Tafuta

Vatican News
Visa vya vurugu na uporaji vimeendelea nchini Chile katika siku ya tatu ya ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo na kusababisha vifo vya  watu 12 Visa vya vurugu na uporaji vimeendelea nchini Chile katika siku ya tatu ya ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 12  (AFP or licensors)

CHILE:kuna waathirika zaidi katika maandamano dhidi ya maisha magumu!

Visa vya vurugu na uporaji vimeendelea nchini Chile katika siku ya tatu ya ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo na kusababisha watu 12 kuwawa na karibia 1500 wameshikiliwa mbaroni,kati yao 650 ni wa Santiago ya Chile.Askofu Msaidizi Alberto Lorenzelli wa Santiago anasema ni kipindi kigumu cha ghasia na kutumia nguvu.

Na Sr. Angela  Rwezaula – Vatican

Siku ya tatu mfululizo tangu Jumapili 20 Oktoba za vurugu na  mlipuko wa moto huko Santiago ya Chile, mahali ambapo maandamano  yanaendelea kuhusu maisha magumu na ambapo wanathibitisha hadi sasa  kuwawa kwa watu 12 wakati wa tukio hayo ya maandamano na uporaji katika maeneo tofauti ya Santiago. Ni hali ya kutia wasiwasi mkubwa ambao haupungui. Maandamano ya amani yamegeuka kuwa mabaya katika la Irarrazaval, ambayo yameunganisha na watu wengine katika eneo la Plaza Italia nchini humo. Mwathirika wa kwanza ameuwawa na lori moja karibu na mji wa Talcahuano.

Huko Santiago ya Chile hali ni ngumu

Wanaume watano wamekufa kwenye moto uliolipuka katika kiwanda cha kusuka vitambaa na wanne katika Supermarke, pia watu wawili katika duka la kutengeza vifaa vya ujenzi. Meya wa mji mkuu wa Santiago ya Chile Cile, Karla Rubilar,  amesema kuwa hata kama ni siku  ngumu, lakini watu wanaweza kurudi kuzunguka kawaida. Tarehe 21Oktoba, matawi kadhaa ya benki yalifunguliwa tena katika sehemu ya mashariki mwa mji mkuu wa Chile, wakati maduka makubwa yamefungwa na watu wachache wanasafiri kwenda mjini, hasa baada ya shughuli za kielimu kusitishwa katika eneo la mji mkuu wa Santiago

Amnesty inaomba kuheshimiwa kwa haki za binadamu, kufuatia na kukamatwa watu kwa wingi

Karibu watu 1,500 wamekamatwa, kati yao 650 ni wa kutoka mji wa  Santiago ya Chile. Katika suala hili, Amnesty International imemhimiza Rais wa Chile Sebastian Pinera kuhakikisha kuwa anaheshimu haki za binadamu wakati wa hali ya dharura, wakisisitiza kwamba uamuzi huu, ambao wanategemea vikosi vyenye silaha kudumisha utulivu wa umma, badala ya kuongeza  hatari tu za ukiukwaji. Pinera, tarehe 21 Okotba alikuwa amesema kwamba nchi hiyo iko vitani dhidi ya adui mwenye nguvu isiyowezekana na ambaye haheshimu chochote au  mtu yeyote.

Askofu Albertelli: mivutano ni mingi ya kijamii na watu wamechoka

 Naye Askofu Msaidizi wa Santiako Alberto Lorenzelli, amesema ni kipindi kigumi kinachoonesha vurugu na kufikiri kidogo. Kina mivutano ya kijamii ambayo inapaswa ieleweke lakini hiyo siyo njia kwa sababu hali inazidi kuwa ngumu na watu wamechoka. Hata hivyo taarifa zaidi ni kwamba waandamanaji nchini Chile wamekasirishwa na kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha, hali iliyochochewa baada ya serikali kupandisha nauli ya basi nchini humo. Licha ya serikali kutangaza kuondoa nyongeza hiyo, waandamanaji wenye hasira wameendelea kupambana na maafisa wa usalama katika jiji kuu Santiago na miji mingine. Kiwanda cha kutengeza nguo kimevamiwa na waandamanaji, ambao wamepora bidhaa na kukiteketeza kwa moto.

Rais anawanyoshea kidole maadui zake

Wakati huo huo Rais wa Chile Sebastian Piñera amenyooshea kidole cha lawama maadui zake akisema, mambo yameeleweka: nchi iko vitani. Katika siku mbili kwanza serikali ya Chile ilikuwa imetamgaza hatua ya kutotoka nje usiku katika mji wa Santiago. kuanzaia saa moja usiku hadi saa kumi mbili asubuhi. Wakati huo huo, hali ya dharura ilitangazwa katika Majimbo matano, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wenye wakaazi milioni 7. Demokrasia ina jukumu la kujilinda,"Rais wa Chile Sebastian Piñera alisema akitetea hatua hizi za dharura, baada ya mkutano na spika wa Baraza la wawakilishi, rais wa Bunge la Seneti na Seneti na rais wa Mahakama kuu. Na kwa maana hiyo baadaye rais Sebastian Piñera alizungumza mbele ya waandishi wa habari na kusema “Tuko vitani na adui mwenye nguvu, ambaye haheshimu chochote wala mtu na ambaye yuko tayari kutumia vurugu na machafuko mengine bila kikomo.” 

Wakazi walipewa taarifa mapema wawe na utulivu ndani ya nyumba zao

Jenerali Javier Iturriaga, ambaye alipewa majukumu ya kusimamia usalama wa umma na Rais Piñera Ijumaa 18 Oktoba 2019 alikuwa amewataka wakaazi kuwa watulivu na wasiondoke katika makaazi yao. Hata hivyo machafuko mabaya ambayo hayajawahi kutokea nchini Chile kwa miongo kadhaa, yaliendelea hata siku ya Jumapili  20 Okotba 2019 nchi humo. Makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yalitokea katika eneo la Plaza Italia, katikati mwa mji wa Santiago, ambapo polisi walijibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. Na wakati huo huo, visa vya uporaji vilishuhudiwa katika sehemu kadhaa za mji mkuu.

22 October 2019, 15:37