Vatican News
Askofu wa Colombia aingia katika ukumbi wa Mkutanoa kama hasiyekuwa na makazi Askofu wa Colombia aingia katika ukumbi wa Mkutanoa kama hasiyekuwa na makazi 

Colombia:Askofu ajifanya asiye na makazi katika mkutano!

Askofu Callosi Quintero Colombia anaelezea juu ya uzoefu wake wa kusubiriwa kwa muda mrefu katika Mkutano wa Kichungaji-kijamii na akafika akiwa kama hasiye kuwa na makazi.Hakutambuliwa au kukaribishwa na wala kusemezana na yoyote.Anathibitisha kuhisi upweke ndani ya moyo,kutelekezwa na sintofahamu za watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Mkutano wa Kichungaji- jamii uliofanyika hivi karibuni katika Jimbo la Armenia, huko Quindío nchini Colombia, washiriki walibaki wakimsubiri Askofu wao na badala yake, Askofu akajifanya asubiri yeye. Askofu Callosi Quintero alifika katika ukumbi wa mkutano akiwa amevaa nguo chakavu kama vile za mtu asiye kuwa na makazi, alipoingia akasababisha aibu hata usumbufu kwa  wale waliokuwepo. Na mwingine aliamua hata kuondoka kutoka katika ukumbi! Mtu huyo mwenye nguo chakavu hasiye kuwa na makazi alipoingia  ajifanya kunza kukaa hapa na pale,huku akizunguka na mara kadhaa alijikwaa lakini  bila mtu yeyote kumsaidia ... Halafu, kwa kushangaza, alichukua hatua ya kupanda kwenye jukwaa la watoa mada … na ndipo alijifunua na kuonekana utambulisho wake wa kweli!

Askofu kujifanya hasiye makazi

Hili ni jambo zaidi ya kichocheo, hasa matendo ya kuonesha kwamba mtazamo wa Kanisa unapaswa uwe wa kimasikini na kwa ajili ya masikini. Hili ni wazo ambalo limekomaa kwa muda mrefu yaani tendo la kujificha ndani ya mtu kama masikini. Aidha ni tendo ambalo limekuwa na mwangwi mkubwa kwa waandishi wa magazetu na vyombo vya habari kwa sababu haijawali kutokea kusika kwamba Askofu anachukua hatua ya  kufanya uchaguzi kama huo, kuhutumia kamba mbinu ya huduma yake ya kutangaza Injili. Lakini alifanya hivyo makusudi ili kuonesha kwamba Neno la Injili ni hai, hasa  kwa kile ambacho Yesu alisema, hata sasa anaendelea kusema ( nilikuwa mgeni hamkunikaribisha...). Ni Askofu Quintero, mwenye umri wa miaka 50  ambaye karibu ni mwaka mmoja  tangu kuanza kuongoza Jimbo ambalo liko Colombia Mashariki. Ni eneo linalojulikana kwa wakulima wa kahawa, pia ni eneo la kitalii sana linaoonesha uwanda mzuri, japokuwa kwa bahati mbaya ni moja kati ya eneo masikini sana katika nchi za Amerika ya Kusini.

Wazo la Askofu ni la siku nyingi 

Askofu Quintero akihojiwa na waandishi wa Gazeti Katoliki la Sir kuhusiana na tukio hili amethibitisha ukweli wa wazo  hilo ambalo anasema alikuwa nalo kwa kipindi kirefu na kwamba hata kabla ya kuwa Askofu. Nia yake ilikuwa ni kutaka kuona ukweli wa hisia ipi kwa watu wanapomwona masikini, au asiye kuwa na makazi anaingia kanisani au katika ofisi, hivyo alikuwa anasubiri siku moja apate fursa hiyo. Kwa bahati nzuri fursa hiyo ilipatikana katika  Mkutano wa Kichungaji katika Jimbo lake. Askofu aidha ameelezea kuwa hiyo ni sekta ambayo mwenyewe yuko makini sana na ambayo amewaomba wanaparokia na wahudumu wote wa sekta mbalimbali za kijamii katika jimbo lake  waweze kusaidia walio maskini zaidi. Na “hata hivyo mtazamo wetu wa Kanisa unapaswa kuanzia na maskini na kwa ajili ya umasikini, kama ilivyo msimsitizo wa kila mara wa Baba Mtakatifu Francisko” amesisitiza Askofu Quintero.  

Nilifika mapema kujiandaa na mkutano huo

Akiendelea na ushuhuda wa uzoefu wa kuwa kama hasiye kuwa na makazi amesema, “Nilifika mapema nyuma ya ukumbi wa mkutano na kuanza maandalizi ya uvaaji wa mavazii, kwa kusaidiwa na kikundi cha “tamasha la sanaa za  michezo  la ‘Versión Libre Teatro’. Hata hivyo ameongeza kusema . “ni watu wachache walikuwa wanajua nia hiyo na ndipo niliingia katika ukumbi, askofu  mahali ambamo wote walikuwa wanasubiri kufanya mkutano”. Askofu Quintero akisimulia hisia gani alipata alivyoingia ukumbi wa mkutano amesema, “ Nilihisi kutojaliwa kwenye ngozi yangu. Tangu mwanzo nilijaribu kujitambulisha kwa mtu ambaye nilikuwa namwakilisha. Na lazima niseme kwamba nilionja huzuni mkubwa na upweke wa ndani. Mara kadhaa nilikataliwa na wale waliokuwepo, wengi walikuwa na aibu na wengine walihisi usumbufu. Kiukweli hakuna mtu aliyenitendea vibaya, lakini nimehisi katika ngozi yangu, kutelekezwa sana na kuona sintofahamu. Ikiwa ninataka kusema kwa neno moja la uzoefu nilioufanya ni ule wa sintofahamu ya kweli. Hakuna aliyeniita, hakuna aliye semezana nami. Nilielewa kwa kina ule upweke wa watu ambao wanajikuta katika hali kama hii! Amethibitisha Askofu Quintero.

Je baada ya Askofu kujionesha utambulisho wake

Askofu Quintero ameelezea pia mara baada ya kujitambulisha kwake jukwaani kuwa: “Wengi walishangaa sana, wengine hata  kutoa pongezi. Lakini, ninaamini kwamba wote lazima kutambua kuwa ni mwaliko wa kufanya tafakari, hasa ya uongofu. Lengo lilikuwa ni kutoa chachu mpya kwa waamini kuwa na hisia kubwa hasa ya  kijamii. Aidha ameongeza kusema kuwa: “Uzoefu huo uliruhusu kuzungumza mada ya ukosefu wa haki kijamii na hali halisi ya watu wasiokuwa na makazi. Kila mtu masikini ana talanta na anaweza kupeleka mchango wake muhimu katika jamii. Kadhalika ni muhimu sana kupeleka imani barabarani, kuingia katika mawasiliano  na watu ambao ni masikini zaidi. Vile vile mada hizi zinataka kuendelezwa, lakini zaidi, bila kuangukia katika suala la utunzaji tu,  badala yake ni kuwasaidia watu waweze kuondakana na hali halisi ngumu na hatimaye waweze kutambea kwa miguu yao.

Umasikini na ukosefu wa usalama

Askofu Quintero akielezea hali halisi ya eneo la Jimbo lake amesema kuwa, kwa bahati mbaya katika jimbo lake, umasikini na ukosefu wa usalama na kama ilivyo  hata idadi kubwa ya watu wanaoishi barabarani inazidi kuongezeka, kwa maana hiyo katika jimbo lao wanao mpango fulani kwa ajili ya kujikita kukabiliana na changamoto hiyo.

 

10 October 2019, 13:59