisi, katika familia yenye umoja kwa sababu wamepokea upendo… Jibu la Mungu linajikita katika ukaribu, ili kukomboa uhusiano binafsi na uhusiano na Kristo. Wewe u-pamoja nami inasema Zaburi, ( Wewe ni Kristo”  anasema Petro(Mt 16,13-19). Mazungumzo ya Yesu na Petro ambaye alimkana, yanashangaza, kwa maaana  Yesu Petro anamwambia “ wewe ni Kristo”, na Yesu pia anamwambia, “Wewe ni Petro”, majibu ni mzizi wa utakatifu. Katika nyakati za giza, ya historia, Mungu mara nyingi hutoa watakatifu, hutoa wachungaji ambao wanasindikiza zizi. Na picha ya mchugaji siyo kwa bahati mbaya; katika utamaduni wa kiyahudi, mchungaji ni yule ambaye anaishi kwa ajili ya wokovu wa zizi na kwa maana hiyo anakabiliana na hatari ngumu, hadi kufikia kupoteza maisha yake. Ni zawadi ya wanajeshi wengi kuwapo duniani, huku wakiendeleza historia kuwa tajiri zaidi ya upendo, kujitoa sadaka, na  utakatifu. Utakatifu ule ambao Mtakatifu Yohane XIII anaendeleza na kuwasindikiza kama msimamizi, padre, kaka na rafiki.

 

11 October 2019, 11:08