Tafuta

Vatican News
 Padre Michael Maingi Kyengo wa Jimbo la Machakos nchini Kenya aliyekuwa amepotea tangu tarehe 8 Oktoba amepatikana ameuwawa Padre Michael Maingi Kyengo wa Jimbo la Machakos nchini Kenya aliyekuwa amepotea tangu tarehe 8 Oktoba amepatikana ameuwawa   (AFP or licensors)

Kenya:ameuwawa Padre Michael Maingi Kyengo

Ni Padre Michael Maingi Kyengo,wa miaka 43 aliyekuwa anatoa huduma katika Parokia ya Thatha,Jimbo Katoliki la Machakos nchini Kenya ambaye aliuwawa baada ya kuporwa mali zake amepatikana

Mwili wa padre Michael Maingi Kyengo, Paroko msaidizi wa  parokia ya Thatha, jimbo Katoliki la Machakos nchini  Kenya aliyekuwa ametekwa nyara tangu tarehe 8 Oktoba amekutwa amezikwa karibu na mto wa Mashamba huko Makima, karibu na   Embu.  Habari kutoka katika Shirika la Habari za kimisionari Fides zinasema Padre Kyengo, mwenye umri wa miaka 43 alionekana mara ya mwisho tarehe 8 Oktoba. Na tarehe 11 wanafamilia wake walikwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kupotea kwake.

Hata hivyo kuhusiana na upelelezi zaidi umefanywa na kugunduliwa mshukiwa kutokana na kushikwa kwa simu ya mkono, gari na kadi ya Benki ya padre  huyo aliyekuwa amepotea. Baada ya kumweka mbaloni huyo mtu, amewapeleka polisi hadi mahali mbapo wamekuta mwili wa Padre Kyengo. Upelelezi huo unabainisha kwamba muuaji huyo alimkaba kwanza na baadaye akamkata koo. Kijana huyo aliyekamatwa ni Michael Muthini Mutunga, mwenye umri wa miaka  25 na ambaye wanasema hakuwa peke yake bali na watu wengine ambao kwa sasa wanatafutwa! Padre Kyengo alikuwa amepewa daraja la Upadre kunako mwaka 2012  na tangu wakati huo alikuwa anatoa huduma ya kikuhani katika parokia ya Thatha nchini Kenya.

18 October 2019, 16:08