Tafuta

Morocco: Heshima za utu ni nyenzo muhimu katika kupambana na biashara ya binadamu, na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.  Morocco: Heshima za utu ni nyenzo muhimu katika kupambana na biashara ya binadamu, na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.  

Askofu Mkuu Gallagher asema; Biashara ya binadamu idhibitiwe!

Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo OSCE: limeanza kupambana vikali katika kuliwanda wanyonge dhidi ya biashara ya binadamu na kumlinda mwathirika na mitindo mbalimbali ya nyanyaso. Linahamasisha heshima za utu kama nyenzo za ki-jamii dhidi ya biashara hii ya utumwa na kuna umuhimu wa mchango wa jamii za kisiasa vikiwemo vyama vya kidini.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican katika mahusiano ya kimataifa, amelitaka Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE kudhibiti biashara ya binadamu hususani kwa wakimbizi, waliosetwa na walioko hatarini kutengwa na jamii. Akitoa mada katika mkutano wa Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE Askofu mkuu Paul Richard Gallagher amesema, biashara ya binadamu ni jeraha kubwa katika heshima na utu wa mwanadamu unaolindwa na haki za binadamu na ni changamoto katika uwanja wa uinjilishaji. Akinukuu katika ujumbe uliotolewa na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 2 Februari 2019 amesema, hata kama bishara ya binadamu itapuuzwa lakini uhalisia na madhara ya utumwa huu hatuwezi kuyaepuka na pengine kwa wakati huu ndiyo umepamba moto zaidi ya vipindi vingine vya kihistoria. Vita dhidi ya biashara ya binadamu ni jukumu la OSCE na Vatican inaunga mkono  maamuzi na jitihada zilizotolewa na sharia ya utawala wa jamii kubwa za wahamiaji na wakimbizi MC katika kulinda na kupambana na biashara ya binadamu wakiwemo kundi la vijana wadogo wasio na ulinzi.

 Nchi zote 57 wanachama wa OSCE zimeanza kupambana vikali katika kuliwanda wanyonge dhidi ya biashara ya binadamu na kiini cha mapambano hayo ikiwa ni kumlinda mwathirika na mitindo mbalimbali ya nyanyaso na kuhamasisha heshima za utu kama nyenzo zinazoongoza jamii dhidi ya biashara hii ya utumwa. Maamuzi hayo pia yalitambua umuhimu wa mchango wa jamii za kisiasa vikiwemo vyama vya kidini katika kupambana na vita hiyo. Aidha Vatican inatambua pia mchango mkubwa uliotolewa na umoja wa Mataifa katika kulijengea uwezo Shirikisho la la Ushirikiano wa kimataifa, usalama na maendelao na kuliomba kutoa kipaumbele kwa makundi ya wahamiaji, wakimbizi na waliosetwa na jamii. Hii kiwemo pamoja na haki ya kuishi, utawala wa sharia, uhuru wa dini na haki kwa wote katika familia.  Pamoja na hayo Vatikani imetoa mapendekezo yake kuwa; nchi wanachama waendele kuchakata namna ya kushughulikia masuala ya wahamiaji na kuweka mifumo inayopinga biashara haramu ya binadamu. Kitengo kinachohusika na uchaguzi kihusishe jamii ya za kisiasa na wadau kutoka mashirika mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.   

03 October 2019, 14:33